Kuna anguko kubwa sana la kujua kuandika sentensi na herufi sahihi za maneno miongoni mwetu Watanzania

Issue ni kwamba wanaandika kama wanavyo tamka.
Kwanini utamke Ela. Badala ya Hela na kwanini utamke Mpila badala ya mpira ,Kwanini useme Alusi au arusi badala ya Harusi...

Huu hapa ukweli Mchungu kusikia...
Lugha ya kiswahili ina maneno mengi sana yanayohitaji kujifunza Zaidi kama unaongea kiarabu..

Kwa zamani watoto wengi walipelekwa madrassa kujifunza lugha tu hata kama sio waislam ilichangia wazee wetu kujua lugha sanifu na matamshi kuntu..
ila siku hizi ni vigumu kumkuta Mkristo akijaribu kuumba herufi kwa kiarabu au kukaribiana na kiarabu, wanaona sjui wakifanya hivyo watabadilika na kuwa waislam na hiyo ndo tatizo lilipoanzia ....kwa baadhi ya herufi...
 
Herufi H na Herufi R inapotea sana ila me nahisi sababu naijua
H, E na L pia
Mchere = Mchele
Rucy = Lucy
Sukali= Sukari
Mahalage = Maharage
Kulwa = Kurwa
Mpila = Mpira
Amsini = Hamsini

Mkuu, na mimi natamani kujua sababu, unaweza kuiweka hapa kwa manufaa ya wengi?
 
Yote yamesababishwa na Muingerza kuondoa kiswahili katika herufi za Kiaarabu kama ilivyokuwa awali, Ingekuwa unyama sana na makosa yasingekuwepo Kiswahili tungekuwa tunaType na kuandika kwa maandishi ya Kiaarabu.

Cc : Maghayo MK254
 
sawa. nawew rekebisha kwanza haya uliyoandika hapa-

utapia kichwa
utapia ujinga
sms
chats
etc.
 
Tetea hoja yako.
Mimi nimetetea kwa kutumia hiyo nafsi ya kwanza umoja na uwingi.

Tetea na wewe tuone huenda ukawa sahihi.
Mkuu Mimi hata nikisema ntarudia maneno yale yale!
Na mwisho ntakuwa kama naboa tu..
Maneno kama...

Twangojea =Tunangojea✓
Twasoma =tunasoma✓
Sote= sisi wote✓
Twapita= Tunapita✓
Twonane =Tuonane✓
Twaenda= Tunaenda..✓
Twende =tuende✓

Hili swala dogo tu la lahaja mkuu..

Sote ni lahja ya kitumbatu
..........
Twangoja na zingine zote zenye neno Twa au 'tw'

Neno twa au tw ni neno linalomaanisha wingi kama ilivyo tu sema hapa ni wenye heshima na ndo maana hata watu wa pwani akiwa hata kama mmoja akipita sehemu atakuambia..
Twapita badala ya napita...

Maana ya pili ni Wingi kama ilivyo tu
Kama...
'Naenda zangu'
Kuwa
'Twaenda zetu'
Au 'twenda zetu'

Zote hizi zinaongewa na zipo kwenye lahaja ya Pate ,
Lahaja ya pemba ,Lahaja ya kimtang'ata,lahaja ya unguja na lahaja zote za pwani..

Na ndo maana Mtu wa bara akienda pwani zanzibar au Tanga watamshangaa anavyotamka na kuumba herufi...

Kadhalika mtu wa Pwani au zanzibar vivyo hivyo...

Kuna maneno ambayo hutakuja kuyasikia Bara ila pwani na zanzibar ni kawaida kutuka...

Kama kusikia mtu anasema 'Yule yuapita hapa/pale'
Wakati bara hutumia Yule anapita hapa/pale..

Na hiyo ipo kwenye ngeli ya Yu-a-wa...
 
Yaaniii
 
Umasikini na Ujinga, ni mtaji wa ccm!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kila sekta nchini Tz inarudi nyuma badala ya kwenda mbele kimaendeleo. Hatuna umakini katika lolote.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…