Kuna Genge ndani ya CCM linajiandaa kumuondoa Samia 2025 kwa Mlango wa Nyuma

Rais SSH amekuwa rais wa viwango tangu aingie madarakani 2021, Bahati mbaya ameangukia kwenye kundi lenye uroho wa Madaraka na Wapiga dili wa tangu kale.

Bahati mbaya SSH amekuwa akiamini ndio kundi lenye kumshauri vizuri,kumbe ni kundi lenye Maslahi binafsi haliamini Kama Samia anaweza akatekeleza matakwa yake yote.

Bahati mbaya SSH amekuwa akiteua ama Mawaziri ama Makatibu Wakuu ama Wenyeviti na Wakurugenzi wa Bodi mbalimbali akiamini anafanya yeye kumbe Mtandao umemchomekea Majina.

Bahati mbaya kundi linaloongozwa na JK limekuwa likisherekea kila siku kuwa wameweza kuishika Ikulu na Chama kwa kila pembe ndio maana kila Weeknd kundi hili linakutana Msoga kukata Keki na kufungua Shampeni.

Bahati mbaya haya yanafanyika Wananchi wanajua kuwa kundi la JK lilimchukia Magufuli kwa msimamo wake wa kusimamia Maslahi ya Wanyonge na Nchi kwa ujumla, nasema Bahati mbaya kwasababu Visasi vinavyofanywa Wananchi wanajua.

Bahati mbaya SSH ameshauriwa kumweka Makamu wa CCM Tanzania Bara Ndugu Kinana ambaye kwasasa Nguvu zake za ushawishi zikiwa zimepungua sana baada ya kumtukana Magufuli wakati ule na kuhusishwa hapo baadae na kifo chake, Baadhi ya Makada wa CCM hawakufurahishwa na Kinana kupewa nafasi kwasababu ya kasoro hizo.

Kinana anahusishwa kwenye kashfa nyingi za wizi, Magendo na Mitandao ya Rushwa ikiwemo Mipango ya upigaji ya Marafiki wa JK, Bahati mbaya Wananchi wanajua hili.

Bahati mbaya kwa SSH hajajua kuwa Hana Nguvu za ushawishi Ndani ya Chama na kwa Wananchi hasa Bara, na kwa Hali hiyo kundi hili limekuwa likijiandaa kumshauri asigombee Mwaka 2025 na hivyo kumshauri vibaya ili aendelee kukosea, mfano safari za Nje, Mfumko wa Bei Kama umeme na bidhaa za chakula na mikopo mingi kinyume na JPM alivyowaaminisha Wananchi.

Bahati mbaya SSH amekuwa akisifiwa na kundi hili kuwa 'Anaupiga mwingi' ili avimbe kichwa lakini uhalisia huku mitaani Hali ni mbaya sana na Kama Kura zingepigwa leo Samia hawezi kutoboa.

Bahati mbaya Wananchi wanajua kuwa SSH ana'limoti'wa na JK ndio maana kila teuzi karatasi inatoka Msoga, na hili hakuna atakae amini kuwa haya ni maamuzi huru ya Rais kwasababu wataeule wengi ni Wana Mtandao ama Wana nasaba na JK.

Bahati mbaya serikali ya SSH kwasasa imeanza kunukia " udini" hii imekwenda mpaka kwenye Chama, Samia Ni dini Moja na Makamu wake Kinana hii inanung'unikiwa sana kuwa miwani ya SSH haikuliona hilo vizuri.

Bahati mbaya SSH amekuwa akiteua watu toka Zanzibar kwenye mambo yasiyo kuwa ya Muungano, Kama Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Baadhi ya Taasis za kiserikali zisizohusu Muungano. Pamoja na hilo Baadhi ya Mikopo na Misaada ya Nje Zanzibar imekuwa wanufaika wakubwa huku gharama za ulipaji zikielemea bara, hii amekuwa akipigiwa makofi tu Lakini Ni kaa la Moto linaloshusha ushawishi wake upande wa Bara, Hivyo kundi hili analolibeba litatumia sababu hii kumshawishi asigombee 2025.

Bahati mbaya SSH hajui kuwa kundi hili analolibeba taswira yake inanuka ufisadi na kwa namna wanavyomshauri atadumbukia kwenye mtego wa kuachia ngazi ya kugombea urais 2025 nao wataweka mtu wao ili kuendeleza upigaji wa tangu enzi zile.

Bahati mbaya SSH hana washauri wazuri Ndani ya serikali na Chama ambao watamshauri kuchunga kauli zake zinazochochea kugawa watu ama kuwafanya wafanyabishara kupandisha bei kiholela, kundi lake linafurahi anapokosea ili iwe rahisi azma yao ya 2025.

Bahati mbaya mpaka 2025 sifa za SSH zitakuwa zimeshuka sana kwa kiwango cha kutisha hasa Bara na hapo kazi ya kundi hili itakuwa rahisi kumwambia arudi Kizimukazi kulea Wajukuu na kutunza Ndoa na wake wenzie.

Rai ya uzi huu ni kumushauri SSH kuwa Makini na kundi la JK na kuangalia upya uteuzi wa Kinana maana hauna Taswira nzuri KIDINI na kiutendaji na hasa kumbukumbu ya Kinana na kundi lake kutukana Wasukuma na JPM kuwa ni washamba, Asiposikia na kulijua hili zigo litamrudia 2025, ama Ndani ya Chama ama kwa Wananchi.

Rai kwa SSH awe makini na Mawaziri mizigo ambao wanafanya serikali yake kukosa mvuto na kuvunja Imani ya Wananchi, asiposikia 2025 zigo litamrudia.

Bahati mbaya kufa kwa Kenge mpaka damu itoke masikioni.

Bahati mbaya Wapambe watamwambia huu uzi ni upepo tu utapita.
Mwamba usihangaike na viongozi wa mpito, SSH ni kiongozi wa mpito apende asipende ndiomana sasa hivi anafanya potelea mbali aendelee kula kwa urefu wa kamba yake kwa sasa hadi 2025
 
Mama Samia Mungu amfungue macho na roho.

Yaani kosa lake la kwanza ni pale alipojitutumua kuanza kuonesha yeye ni rais baada ya kifo cha Dkt Magufuli. Hakuwa na strategists wa kumshauri cha kufanya. Hakupaswa kabisa kipindi hicho kutoa hotuba ndefu, alipaswa atulie kama mwezi mzima na kusema nchi iko salama kila kitu kipo sawa.

Baada ya hapo angeona wanao mdharau na angewajua wabaya wake kutokana na ukimya. Baada ya hapo angekunjua makucha kwa kuteua si sura toafuti kabisa ambazo hazijazooeleka. Hata watu wa Ikulu alipaswa kudeal nao makini. Ila sasa kafumua fumua utadhani mama hakuwa sehemu ya Dkt Magufuli.

Hivyo kwa sasa mpaka viongozi wanamdhihaki, tena hawana imani naye ila wanalinda vibarua vyao
Hana uwezo
 
Mama hakuwa sehemu ya Magufuli, yeye alikuwa makamu wa rais wala hakuwa muumini wa utawala wa kidhalimu wa Magufuli. Magufuli mwenyewe alikuwa anadhihakiwa na viongozi mpaka akawa anashinda kudukua mawasiliano ya watu kinyume na sheria. Acheni kumtishia huyo mama maana anajua fika Magufuli hakuwa na ushawishi wowote zaidi ya kuburi cha madaraka.

Viongozi gani? Wa kunadi sera za kulamba asali mbele ya mamilioni wasio na uhakika wa kesho yao? Maana ya maneno uongozi wa watu ilipotea katika akili za baadhi ya Watanzania.
 
Genge lenyewe hawa hawa waswaga ng'ombe wa Gamboshi!?
Au genge gani!?

Wape taarifa, wasubirie 2029-2030! Labda wanywe mabele ga nguruwe na matobolwa!

Walishachelewa. Huyo mama hata kutembea anamotembelea ni kuhakikishiwa support during her reign!
 
Ni
Kiongozi wa hilo genge tushamla kichwa sasa hivi anavuna korosho hapo kongwa. Wala hamtutishi.

Ni kosa kubwa kuingia vitani ilkhal humjui adui ni nani, uwezo wake, nguvu alizonazo asili yake wapi nk, waeza jikuta unapambana na KIVULI chako mwenyewe.
 
Bwashee hii nchi ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko kuweza kumpiku Rais aliyeko madarakani kwamba ashindwe kugombea na kushinda
Ukumbuke sasa hivi wale mabingwa wa figisu za CCM ndio Watu wa karibu wa mama.

Ukitaka kuamini subiri kinana apange mkeka wa ndan ya CCM. Nguvu ya mamba iko kwenye maji, ukishatolewa kwenye mfumo unakuwa kama mlevi unayepayuka tu, na ukizidi kupayuka utashughulikiwa kidiplomasia eg Polepole au kibabe
 
Viongozi gani? Wa kunadi sera za kulamba asali mbele ya mamilioni wasio na uhakika wa kesho yao? Maana ya maneno uongozi wa watu ilipotea katika akili za baadhi ya Watanzania.

Magufuli alishashusha heshima ya box la kura, hakuna kiongozi wa ccm tena atategemea kushinda kwa ushawishi, wote watatumia vyombo vya dola na tume isiyo huru ya uchaguzi kukaa madarakani. Hao mamilioni hawana madhara yoyote maana hakuna kiongozi ww ccm anategemea kura zao kukaa madarakani.
 
Kama wananchi walikuwa na imani na Magufuli asingenajisi uchaguzi ili kukaa madarakani kwa shuruti. Hivi vitisho sijui wananchi walikuwa na imani na Magufuli kawaambie wajinga wasiojua lolote.
Kwa raisi msingetoboa hata zikirudiwa. Magufuli alikuwa anaaminiwa sana lbda vibunge uchwara vingne ndo vilipta kwa rafu za uchaguzi
 
Magufuli angeweza kushinda bila hata kuiba kura, ila tofauti ya kura ndio alikuwa hataki kusikia. Hakupora uchaguzi kwa bahati mbaya maana ukweli alikuwa anaujua
 
Kama watanzania hatutaungana 2025 kuing'oa CCM hii ya WEZI titaishi kwa taabu sana,HAKUNA cha maana tena tunachoweza kutarajia kwa CCM HAKUNA hakuna HAKUNA.
 
Rais SSH amekuwa rais wa viwango tangu aingie madarakani 2021, Bahati mbaya ameangukia kwenye kundi lenye uroho wa Madaraka na Wapiga dili wa tangu kale.

Bahati mbaya SSH amekuwa akiamini ndio kundi lenye kumshauri vizuri,kumbe ni kundi lenye Maslahi binafsi haliamini Kama Samia anaweza akatekeleza matakwa yake yote.

Bahati mbaya SSH amekuwa akiteua ama Mawaziri ama Makatibu Wakuu ama Wenyeviti na Wakurugenzi wa Bodi mbalimbali akiamini anafanya yeye kumbe Mtandao umemchomekea Majina.

Bahati mbaya kundi linaloongozwa na JK limekuwa likisherekea kila siku kuwa wameweza kuishika Ikulu na Chama kwa kila pembe ndio maana kila Weeknd kundi hili linakutana Msoga kukata Keki na kufungua Shampeni.

Bahati mbaya haya yanafanyika Wananchi wanajua kuwa kundi la JK lilimchukia Magufuli kwa msimamo wake wa kusimamia Maslahi ya Wanyonge na Nchi kwa ujumla, nasema Bahati mbaya kwasababu Visasi vinavyofanywa Wananchi wanajua.

Bahati mbaya SSH ameshauriwa kumweka Makamu wa CCM Tanzania Bara Ndugu Kinana ambaye kwasasa Nguvu zake za ushawishi zikiwa zimepungua sana baada ya kumtukana Magufuli wakati ule na kuhusishwa hapo baadae na kifo chake, Baadhi ya Makada wa CCM hawakufurahishwa na Kinana kupewa nafasi kwasababu ya kasoro hizo.

Kinana anahusishwa kwenye kashfa nyingi za wizi, Magendo na Mitandao ya Rushwa ikiwemo Mipango ya upigaji ya Marafiki wa JK, Bahati mbaya Wananchi wanajua hili.

Bahati mbaya kwa SSH hajajua kuwa Hana Nguvu za ushawishi Ndani ya Chama na kwa Wananchi hasa Bara, na kwa Hali hiyo kundi hili limekuwa likijiandaa kumshauri asigombee Mwaka 2025 na hivyo kumshauri vibaya ili aendelee kukosea, mfano safari za Nje, Mfumko wa Bei Kama umeme na bidhaa za chakula na mikopo mingi kinyume na JPM alivyowaaminisha Wananchi.

Bahati mbaya SSH amekuwa akisifiwa na kundi hili kuwa 'Anaupiga mwingi' ili avimbe kichwa lakini uhalisia huku mitaani Hali ni mbaya sana na Kama Kura zingepigwa leo Samia hawezi kutoboa.

Bahati mbaya Wananchi wanajua kuwa SSH ana'limoti'wa na JK ndio maana kila teuzi karatasi inatoka Msoga, na hili hakuna atakae amini kuwa haya ni maamuzi huru ya Rais kwasababu wataeule wengi ni Wana Mtandao ama Wana nasaba na JK.

Bahati mbaya serikali ya SSH kwasasa imeanza kunukia " udini" hii imekwenda mpaka kwenye Chama, Samia Ni dini Moja na Makamu wake Kinana hii inanung'unikiwa sana kuwa miwani ya SSH haikuliona hilo vizuri.

Bahati mbaya SSH amekuwa akiteua watu toka Zanzibar kwenye mambo yasiyo kuwa ya Muungano, Kama Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Baadhi ya Taasis za kiserikali zisizohusu Muungano. Pamoja na hilo Baadhi ya Mikopo na Misaada ya Nje Zanzibar imekuwa wanufaika wakubwa huku gharama za ulipaji zikielemea bara, hii amekuwa akipigiwa makofi tu Lakini Ni kaa la Moto linaloshusha ushawishi wake upande wa Bara, Hivyo kundi hili analolibeba litatumia sababu hii kumshawishi asigombee 2025.

Bahati mbaya SSH hajui kuwa kundi hili analolibeba taswira yake inanuka ufisadi na kwa namna wanavyomshauri atadumbukia kwenye mtego wa kuachia ngazi ya kugombea urais 2025 nao wataweka mtu wao ili kuendeleza upigaji wa tangu enzi zile.

Bahati mbaya SSH hana washauri wazuri Ndani ya serikali na Chama ambao watamshauri kuchunga kauli zake zinazochochea kugawa watu ama kuwafanya wafanyabishara kupandisha bei kiholela, kundi lake linafurahi anapokosea ili iwe rahisi azma yao ya 2025.

Bahati mbaya mpaka 2025 sifa za SSH zitakuwa zimeshuka sana kwa kiwango cha kutisha hasa Bara na hapo kazi ya kundi hili itakuwa rahisi kumwambia arudi Kizimukazi kulea Wajukuu na kutunza Ndoa na wake wenzie.

Rai ya uzi huu ni kumushauri SSH kuwa Makini na kundi la JK na kuangalia upya uteuzi wa Kinana maana hauna Taswira nzuri KIDINI na kiutendaji na hasa kumbukumbu ya Kinana na kundi lake kutukana Wasukuma na JPM kuwa ni washamba, Asiposikia na kulijua hili zigo litamrudia 2025, ama Ndani ya Chama ama kwa Wananchi.

Rai kwa SSH awe makini na Mawaziri mizigo ambao wanafanya serikali yake kukosa mvuto na kuvunja Imani ya Wananchi, asiposikia 2025 zigo litamrudia.

Bahati mbaya kufa kwa Kenge mpaka damu itoke masikioni.

Bahati mbaya Wapambe watamwambia huu uzi ni upepo tu utapita.
Rubbish 🚮🚮
 
Back
Top Bottom