Kuna haja ya Umoja Party kubadili jina kwa manufaa mapana ya Taifa

Kuna haja ya Umoja Party kubadili jina kwa manufaa mapana ya Taifa

Naona unataja watu ambao mioyoni mwa watanzania wanakubalika kinoma. Pole sana, maana mlivyo wachafu hata kuingia mitaani mnaogopa. Makamba alienda kule Stigler basi akafika akashusha vioo asalimie aisee watu walimkaushia yaani walimuona ni kituko.
Nchi iko salama, na haitaongozwa kutoka chini ya kaburi au kuzimu anakoishi mwendazake pamoja na yule aliyefukuzwa mbinguni
 
Chini ya Katiba hii inayomilikiwa na wezi na Majambazi na wapigaji wa nchi hii ,hakuna Chama kizuri Wala kibaya. Nchi Haina dira hivyo inategemea rubani anauwezo wa kubahatisha au laa. Chini ya Katiba hii ya Kikoloni iliyoboreshwa na kuondolewa dira ya Taifa usitegemee Chama au mtu alifikishe sehemu sahihi Taifa hili.

Taifa lenye Mito mingi sana.
Taifa lenye gesi nyingi.
Taifa lenye Eneo kubwa la bahari na fukwe nyingi
Taifa lenye madini ya kila aina.
Taifa lenye visiwa.
Taifa lenye ardhi kubwa .
Taifa lenye mifugo wengi.
Taifa lenye wanyama wengi.
Taifa lenye Milima na mabonde ya ajabu.
Taifa lenye Jeshi la uzinzi tiifu kwa raia wanaotawala.
Taifa lenye majeshi Mengi kuliko majeshi yote Duniani( Jeshi la wanyama pori,Jeshi la uhamiaji,Jeshi la mambo,Jeshi la kujenga Taifa,Jeshi la zimamoto, Jeshi la magereza, Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi (Bado TISS) lakini ni Taifa ambalo linapigwa na wezi wa Mali za umma vibaya mno.
Taifa Lenye amani.
Taifa lenye vipaji vya kila aina kutokana na kuwa na makabila Mengi.

Taifa la Kijamaa lenye watawala Mabepari wanaojimilikisha Mali za umma na kuiboresha maisha yao huku Wanyonge wakiwa wanaufyata Kwa kutishwa na vyombo vya Dola vinavyokanyaga katiba Kwa manufaa ya watawala Mabepari.

Taifa la watu waliojengwa kinafiki na Roho mbaya.

Taifa lenye wabunge wanaotumikia serikali na matajiri badala ya Wananchi waliowatuma bungeni.
Taifa lenye serikali kubwa yenye watumiaji wengi wa Kodi ya Wananchi kuliko wazalishaji.
Taifa lenye bodi mashirika ya umma yenye bodi nyingi kuliko wafanyakazi.
Taifa lenye vyama vya ushirika vyenye wafanyakazi wanaojitajirisha Kwa jasho la wakulima huku wakulima wakibaki kuwa maskini.
TAIFA LENYE RUSHWA MKUBWA WAKATI WA UCHAGUZI NA KUPATA MAWAZIRI NA MANAIBU ,WAZIRI MKUU ,WABUNGE,MADIWANI, SPIKA ,WAJUMBE WA KAMATI ZA BUNGE NA NAIBU SPIKA WALIOZALIWA NA NGUVU YA RUSHWA NA DHULMA.

Kamwe hakuna Chama chochote kitakachoweza kupambana na Chama kinachowekwa madarakani na kulindwa na mifumo na Katiba isiyo na dira isipokua Chama hicho kipate wapinzani wa ndani wanaoamini katika Haki, usawa wa kibinadamu na utu wa mwanadamu na Demokrasia ya kweli.

Siku watu wema wakiwa wengi kuliko waovu ndani ya CCM ndipo mabadiliko ya kweli yatakapotokea.
Watu wema wanatabia Moja ya kuweza kujitoa kufa au kupoteza maslahi yao Kwa ajili ya kutetea wengine.
Yesu alifanya hivyo kama wanavyoamini wakristo.
Lakini Mtume Mohamad pia alikua mstari wa mbele kupigania haki na kuondoa dhulma Kwa umma wa kipindi chake. Hakuweka mbele maslahi yake Bali aliamini katika Haki na kupigania dini ya Allah.

Nyerere alisema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM.

Chadema wanakosea sana kushindwa kuunda Chama Cha siasa mpaka Sasa kwani kina wanachama wengi sana lakini nacho kina tatizo lile lile la CCM la kuwa na viongozi wenye uchu wa fedha na Mali kuliko uhalisia wa watanzania.
ACT ni Chama Cha wachuuzi wanaangalia dau tuu. Ni chama Cha Kijamaa chenye viongozi wenye tamaa ya fedha na Mali kama ilivyo CCM tofauti na CCM ni kwamba CCM kina mtandao mkubwa wa walaji.
CUF ndicho Chama pekee chenye itikadi japo kilipata wakati mgumu wakati wa Serikali ya awamu Ile mana kilijichanganya kinyumbaninyumbani na kuyumba.

CUF ipi? Ya Lipumba? Mna haraka ya kusahau. Tanzania vyama Ni viwili tu CCM na CHADEMA. Ndio maana CCM abakihujumu Sana Chadema maana ndio tishio kwake.
 
Naona unataja watu ambao mioyoni mwa watanzania wanakubalika kinoma. Pole sana, maana mlivyo wachafu hata kuingia mitaani mnaogopa. Makamba alienda kule Stigler basi akafika akashusha vioo asalimie aisee watu walimkaushia yaani walimuona ni kituko.

Mpina mwenyewe wavuvi hawataki kumsikia.
 
Chama cha waumini wa Magufuli.
Habari njema sana hiyo sasa wale waliokuwa wanasema jpm kaiba kula wataumbuka baada ya kukiona hicho chama kimekuwa chama chenye nguvu kwa muda mfupi kuliko vyama vyote tz ,hapo tutakuwa tumelitakasa jina la JPM ,tutakuwa tuna shambulia kwa kutumia chama cha upinzani na ndani ya ccm tunajiimalisha pia
 
Kwa sasa hali ya kisiasa nchini ilivyo.

Kinahitajika chama cha UKWELI chenye nia thabiti ya kuwakomboa wananchi dhidi ya Wahuni na wanasiasa maslahi waliotapakaa kila chama kilichopo nchini.

Kikitokea kweli na kikaaminika.........
True chama kiitwe JPM AND NYERERE LEGACY kwa kifupi kiitwe JN-LEGACY
 
Baada ya vuguvugu kubwa la kuanzishwa kwa chama cha siasa cha Umoja Party ni dhahili sasa safari imeanza lakini nna ombi moja tu tubadili Jina kuwa Chama cha Ukombozi na Umoja Tanzania (CUUTA).

Sababu kubwa ni kwamba kwanza tunahitaji kukomboa watu kifikra na kiuchumi na ndipo tuwaunganishe.

WanaJf mnaonaje?
CHADEMA inatutosha
 
Baada ya vuguvugu kubwa la kuanzishwa kwa chama cha siasa cha Umoja Party ni dhahili sasa safari imeanza lakini nna ombi moja tu tubadili Jina kuwa Chama cha Ukombozi na Umoja Tanzania (CUUTA).

Sababu kubwa ni kwamba kwanza tunahitaji kukomboa watu kifikra na kiuchumi na ndipo tuwaunganishe.

WanaJf mnaonaje?
Hakuna Chama pale , ni kikundi cha ngoma
 
Kalemani na Polepole ndio wafadhili wa hiki chama, pamoja na Luhaga Mpina na Bashiru.

Nashauri kiitwe Chato Democratic Party -CDP
IMG-20220419-WA0239.jpg
 
Kalemani na Polepole ndio wafadhili wa hiki chama, pamoja na Luhaga Mpina na Bashiru.

Nashauri kiitwe Chato Democratic Party -CDP
Hao watu waamue kuanzisha chama na kipate usajili smoothly? Ukiona hivi ujue hamna chama hapo!
 
Back
Top Bottom