Ngoja nikusapoti kwa visa hivi viwili vya kweli kabisa na kimoja ni cha miaka ya KARIBU Sana Sana
1. Miaka kadhaa nasoma A'level nilikua kama boya Tu, sikua na influence kihivyo na maisha hayakua mazuri sana japo hayakua mabaya Sana, alikuja Jamaa Mmoja, aiseee jamaa hajawahi hata kunisalimia, of course alikua Sahihi maana sikua wa "type" yake. Tulipokua chuo, huko Dar - UDSM nilishangaa napigiwa simu, tena miaka ile Ninamiliki Motorola C25, Jamaa alijitambulisha Sana Kwangu kuwa tulikua wote Darasa moja ila kwa kweli sikumkumbuka, nikakubali tuonane. Anyway, kwa kifupi Jamaa niliishi nae room moja Kwa gharama zangu kwa kipindi chote cha maisha ya UDSM.
Sikuwahi kumkumbusha Lolote la A"level Baya, Chuo nilimlisha Mimi tangu day one Hadi mwaka wa tatu nadhani alipopata Mkopo baada ya Serikali kusema kuwa mikopo ni ya wanafunzi wote, bado baada ya hapo alipomaliza Chuo hakuwahi kunitafuta na yeye alitangulia kupata KAZI Serikalini tena position nzuri Tu.
Huyu Jamaa Hadi ninavyoandika hapa, atanitafuta akiwa na Shida Tu ila wewe ukiwa na Shida ukamcheki aiseee trust me, huwezi ambulia hata elfu kumi. Ni maisha, nafurahi YANGU yanaenda na yake pia.
Kisa kingine, NAOMBA nisitaje mwaka, niliwahi kufanya KAZI kwenye NGO hizi kubwa Tu hapa nchini, tukapata Mradi Mkubwa sana na Sisi tukawa ndio PR (Prime recipient), kwahio kibunda nilikuepo, kama staffs WA ule Mradi tulikua na group letu la WhatsApp la kwetu Tu ukiacha lile la shirika, kwa bahati mbaya Sana, Mradi ule ulikatishwa mwaka wake wa tatu wa implementation, sasa wenzangu (baadhi) walihamishiwa kwenye miradi mingine na mashirika mengine, kwa bahati mbaya, akina Mimi tukaishia hapo.
Kwa kawaida Ile group iliendelea ku-exist na socialization za hapa na pale, sasa buana, kipindi tuko pale kuna mshkaji Sijui alikua na issue Gani ila mara nyingi sana alikua anaishiwa pesa kabla ya Muda wa salary, Nikawa nampiga tafu Sana na anarejesha bila Shaka.
The day nimekaa bench na yeye alikua miongoni mwa waliopata KAZI kwa NGO nyingine, maana ilikua kama Ile project zinafanana Tu, basi huwezi amini kuna siku nimebanwa na Niko kitaa, nikamrukia hewani jamaa, huwezi kuelewa but Jamaa alinitosa kama sio Mimi vile niliyekua msaada kwake, nikajaribu tena siku nyingine, nikadunda, basi sikuwahi kumcheki tena ila tupo wote kwa group na mara moja moja tunasalimiana japo wengine walivyofanikiwa Tu vipindi kile cha mpito na Kwa group wakajitoa.
Funzo, ishi maisha yako, usitarajie kutenda mema ili ulipwe mema! Mafanikio ya mwenzako got nothing to do with you!