Kuna hatari kizazi hiki kikaaminishwa kuwa Tundu Lissu ni moja ya Watu wabaya na sio wazalendo kwa Taifa

..msikilize Tundu Lissu akielezea historia yake na watu wa Nyamongo--Tarime.

..mtu aliyetetea Watanzania kama alivyofanya Lissu utamchafua vipi?

..Na hiyo ni Tarime, bado historia ya Lissu na wananchi wa Rufiji haijaelezwa.

 
Lissu anashutumu watu watatu kwenye tukio lake Magufuli (hayuko hai), Kipilimba (yupo nche ya nchi) na Makonda (kwa sasa ni raia wa kawaida).

Kitu gani kinachomzuia kurudi Tanzania mpaka aombe kuhakikishiwa usalama wake nani anaetaka kumdhuru; huyo Magufuli karibu baraza lake lote la mawaziri wamemgeuka kiutendaji na maoni. CCM ina watu wengine kabisa.

Kwanini Lissu bado anaogopa kurudi Tanzania ilo ndio swali au anaogopa usalama wa taifa kwa ujumla wao kutokana makosa anayoyajua yeye mwenyewe.
 
..aliwatetea Mashekhe wa Uamsho na Answar Sunna wakati wengi waliogopa kuwatetea.

 

..Mnauliza maswali ambayo yanamkandamiza victim badala ya kumtetea.

..Polisi nao wanatoa majibu ambayo yanamkandamiza victim na kuwatetea waliomshambulia.
 
..Mnauliza maswali ambayo yanamkandamiza victim badala ya kumtetea.

..Polisi nao wanatoa majibu ambayo yanamkandamiza victim na kuwatetea waliomshambulia.
Mpira upo kwa Tundu Lissu yeye ndio anajiuma uma kwa sasa kufunga.

Haya IGP hakumtafuta kama anavyodai kwanini asirudi sasa hivi aombe kwenda kusaidia ushahidi wa kesi yake kituo anachotaka badala ya kulalamika mitandaoni; walau afike aseme nimewaeleza yote awajafanyia kazi, kama ni Dodoma kamanda Muroto nae hayupo so hakuna mtu wa Magufuli.

Kwanini anaogopa mpaka leo kila kitu kimebadilika zaidi ya kuendeleza miradi ya kimkakati ya Magufuli, mama Samia anaenda na mziki wake na safu yake ya washauri binafsi ina watu wengine kabisa ambao awawezi beba personal vendettas za Magufuli awajafanya nae kazi kusema wanaweza mshawishi mama Samia ya kuwa Lissu ni adui.

In short Lissu hana sababu inayomzuia kurudi Tanzania leo; zaidi ya zile anazozijua mwenyewe. Kila mtu anamnanga Magufuli siku hizi seuse yeye akirudi akiamua kufanya ivyo.
 

..sidhani kama kutokuwepo kwa TL kunazuia uchunguzi kufanyika.

..pia inasikitisha kwamba Igp anamshambulia mhanga wa tukio baya kama lililomtokea Lissu halafu baadhi yenu mnamuunga mkono.

..Igp alitakiwa awe upande wa TL badala yake kwa kauli na mwenendo wake anaonekana kama yuko upande wa waliojaribu kumuua Lissu.

..hata kauli wanazozitoa juu ya dereva ni kana kwamba dereva ni mhalifu au mhusika, wakati dereva naye ni victim wa tukio lile.
 
Ipo siku Damu ya Lissu italipwa,Wala sio mpaka siku ya huku lakini hapahapa Na nipunde tu.
 

Mkuu mimi sio mwanasiasa. Lissu Ni Kati ya watu wa kawaida sana wasioweza kujicontrol. Na hiiyo mkuu haifutiki. So Tulia. Hawezi kuwa kiongozi hata wa choo cha Kariakoo.
 
Lisu a.k.a mzee wa kuropoka kwa kila jambo anajua yeye wengine wanakosea,huyu mzee ni wa kupuuza tu.
 

1. Kuna watu, very reliable, wanadai aliyetafuta data kuhusu makinikia siyo Lissu, ni mwanasiasa mwingine wa upinzani.

2. Suala la makinikia halikuwa na data au information zozote ambazo ni sensitive. Zile ripoti hazikuwa za taarifa za kuaminika na ndio maana hatukuambulia chochote na sasa hivi huzisikii zikitajwa na mtu yeyote.

3. Serikali na Polisi kushindwa kutoa majibu ni nani aliondoa walinzi area D aliposhambuliwa Lissu kunawafanya wadadisi waamini kwamba wauwaji walikuwa na watu wazito nyuma yao.

4. Polisi hawaonyeshi kama wana nia ya kuchunguza. Ni jambo la ajabu Polisi kuonekana hawana hamasa ya kuchunguza na kukamata wahalifu.

5. Waliomshambulia Lissu wangekamatwa serikali na Magufuli wangejizolea sifa nyingi. Inashangaza jinsi ambavyo Magufuli hakutoa msukumo au msisitizo kwamba waliohusika wasakwe na kuchukuliwa hatua.

6. Pia inashangaza kwamba Magufuli hakuwa mstari wa mbele kumsaidia Lissu. Magufuli aliyesaidia matibabu ya Ruge Mtahaba, Mzee Majuto, Askofu Ruwaichi, Dr.Kigwangala, Jenerali Mritabu,...kwanini hakujitokeza kumsaidia Tundu Lissu?

7. Wito na ombi la Tundu Lissu kwamba vyombo vya uchunguzi vya kimataifa visaidie kuchunguza shambulizi dhidi yake lilikataliwa. Hakuna sababu za msingi kwa serikali kukataa ombi hilo kwani lina faida kwa serikali kuliko kwa Tundu Lissu.
 
K
Kampeni Lissu ameanza mapema sana! Anatafuta huruma kwa ajili ya 2025! Atachoka.
 
Ukweli ni kwamba Tanzania watu wenye Akili, weledi na misimamo thabiti hupigwa vita na wajinga wengi waliomo CCM
Mimi si mwana CCM ila sikukubaliana na Lissu kabisa kwenye suala la kuwatetea Acacia kwenye makinikia pamoja na suala la kutetea ushoga.
 
..haiwezekani kuwadanganya.

..kijijini kwetu hata mtoto ambaye hajaanza shule anamjua Lissu na machachari yake.
Hawa wanasiasa hasa wa Chadema ni wachumia tumbo tu. Lissu ni makamu wa mwenyekiti lakini jimboni kwake Ikungi ofisi ya Chadema ni kama choo licha ya chama chake kupata ruzuku ya zaidi ya bilioni tatu kila mwaka siku za nyuma.
 
Hawezi kurudi, watu wanadai kuna kitu kanogewa.
 
Hawa wanasiasa hasa wa Chadema ni wachumia tumbo tu. Lissu ni makamu wa mwenyekiti lakini jimboni kwake Ikungi ofisi ya Chadema ni kama choo licha ya chama chake kupata ruzuku ya zaidi ya bilioni tatu kila mwaka siku za nyuma.

..ccm wanatembelea V8 huku shule zetu hazina matundu ya vyoo, wananchi hawana maji safi na salama, na matatizo mengine lukuki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…