Kuna haja ya Tundu Lissu kuandaliwa kuiondoa CCM 2025 madarakani?

Kuna haja ya Tundu Lissu kuandaliwa kuiondoa CCM 2025 madarakani?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari wana Jf, kwa mara ya kwanza nimejikuta nasikitishwa sana na umasikini na ugumu wa maisha unaoendelea kuongezeka huku kukiwa hakuna suluhisho la kueleweka Kutoka CCM.

Nimewaza sana na kujikuta naona Tundu Lissu ndiye anaonekana mtu pekee kwa sasa mwenye ushawishi na uwezo wa kuongoza nchi, hasa kuiondoa CCM madarakani kupitia chama chochote hata kipya, aandaliwe na kuweza kuja kuiondoa CCM.

CCM imeongoza nchi kwa zaidi ya miaka 40 lakini imeshindwa hata kuwatua kina mama ndoo za maji mijini kote. Pia imeshindwa kwa kiwango kikubwa katika kupiga vita ufisadi, kuendeleza na kujenga viwanda, kuondoa shida ya ajira, kuboresha huduma za afya na nk.

2025 CCM inaweza ondoka, aandaliwe vizuri tu.
 
Habari wana Jf ,kwa mara ya kwanza nimejikuta nasikitishwa sana na umasikini na Ugumu wa maisha unaoendelea kuongezeka huku kukiwa hakuna suluhisho la kueleweka Kutoka CCM .

Nimewaza sana na kujikuta naona ni Bora Tundu lissu ambae anaonekana ndiye mtu pekee kwa sasa mwenye ushawishi na uwezo wa kuongoza Nchi hasa kuiondoa CCM madarakani kupitia Chama chochote hata kipya aandaliwe na kuweza kuja kuiondoa hii CCM.

CCM imeongoza Nchi kwa zaidi ya miaka 40 lakini imeshindwa hata kuwatua kinamama ndoa za Maji mijini kote na imeshindwa kwa kiwango kikubwa katika kupiga vita Ufisadi , kuendeleza na kujenga viwanda ,kuondoa shida ya Ajira ,kuboresha huduma za Afya na nk .

2025 CCM inaweza Ondoka aandaliwe vizuri tu .
Ha ha 😂😂 Tundu huyu huyu au tusubiri azaliwe mwingine. Kama ni huyu wa Ubeligiji Mzee haupo serious
 
Anayewaza vyema kwa sasa ni yule tu anayepanga kukinukisha kwa kudai katiba kwa mtutu! Na back up kidogo ya West!
Nyingine ni porojo.
Tuwatoe kwenye comfort zone kwanza walafi.

(IF YOU WANT PEACE START A WAR)
 
Tundu Lissu Hana uwezo wa ku-mobilise watu wa chini.

Ana vijikauli vingi sana vya dharau kama Mimi sina Hela huku anajenga ghorofa Tegeta.

Mabadiliko huletwa na watu wa chini
Tofauti ya Tundu Lissu na Magufuli ni kwamba Lissu anasoma sana na anaelewa mambo mengi sana. Kwa tabia ni kama wanafanana tu, wote wana mihemko na ni mbaya kwa kiongozi wa ngazi ya Rais.

Upinzani nikijaribu kuangalia vyama vyote pamoja na hivi vingine ambavyo viongozi ndio wanachama pekee waliopo, Mbowe pekee ndio ana utulivu wa akili wa kutosha kwa ngazi ya Urais. Labda na 'Mama Tanzania' kwa mbali.
 
Ni mama Samia suluhu Hassani Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndio chaguo la watanzania kwa Sasa, Hakuna mpinzani Wala chama chochote kinachoweza itikisa CCM kwa Sasa

Katika uongozi wa mh mama Samia suluhu Hassani ndio ameupoteza kabisa upinzani kwa kuunyima ajenda, maana anatekeleza na kufanyia kazi Kero za wananchi,

Ndio maana huwezi ukawambia watanzania habari za upinzani wakakuelewa kwa sasa,

Huyo Tundu lisu ndio maana unaona kajitulia zake huko aliko bila makerere maana ameshaona namna mama anavyofanya kazi zinazogusa maisha ya watu na namna watanzania tunavyomuunga mkono Rais wetu
 
Habari wana Jf ,kwa mara ya kwanza nimejikuta nasikitishwa sana na umasikini na Ugumu wa maisha unaoendelea kuongezeka huku kukiwa hakuna suluhisho la kueleweka Kutoka CCM .

Nimewaza sana na kujikuta naona ni Bora Tundu lissu ambae anaonekana ndiye mtu pekee kwa sasa mwenye ushawishi na uwezo wa kuongoza Nchi hasa kuiondoa CCM madarakani kupitia Chama chochote hata kipya aandaliwe na kuweza kuja kuiondoa hii CCM.

CCM imeongoza Nchi kwa zaidi ya miaka 40 lakini imeshindwa hata kuwatua kinamama ndoa za Maji mijini kote na imeshindwa kwa kiwango kikubwa katika kupiga vita Ufisadi , kuendeleza na kujenga viwanda ,kuondoa shida ya ajira ,kuboresha huduma za Afya na nk .

2025 CCM inaweza Ondoka aandaliwe vizuri tu .
Lissu hana tofauti na Magufuli, kitabia na hata kimatendo.
 
Back
Top Bottom