Kuna faida gani kumpaka mtoto aliyezaliwa damu ya uzazi?

Kuna faida gani kumpaka mtoto aliyezaliwa damu ya uzazi?

Pengine inawezekana ni kweli hao Watutsi hupaka damu ya uzazi kwa watoto wao.

Kama ni kweli, Basi huo ni utamaduni wao na uhuru wao wa kimila kufanya hivyo.

Lakini hakuna ukweli wowote kwamba hiyo damu ya uzazi itawakinga hao watoto na husda za walimwengu.

Hizo ni imani zao uchwara tu zisizo na ukweli wowote.

Hata uchagani miaka ya zamani walikuwa wanaamini kuzaa watoto mapacha ni nuksi kwenye ukoo.

Hivyo ilikuwa ukizaa watoto mapacha, wanamuua mtoto(pacha) mmoja wakiamini eti wanafuta laana kwenye ukoo.

Kumbe ni mila uchwara tu za kijinga.
Umaskini wa kifikra
Kuna ile uchagani watoto wakiota meno ya juu kwanz ni laana na nuksi😂
Huu uzi hauwafahi..!
 
Kuna dada ni rafiki wa mama yangu huwa analalamika mumewe anataka kumtoa kafara ili apate utajiri.
Juzi kati alipata ajali mbaya sana akapelekwa hospital madaktari wakadhibitisha amefariki hivyo apelekwe mochwari.

Walivyomfikisha mochwari ile wanataka kumchoma sindano marehemu akazinduka.
Sasa wakati anamsimulia mama yangu changamoto za kishirikina anazokutana nazo kwa mume wake akasema "Huyu mwanaume hawezi kunishinda, mimi ndiye mtutsi original labda kama nisingepakwa damu ya uzazi"

Mama yangu akamuuliza kuhusu damu ya uzazi ndio akaambiwa ila kwa ufupi.
Alikuwa hajafa huyo.
 
Huu uzi hauwafahi..!
Ukishaweka uzi wako JF umeuweka public forum.

Kila mtu anaweza kuuona, kutoa maoni na kuchangia chochote kile kwa wakati wowote ule.

Huwezi kutaka privacy kwenye public forum.

Ungetaka privacy ungetafuta members wako wanaokufaa muende PM mkajadiliane huko.

Ukishaweka uzi wako public, Huo ni wa kila mtu.
 
Wanasema mtoto aliyepakwa damu ya uzazi hata lasna na mikosi ya ukoo inampitia mbali, ataishi duniani na nyota yake ya asili.
Wachawi watu wenye nia ovu juu yake wanagonga mwamba.
Faida hii mojawapo umeitaja.
 
Kuna baadhi ya mama huwapaka watoto wao damu inayotoka ukeni punde baada ya kutoka kujifungua.

Kwa nilivyosikia hii kitu ipo sana kwenye jamii ya Watutsi.
Wanasema punde mama anavyokabidhiwa mtoto wake basi hufanya kitu hiki huku akinenea maneno.

Inasaidia mtoto asipate husda yoyote inayosababishwa na walimwengu.
Watu waliofanyiwa kitu hiki huwa hawarogeki, wengine wanakua na nyota kali sana.
Chochote kibaya kinachowapata labda akisababishe mwenyewe ila sio kwa kusababishiwa na watu.

Hii ishu nimeisikia mara mbili, na jamii hizo hufanya jambo hili kwa siri ndio maana sio kila mtu anajua kuhusu hii mila au desturi.

Nikaona nije kuuliza humu sababu kuna wajuzi wa mambo.
Naomba kujua ukweli wa jambo hili.
Mshana Jr LIKUD GENTAMYCINE mdukuzi ngara23 Kapeace
Imani yako ndio itafanya kile unochoamini kitakuwa
 
Hiyo uliyotaja ndiyo faida kuu ya msingi-Kutoa ulinzi wa mtoto maisha yake yote na nyuma ya hili huwa kuna malaika mlinzi.

Faida nyingine ni kwamba ile hali ngumu ya uchungu aliyoipata mama huwa imebeba siri inayoonyesha utajiri wa mtoto.Kila mtoto huwa amebeba siri ya aina yake ambayo hata mama yake haijui.Wana mpaka damu ya placenta mtoto ili kumrahisishia katika njia zake huyo mtoto akikua siku moja aje kufunuliwa siri yake.Mtoto wa aina hiyo anapoijua siri yake,huwa anazidi kufurahi kuona hadithi yake ya mafanikio inadumu kuwapendeza wasomaji wengi.

Hiyo ndiyo faida nyingine ninayoijua.

Na wengine wataendelea kuongezea faida wanazozijua.
 
Na pia kuhusu kitovu Cha mtoto unakichukua unakiweka katika kopo.

Yote hufanya Sana Wahaya , waganda na watusi Kwa lengo hasa la kuzuia watoto wao wasirogwe .

Ila Mara nyingi michipuko ndo hufanya hizi mambo au wale walioa wanawake wengi.

Nkmeona sehemu kama 03 Nyumbani Bukoba
Mkuu,

Hivi kwanini wanawake wa Kihaya wakishika mimba lazima waende kwao kunywa dawa au la hutumiwa dawa hito toka kijijini?.

Ni dawa za uzazi tu au kuna mengine huchanganywa humo?
 
Hiyo uliyotaja ndiyo faida kuu ya msingi-Kutoa ulinzi wa mtoto maisha yake yote na nyuma ya hili huwa kuna malaika mlinzi.

Faida nyingine ni kwamba ile hali ngumu ya uchungu aliyoipata mama huwa imebeba siri inayoonyesha utajiri wa mtoto.Kila mtoto huwa amebeba siri ya aina yake ambayo hata mama yake haijui.Wana mpaka damu ya placenta mtoto ili kumrahisishia katika njia zake huyo mtoto akikua siku moja aje kufunuliwa siri yake.Mtoto wa aina hiyo anapoijua siri yake,huwa anazidi kufurahi kuona hadithi yake ya mafanikio inadumu kuwapendeza wasomaji wengi.

Hiyo ndiyo faida nyingine ninayoijua.

Na wengine wataendelea kuongezea faida wanazozijua.
Nitarudi kesho kusoma hii comment tena, leo nimetoka kapa.
 
Back
Top Bottom