Umezungumza kitu kama “hao wazee wanaowashauri vijana waoe maisha yao nao ni mabaya kwa maana kuoa kungekuwa kunarahisisha maisha wasingekuwa maskini bado kama walivyo” ukiunganisha na ulivyomaliza pale chini ndipo hoja yangu iliposimama.
Kwamba wewe binafsi upo ktk hatua gani kwanza kiumri,kimafanikio huku ukimuiga baba yako tajiri mwenye tofauti na hao wazee uliowataja hapo juu?
TUKIWAULIZA MNAOA/KUOLEWA KWA MADHUMUNI GANI MATAJIBU?
hawa vijana wanaokimbilia ndoa hawanaga sababu ya maana, zaidi ya kufuata mkumbo/ngono ya bure na upuuzi ufananao na huo, na kwa mwanamke anaolewa ili ajenge status ktk jamii na kujikomboa kiuchumi, hakuna sababu za msingi.
Ewe kijana&binti, kataa ndoa za mchongo, hasa kwa mwanaume, usioe mpaka uwe stable kiuchumi, oa ukiwa na hakika ya kumlisha binti wa watu kwa nyakati zote, oa ukiwa na hakika ya kusaidia ndugu zake ambao itakulazimu ufanye hivyo utake ama usitake,
Oa ukiwa na hakika ya kumhudumia mkeo akiwa ktk shida za kiafya, bila kusahau wazazi wake wakipata shida za kiafya&kiuchumi hilo ni jukumu lako ewe muoaji.
Oa ukiwa na hakika ya kuwatunza watoto wako, uwe na hakika ya kuwapa mahitaji yote na haki zao zote za msingi ikiwepo elimu bora na urithi wa kudumu, na utambue hili urithi kwa wanao ni Mali na pesa wala sio elimu, elimu ni wajibu wa mzazi kumpatia mtoto, elimu sio mali na sio urithi, ndiomaana huwezi kumrithisha mwanao hizo degree zako na sifuri zako ulizopata form 4, hivyo basi andaa mali na pesa za kutosha kwaajili ya warithi wako.
Ewe kijana kataa kudanganywa, na hao motivation speakers wenye mindset za kizaman et wengine wanadai ndoa ni baraka sijui ndoa ni nguzo ya dini, wengine eti ndoa ni Sunna, pumbavu hizi habari za sunna ni mawazo ya wazee wa zaman uko ambao waliiishi dunia ikiwa uncivilised, jitu linaoa wake 10 kuwahudumia inategemea bahati na Nguvu kazi ya shamba/ufugaji na vyakula vya bure huko maporini, tofauti na sasa, kila kitu kinahitaji pesa.
Ndoa sio sunna wala sio baraka ni maandalizi ya kiuchumi, kisaikolojia na kila kitu, ndoa itakuwa Sunna kwa watu wenye akili timamu.
Sasa wewe mwanaume kama unaweza timiza yote hayo basi oa, lkn kama unaishi maisha ya kubeti na kutegemea ndoa ikukomboe, aisee utaishia kurithisha laana, mikosi na ufukara ktk Ukoo wako na familia yao.
Tafuta sana pesa, na hayo mengine utazidishiwa.