Kuna anayejua Pesa za Kodi, Tozo, Misaada na Mikopo zinakwenda wapi?

Tembelea hapo Mkuu Kuna source

Tanzania walipa Kodi wanaotambulika Tra ni milioni 2.2 tu, hata ukitoa watoto na wazee Kuna watu zaidi ya milioni 20 Wanapaswa kulipa kodi,

Mfano Kenya wanaolipa kodi ni milioni 5.5 na Sisi tupo wengi kushinda wao.
Siyo kweli labda useme wenye TIN number. Kodi karibia kila mtu hulipia labda mfumo ndo haujakaa sawa. Kwenye bidhaa wanalipia, betting huko ndo usiseme kila siku wanalipia, mafuta ukinunua wanalipia kodi tayari. Unasemaje ni mil.2 ndo walipa kodi?
 
Unapobet Hela imetoka kwako ila kimahesabu Mmiliki wa betting ndio amelipa Kodi.
 
Hizo hazihesabiki, nazungumzia walipa Kodi wenye Tin numbers wanaotambulika Tra,
Tozo ni aina Nyengine ya makusanyo
Sasa hapo unakosea. Mlipaji kodi mkubwa huenda kumzid mwenye tin number ni hawa wanunuz wa mafuta. Kila akipita kituo cha mafuta akajaza kalipa kodi huyo.
 
Hao wanaotia mafuta hela zao wanapata wapi? Sababu anaelipa kodi hapo ni mwenye kituo cha mafuta. Imeingia kodi ya Mtu mmoja,

Huyo anaejaza mafuta Sasa sehemu anayoingizia Kipato amelipa Kodi?
 
Unapobet Hela imetoka kwako ila kimahesabu Mmiliki wa betting ndio amelipa Kodi.
Ndo kukosa weledi huko. Mi nibet nitoe hela yangu na 15% ama 10% inasoma ni TAX halafu mmiliki ndo asomeke kalipa kodi. Mmiliki yeye anayo tin number ambayo inamlazimisha kulipa kodi kila mwezi na ni fixed amount iliyokadiriwa na TRA ila anayebet ya kwake ni moja kwa moja inasomeka TRA.
 
Hao wanaotia mafuta hela zao wanapata wapi? Sababu anaelipa kodi hapo ni mwenye kituo cha mafuta. Imeingia kodi ya Mtu mmoja,

Huyo anaejaza mafuta Sasa sehemu anayoingizia Kipato amelipa Kodi?
Basi hii nchi haiko systematically. Mwenye kituo kila mwezi analipa kodi fixed amount au ina vary kulingana na mauzo? Kama ina vary lazma umhesabie mtumiaji kuwa nae analipa ndo maana bei inakuja ikihusisha na kodi humo humo na mlipaji ni huyo mlaji.
 
Ndo kukosa weledi huko. Mi nibet nitoe hela yangu na 15% ama 10% inasoma ni TAX halafu mmiliki ndo asomeke kalipa kodi. Mmiliki yeye anayo tin number ambayo inamlazimisha kulipa kodi kila mwezi na ni fixed amount iliyokadiriwa na TRA ila anayebet ya kwake ni moja kwa moja inasomeka TRA.
So what Next? Bakhresa sio Tajiri sababu umetoa hela yako kununua Bidhaa yake?

Huyo alietoa hela Kubeti chanzo alichotumia kupata hela Amelipa Kodi? Ukifikiria kwa muono huo ndio utaelewa kwanini walipa kodi ni milioni 2.
 
Basi hii nchi haiko systematically. Mwenye kituo kila mwezi analipa kodi fixed amount au ina vary kulingana na mauzo? Kama ina vary lazma umhesabie mtumiaji kuwa nae analipa ndo maana bei inakuja ikihusisha na kodi humo humo na mlipaji ni huyo mlaji.
Analipa kodi kutokana na mzigo alioingiza, na wewe Umelipa hela aliopanga yeye kwenye sheli yake, yeye ndo anatoa kodi sio wewe.

We una biashara hulipi kodi, then ujaze mafuta ujihesabu umelipa kodi?
 
So what Next? Bakhresa sio Tajiri sababu umetoa hela yako kununua Bidhaa yake?

Huyo alietoa hela Kubeti chanzo alichotumia kupata hela Amelipa Kodi? Ukifikiria kwa muono huo ndio utaelewa kwanini walipa kodi ni milioni 2.
Kwa hiyo tafsiri yako unataka ili uitwe mlipa kodi lazima uwe na TIN uwe unailipia directly whether una biashara au huna ila ukienda kudai risit ya malipo kwa muuzaji we siyo mlipa kodi?
 
Hela zooote hizo zikikusanywa Hazitoshi hata budget yetu kujitegemea wenyewe, tuna tegemea wafadhili watuongezee

Nchi ina watu zaidi ya milioni 60, milioni 2 tu ndo walipakodi, hizo hela unazoona ni nyingi Hazitoshi hata kidogo.

Tra wanakusanya Around Trilioni 1, kwa mwaka ni kama Trilioni 18, Hapo Kuna Trilioni 6 mishahara na Trilioni 7 deni la Taifa, hapo Tayari umekaribia kumaliza hela yote

Bado Kuna Miradi ya Matrilioni ya Hela karibia 20 na matumizi mengine yasiyo Mishahara ya Serikali Takriban Trilioni 4.

Kasome budget yako mambo yote yameelezewa

haya uongo uongo mwingiii
 
Analipa kodi kutokana na mzigo alioingiza, na wewe Umelipa hela aliopanga yeye kwenye sheli yake, yeye ndo anatoa kodi sio wewe.

We una biashara hulipi kodi, then ujaze mafuta ujihesabu umelipa kodi?
Niulize vizuri, nini tafsiri ya utolewaji wa risit za kielectroniki unapoenda kununua mafuta au bidhaa nyingine? Ili kodi ije mwisho wa mwezi ile ya halali au yeye anakuwa ameshalipa kodi kabla hata ya mauzo ya mafuta yake kuuzwa kwa walaji?
 
Mfano amenunua bidhaa China 5000 akifika bandarini analipa kodi, na Tozo nyengine

Then anakuja kukuuzia bidhaa wewe 10000 kwa faida ya 2000 basi hapo halipi tena kodi yote sababu alishalipa mwanzo, ataongeza tu kodi kidogo kwa faida aliyopata toka kwako.
 
haya uongo uongo mwingiii
Waongo sana. Eti walipa kodi ni milion 2, huku mitaani wanapita kila siku wale watoza ushuru. Migodini, ziwani, kodi hadi kwenye maji na umeme ila wao wanahesabu wenye TIN 😁😁
 
Jaribu kwanza kuangalia hali ya nchi. Angalia ni miradi ambayo inatakiwa ijengwe, angalia ghalama za io miradi. Angalia ghalama za mishaara ya watumishi, angalia pia ghalama za uendeshaji wa taasisi za serikali.

We huoni nchi kama Marekani tayari ina miundombinu yote na bado bajeti yake ni kubwa kila mwaka! Uendeshaji
 
Mfano amenunua bidhaa China 5000 akifika bandarini analipa kodi, na Tozo nyengine

Then anakuja kukuuzia bidhaa wewe 10000 kwa faida ya 2000 basi hapo halipi tena kodi yote sababu alishalipa mwanzo, ataongeza tu kodi kidogo kwa faida aliyopata toka kwako.
😂😂😂 sa tunasumbuana kudai risit za EFD mashine ili iweje kama kodi ilishalipwa kitambo, tujue faida yake ama? Hapo hujanishawishi. Umeme ukinunua LUKU si kuna TAX unasemaje silipi kodi hadi niwe na TIN? napo TANESCO wanakuwa wameshalipa bandarini kinachobaki ni ni faida yao? We huna utashi na mambo ya TAX yanavyoenda kalia kusema TIN tu. Miamala ya kifedha ikiongezeka ujue kodi pia imeongezeka sa unasemaje TIN number
 
Waongo sana. Eti walipa kodi ni milion 2, huku mitaani wanapita kila siku wale watoza ushuru. Migodini, ziwani, kodi hadi kwenye maji na umeme ila wao wanahesabu wenye TIN 😁😁
waongo sio wa kuwaamini
 
Back
Top Bottom