Kuna faida gani za nchi kuruhusu mataifa kuingia bila VISA?

Ruto kachanganyikiwa.

Analeta Ujamaa kwenye nchi yenye Katiba ya Kibepari.

Nchi ina madeni, hata kulipa wafanyakazi ni shida, kwa hiyo yote haya kuondoa visa ni kutapatapa tu kutafuta njia ya kujinasua na balaa.
 
Ukilinganisha na majirani zetu, na nchi nyingine za Afrika, sisi wabingo sio watu wa kutoka na kusaka fursa nje ya mipaka yetu.

Ndio maana hoja kama hizi tunazizungumzia kwenye misingi ya uoga na kutoelewa.

Tukiwa watu wa kutoka tutaona alichifanya Kenya na faida sana.
 
Sasa unapoteza nini kufungua mipaka kwa maskini mwenzako?

Na ni nchi ngapi Africa zimeruhusu hiyo free movement au hata hapa Africa Mashariki? Wewe kama unataka nenda tu huko Kenya utatuletea ulichopata siku ukirudi! Kamwambie hivyo na Kaguta Museveni au Kiir wa Sudani Kusini au Tshisekedi wa DRC au huyu wa juzi wa Somalia! Unadhani wao hawapendi hiyo free movement wakati wapo kwenye jumuiya? Mbona unarukia huku Tz? Kawaulize hao niliokutajia kama unadhani free movement ni kama kutafuna njugu!
 
👏
 

Uganda naye kafungua mipaka? Vipi DRC, Sudan Kusini maana hizi zipo hapa hapa East Africa! Nao ni waoga kama wabongo? Na kwa bara zima la Africa ni nchi ngapi zimefanya hivyo! Nenda Africa Kusini bila visa au Nigeria au Misri au Morocco au Libya! Tusione Kenya ndiyo imeonyesha mfano Africa! Kwa nini bara zima la Africa lisifute visa? Lazima zipo sababu! Anayetaka kwenda Kenya ruksa!
 
Kwani una dhani gaidi anakosa dola 30 za visa?
 
Dola 50 iliyopaswa kulipia visa inaweza kutumika kwenye hoteli atakayofikia mgeni, aidha kwa usafiri au kuongeza siku za kukaa hotelini. Mkakati huu unaweza kutumika kupata watalii wengi watakao chagua kutembelea Kenya, Lakini Kenya inajiweka kwenye nafasi kwa passport ya Kenya kukubaliwa bila visa kwa mtindo ule ule .... Kitu wanaita: "Reciprocity"
 
Nilivyomuelewa Ruto, amebadilisha utaratibu tu na sasa 'visa' uwanjani yaani, 'airport' baada ya kuwasili..
 
Ya kwamba magaidi wao ndo watakosa hizo dora 30 za viza?

Au ya kwamba ugaidi una zuiliwa kwa visa? Alafu mbona wasomali wamejaa kila sehemu ya nchi hii na mpaka wengine wana mamlaka makubwa ya kiuongozi ndani ya nchi yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…