Kuna Dada anauza uji soko la Stereo, leo kapigwa marufuku kwa kuwa ni msimu wa Ramadhani

Status
Not open for further replies.
Hakuna hadithi inayokataza kula mbele ya aliefunga mwezi mtukufu wa Ramadhan
Tuvumiliane jamani
Kumpa chakula mtu aliefunga sio vizuri kama unajua ila tunafunga kwa sababu ni lazima kufunga na wala Siwezi kuwa na tamaa kuona uji unauzwa nikanywa

Tuheshimu na tusitukane kwani ni mwezi wa Toba huu
 
Kama unakwazika Rudi kwenu
 
Dada wanamlazimisha asilete bidhaa ( uji) kujipatia ridhiki Kwa kuwahzia watu wengine ambao hawafungi,wakristo na wapagani.Waislamu wamemkataza kufanya biashara
Ukiona hivyo % kubwa hapo ni waislam
 
Hicho mnachokizungumzia hakipo kwenye uislamu. Mlichokifanya hapo ni kuchukua kauli personal na kuusemea uislam. Uislam haupo hivyo. Msikurupuke.
 
Mungu yupi anataka watu wateseke bana..... Hizi dini sizielewi kabisa....mimi nitaendelea kuabudu nature
 
Funga ni jambo la kiimani, je, imani zenu ni haba kiasi kwamba mkiona chakula mnazitupa mbali hizo imani?[emoji848][emoji2827]
Hapo ni swala la tamaduni, na hizo ni tamaduni zetu watu wa pwani.
Na ndio sehemu zenye waislam wengi
Hizo tamaduni haziwezi kuoneka Bara coz sio maeneo yenye waislam wengi.
Ikiwa mgeni wa Pwani lazina Uta shangaa
Mmetaka kuja Pwani basi fuateni tamaduni zetu hamutaki rudini kwenu
 
...Na kama huyo Dada naye kakubali basi ni Mjinga! Nchi Haina Dini. Labda naye ni Muislamu....!
 
Mkuu hizo ni tamaduni za watu wa pwani unapofika mwezi wa Ramadhan.
Sasa kama wewe mgeni fuata tamaduni za wenyeji wako,huwezi rudi kwenu
Hiyo ni jamii iliyotangamana. Kama kila mtu ataleta tamaduni zake itakuwaje. Tuseme kwenye familia zao wote wanafunga? Hakuna wagonjwa au watoto wanaopikiwa chakula. Tamaduni gani hizo zisizotumia akili?
 
Mwezi ukipita madhambi kama yote. Hii dini mi naipenda sana..nipo mbioni kuhamia huko
Mwezi ukipita madhambi kama yote [emoji1787]
Kuna Rafiki yangu mmoja anaitwa ISSA enzi hizo niko nyumba zetu zileee za kushea, alikuwa anatukaribisha misosi ya nguvu mno kipindi kama hiki.

Saa 12 jioni, ftari na uji, 2 usiku daku, 4 usiku menyu kamili, na 10 au 11 alfajiri kukazia menyu.

Sasa najiuliza hivi huku ni kufunga kweli au kubadili tu ratiba ya msosi [emoji848]

Tena si msosi wa kawaida kama siku ambazo Jamaa hafungi bali ni msosi wa nguvu haswaa [emoji16]
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…