Kuna anayejua Pesa za Kodi, Tozo, Misaada na Mikopo zinakwenda wapi?

Kuna anayejua Pesa za Kodi, Tozo, Misaada na Mikopo zinakwenda wapi?

Watakuonyesha madarasa ya misaada ya covid
 
Moja inagharamia usajii na malipo ya wachezaji wa timu singida, nyingine zinaenda kujenga Zanzibar, gharama za safari za kufungua nchi mengine mtajazia
 
Tatizo wengi wa hao wapo informal sector, ila wanalipa Kodi indirect nyingi tu mfano hawana account za benki ila wanakatwa Kodi kwenye miamala ya M pesa. Hawakatwi PAYEE ila wanakatwa tozo mbali mbali kwenye biashara na ujasiriamali wanaofanya.

Hao Kenya walichofanya ni kuformalise kazi nyingi mpaka wanaochomelea na kuuza vyuma chakavu Wana trade unions zao na wanakatwa Kodi which in turn Tanzania wapo ila hawajawa formalized tu.

Na kingine uwezo wa kukusanya Kodi sio kuongeza namba ya walipa Kodi ILA ni kuongeza Volume ya malipo ya Kodi. Unaweza wasamehe makapuku million 2 ila ukabana biashara kubwa 100 tu zikafidia!! So kudhani kwamba muuza mishkaki akitoa Kodi ndio kutapandisha mapato ni kujidanganya kama hatutoweza kumaximise Kodi hasa kwenye investments kubwa.
Sheria ya Nchi ipo wazi ukiwa unaingiza zaidi ya milioni 4 Tra inakuhusu.

Mimi ni Mfanyabiashara kuweka mambo sawa kusema Kubana biashara 100 kubwa huo ndo upuuzi wenyewe ninaoongelea hapa, kwanini walipe wachache kodi halafu wengine wasilipe? What so special kuhusu hao wengine? Hawatembei barabarani, hawaendi hospital? Hawapeleki watoto shule? Kwanini kikundi kidogo kihudumie nchi Nzima na wengine wale Bata?

Tunaishi nchi ambayo Machinga anauza begi moja 200,000 ana mabegi zaidi ya 100 na store 3, Machinga anauza sufuria hadi 80,000 kazi panga ndefu kama minara, kawaida kabisa kukuta Machinga anauza mamia ya mamilioni ya bidhaa kwa mwaka.

Kariakoo kila siku maduka yanageuka Magodown biashara zote ni za Machinga, so unahisi solution sio kuongeza wigo wa walipa kodi Bali ni kuwabana wafanya biashara wakubwa?

Hawa wadogo waachwe wanalipia hela ya Meza na kutumia mpesa?
 
Hapana ni makosa kudhani direct tax ndio Kodi, mfano Kodi ya majengo watu kibao walikua hawalipi ila ilipowekwa kwenye Luku haikwepeki kulipwa na mapato kutoka hiyo segment yamepaa mara dufu sababu hayakwepeki.

So ukisubiri mpaka Kila mtu awe na ajira azalishe ndio alipe Kodi tutachelewa. Hata betting tu watu wakishinda wanakatwa VAT inaenda serikalini sasa utasema hawalipi Kodi kisa ana bet?
Unapolipa Kodi betting umelipa wewe imelipa kampuni ya Kubeti?
 
Wing wetu na hela vinahusiana vip mana hamna anae kula Serikalin maskin wote wapo bize na bado wananyonywa
Unakuwa na working force kubwa halafu chini ya Asilimia 10 wanalipa kodi ni majanga,

Lipa kodi Kwanza then fuatilia kodi yako inafanyiwa nini, kosoa serikali, strive for mabadiliko.

Ila unakaa hulipi kodi, unaingiza mpunga wa Kutosha, unasubiria Mzungu ulaya akuwekee paracetamol Hospital usitegemee maendeleo.
 
jitahidini muwe na uwezo mkubwa wa kufikiri nchi hii inakusanya pesa nyingi sana kwa mwezi
 
Tembelea hapo Mkuu Kuna source

Tanzania walipa Kodi wanaotambulika Tra ni milioni 2.2 tu, hata ukitoa watoto na wazee Kuna watu zaidi ya milioni 20 Wanapaswa kulipa kodi,

Mfano Kenya wanaolipa kodi ni milioni 5.5 na Sisi tupo wengi kushinda wao.
Ila hoja ya mtoa mada ina mashiko, kweli inawezekana walipakodi tz 2.2m , wanaotambulika na TRA, ila KWa fact wanaolipa kodi KWa njia MOJA au nyingine ni wengi

Ndo maana Kuna makusanyo kwe halmashauri, KILA mkoa izo pesa si bado zinakusanywa KWa wananchi, na si zinapekwa kwenye mfuko mkuu wa serikali
Hapo bado vyanzo vingine wakiwepo hata wafanyakazi ,sijui Kama pesa za kodi zimo ndani TRA, WEKA TOZO ,WEKA PESA AMBAZO TUNASAIDIWA WADAU WETU WA MAENDELEO, WEKA MIKOPO

Mtoa mada ana haki ya kujiuliza, alafu mapato binfsi nasikiaga TRA imekusanya kiasi flan, haya mengine hutangazwa na nani? Au yote huwa yamejuishwa ndani ya yale yaTRA?
NIkupongeze mtoa mada KWa uzi fikilishi
 
😂😂 mr. Takwimu we ni km mr. Kuku tu au wa vanila village. Indirect tax payers wapo kibao takribani kila mtanzania ni mlipaji wa kodi.
Bila Takwimu hakuna kitu utafanya ,utaishia kuwa kama Jiwe unashika kila kitu afu humalizi.
 
Ila hoja ya mtoa mada ina mashiko, kweli inawezekana walipakodi tz 2.2m , wanaotambulika na TRA, ila KWa fact wanaolipa kodi KWa njia MOJA au nyingine ni wengi

Ndo maana Kuna makusanyo kwe halmashauri, KILA mkoa izo pesa si bado zinakusanywa KWa wananchi, na si zinapekwa kwenye mfuko mkuu wa serikali
Hapo bado vyanzo vingine wakiwepo hata wafanyakazi ,sijui Kama pesa za kodi zimo ndani TRA, WEKA TOZO ,WEKA PESA AMBAZO TUNASAIDIWA WADAU WETU WA MAENDELEO, WEKA MIKOPO

Mtoa mada ana haki ya kujiuliza, alafu mapato binfsi nasikiaga TRA imekusanya kiasi flan, haya mengine hutangazwa na nani? Au yote huwa yamejuishwa ndani ya yale yaTRA?
NIkupongeze mtoa mada KWa uzi fikilishi
Hoja ina mashiko sikatai, ila kinachokusanywa hakikidhi mahitaji, ni kinatumika chote na hakitoshi. Sababu matumizi ni mengi kuliko tunachochangia mwisho wa siku tunakuwa selfish, cha kwetu tunakila na most of time kwenye matumizi yasiyo na tija huku tukisubiria tujengewe Vyoo.
 
Hizo link wametoa wenye tin number siyo idadi ya walipa kodi. Kulipa kodi ni wajibu wa kila raia ndo maana tunasisitizwa kudai risit halali ya malipo tuliyofanya ili kodi zetu zifike kiuhalisia.
Ulipo happy hata ukienda dukani hudai risiti,ukiuza hutoa risiti sasa kwa nini Serikali isiweke tozo?
 
Bila Takwimu hakuna kitu utafanya ,utaishia kuwa kama Jiwe unashika kila kitu afu humalizi.
Sawa mr. Takwimu japo hata jiwe tulikuw tukiona akitoa yakwimu za samaki majini, mara barabara kilomita kadhaa. Lkn wte ni blah blah tu
 
Back
Top Bottom