Kuna jamaa yangu alikua USAID akawa ananifungia vioo, leo kanitumia ujumbe kama nina mchongo wowote nimpasishie

Kuna jamaa yangu alikua USAID akawa ananifungia vioo, leo kanitumia ujumbe kama nina mchongo wowote nimpasishie

Kwa kweli kama Mungu alikuinua na wewe ukawa kwenye nafasi ya kuwainua wenzako kwa makusudi kabisa ukaamua kuwaacha wazame kwenye dhiki huku wewe ukifurahia raha inaumiza sana hasa ikiwa ni mtu wako wa karibu.......

Ni kweli msaada sio haki yako lakini na wewe kama ulisaidiwa kwa namna moja au nyingine kufikia hapo ulipo basi ni vyema na wewe ukawatazama wenzako kwa jicho la kibinadamu kwa kile utakachojaaliwa........

Kuwatumia watu kuvuka madaraja ya mafanikio na kisha kuwatelekeza huo ni USHETANI....na sio katika matendo ya kibinadamu......

Watu wema hukumbuka fadhila bali wale wabaya na waovu hujitia upofu......

Unapowakataa watu nyakati za DHIKI zao ukiwa kwenye mafanikio yako basi waache moja kwa moja.....kurudi tena kutaka msaada kwa watu walioukufadhili alafu ukawakimbia hizo ni dharau.....na kebehi......

Maisha ni safari ndefu sana kuna leo lakini hakuna ajuaye kesho yake.......kwani kesho ni fumbo.......

Kumuacha mtu wako karibu kwenye hali NGUMU na wewe Una nafasi ya kumsaidia huo ni USHETANI......

Hata muumba anatufanyia mema na yeye anapenda tumlipe mema kwa kumuabudu lakini tukimfanyia uovu anatuandikia dhambi........
 
- Hivi kwa nini baadhi ya watu wakifanikiwa wana watenga wenzao?
Watu wanatenga Hadi Wazazi wao sembuse mtu back?

Kuna Mzee alikuwa analalamika kusomesha mtoto wake ambae anafanya kazi Wizara ya viwanda huko anadai ameacha kwenda kwake,akirudi halali kijijini huko nk

Sasa anasema hamtaki ila akija atamoa vyakula lakini hampi urithi wowote wa mang'ombe kama buku hivi atampa ambae gajasoma.na Yuko nae huko Kijijjini.
 
Unajua maana ya urithi wewe?
 
Una Roho ya kimaskini, ulichokifanya kimekuweka kwenye position ya kufanana nae, namshukuru MUNGU sijawahi kuwa na Roho ya kimaskini Kiasi hiki.

Nikikusaidia na ukafanikiwa, nitafurahi Sana, ukifanikiwa kabla Yangu, namshukuru MUNGU maana najua na Mimi Kesho Yangu ipo, nikifanikiwa kwa namna Yoyote ile, nitafurahi kuona nakua na Msaada Kwako.

Kama Una ubaya ni wa Kwako Sio wa Kwangu, siwezi kuumia kwa MTU mwingine kufanikiwa (mafanikio mema lakini) au siwezi kufurahia MTU mwingine akipata shida. Hii ndio Imani Yangu.
Inapunguza stress na unnecessary makasiriko
Ok
 
Kuna watu sijui ni ulimbukeni au ushamba.

Huyu jamaa yangu yeye alibahatika kupata kazi tu after graduation kwenye hizi NGO zilizokua chini ya USAID, kwa kipindi kile kijana mdogo kulipwa 3m per month ilikua ni pesa nyingi mno.

Jamaa akaanza maringo na akawa anatuona akina sisi ambao by that time tulikua majobless sio wa standard zake. Imepita miaka kadhaa hatimae Trump kafanya yake huko.

Jamaa leo kanitumia ujumbe eti nikisikia au kama nina mchongo wowote nimpasishie. Nimemjibu me niko nalima kijijini kwetu kama unaweza njoo tupige jembe, huo ndio mchongo nilionao kwa sasa.

Jamaa hajajibu kitu.
Wewe una akili za kimaskini sana. Ulitaka uwe mnufaika wa mshahara wake?
 
Ila wafanya kazi kwenye makampuni waliotegemea misaada ya USAID hivi sasa kila mahala ni kilio, wanatia sana huruma, wengine wameanza kutembeza CVs zao kwenye makampuni mengine..

Ila mzee sijui utakavyomtangaza msela, kama hadi umemfungulia nyuzi basi jamaa atatubu na hatorudia, kuwa makini umbea utakaopiga na wenzako inawezekana jamaa akajua, ujue kumfungulia nyuzi mtu, ina maana ndugu, majirani, mkeo hadi mtaa umewapa hii story..
Mleta uzi ataingia motoni kwa dhambi ya kipuuzi sana inayoitwa usengenyaji.
 
Hakika Amekwisha, aanze kuuza hata maandazi kama hawezi kulima
Kuna watu sijui ni ulimbukeni au ushamba.

Huyu jamaa yangu yeye alibahatika kupata kazi tu after graduation kwenye hizi NGO zilizokua chini ya USAID, kwa kipindi kile kijana mdogo kulipwa 3m per month ilikua ni pesa nyingi mno.

Jamaa akaanza maringo na akawa anatuona akina sisi ambao by that time tulikua majobless sio wa standard zake. Imepita miaka kadhaa hatimae Trump kafanya yake huko.

Jamaa leo kanitumia ujumbe eti nikisikia au kama nina mchongo wowote nimpasishie. Nimemjibu me niko nalima kijijini kwetu kama unaweza njoo tupige jembe, huo ndio mchongo nilionao kwa sasa.

Jamaa hajajibu kitu.
 
Mssamehe tu mkuu, watu wengi wako hivyo. Mimi classmate wangu mmoja aliwahi kuoata kazi benki moja hivi, akapata vijisenti wakati wengine bado tunajitafta, akawa na maringo mengi sana hata kwenye group la darasa letu wa mwaka wetu akajitoa. Miaka michache iliyopita nadhani pale kazini paliota nyasi, akaanza kututafta ambao hatukua na chochote( kwa sasa tuna zaidi ya chochote)

Akaanza kuomba akopeshwe elfu 20, mara 30 eti atalipwa siku flani, siku flani. Akaanza kuomba akopeshwe kiwango cha pesa ambacho mimi siwezi kumkopesha mtu, below 100k sikukopeshi, nakupa tu, sasa ajabu mtu ananiomba nimkopeshe elfu 20 au 30 nikajiuliza sasa hii inamsaidia nini huyu boss?

Mpuuze tu mkuu.
Kumbe unakopesha na sijui!!
 
Back
Top Bottom