Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Ukristo haukuletwa na Yesu, ulianzishwa na kila Peter miaka mingi baada ya Yesu kupaishwa mbinguni. Unapingwa kwa sababu ni dini inayoabudu mtu badala ya Mungu ambae ni Elloi Elloi lamma sabaktany?
Acha kuropoka.
Ukristo ulianzishwa na Yesu Kristo siku ile ya Alhamisi Kuu, siku moja kabla ya kifo chake. Mara baada ya ufufuko wake, akawapa agizo mitume wake 11, agizo la kwenda Duniani kote kuwafanya wanadamu wote kuwa wafuasi wake. Lakini nguvu ya utekelezaji wa agizo lake ulianza siku 50 baada ya kuondoka Yesu Duniani, yaani siku ya Pentekoste.
Mat: 18: 17-19
17 Walipomwona, walimwabu du. Lakini baadhi yao waliona mashaka.
18 Yesu akawakaribia akawaambia, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Kwa hiyo nendeni mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu: mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Petro na mitume walianza kutengeneza Kanisa la Kristo mara baada ya agizo la Kristo. Nguvu kubwa ya kanisa hilo ilianzia siku ile ya 50 toka Yesu kuondoka Duniani, baada ya mitume na waumini wa mwanzo kupokea Roho Mtakatifu. Ndipo wanatoka na kufanya mahubiri kwa nguvu na uwazi mbele ya maelfu ya watu. Ndipo Petro ananena kwa sauti kubwa:
Matendo 2:
34 Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini alisema, ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: kaa upande wangu wa kulia, 35 mpaka nitaka powafanya maadui zako kiegemezo cha miguu yako.’
36 “Basi nataka niwahakikishie Waisraeli wote ya kuwa, Mungu amemfanya huyu Yesu ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa ndiye.
37 Watu waliposikia maneno haya yaliwachoma moyoni, wakawau liza Petro na wale mitume wengine, “Tufanye nini ndugu zetu?” 38 Petro aliwajibu, “Tubuni, muache dhambi na kila mmoja wenu abatizwe katika jina la Yesu Kristo, ili msamehewe dhambi zenu; nanyi mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu. 39 Kwa maana ahadi hii ilitolewa na Mungu kwa ajili yenu na watoto wenu, na wale wote walio nchi za mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu anamwita kwake.
NB. Wasiomjua na kumkiri Kristo wanefanywa viegemezo vya miguu ya waliompokea Kristo.