Serikali inatakiwa ku - cut off some spending kwenye baadhi ya maeneo ambayo hayana athari za moja kwa moja kwa maisha ya watu na kinachokuwa saved kutolewe kama subsidy kwenye sekta ya umeme na mafuta ili kuleta nafuu ya maisha kwa wananchi..
Mathalani tunaweza ku - cut off spending kwenye maeneo haya inagalau ktk kipindi hiki cha mpito wa hali ngumu ya kiuchumi:
1. Ondoa au fupisha vikao vya bunge la bajeti toka miezi mi3 hadi wiki 2 tu.
2. Ondoa safari zote zisizo za muhimu za viongozi..
3. Futa hiki kinachoitwa "mbio za mwenge wa uhuru" kabisa.
4. Futa warsha na semina zote zisizo na umuhimu.
5. Suspend kutoa pesa kwenye baadhi ya miradi inayoendelea sasa. Hapa umakini ni muhimu sana kwa sababu projects hizi mara zote huhusisha mikataba ya kimataifa..
##Kwa kufanya haya, mabilioni ya fedha yataokolewa na hizo fedha sasa zifanye haya;
1. Zitolewe kama subsidy kwenye maeneo ya huduma hususani kwenye sekta ya mafuta na umeme ambazo zinaathiri maisha ya watu kila siku..
2. Lipa marupurupu na mishahara mizuri kwa watumishi wa umma na binafsi ili fedha hiyo in return iingie kwenye mzunguko wa uchumi, ichangamshe uchumi..
## Mimi siyo mwana uchumi, lakini UONGOZI ni bongo/akili tu ya kufikiri na kupanga mipango mizuri inayotekelezeka
## Na kama hizi steps zitachukuliwa, mwananchi wa kawaida hawezi ku - feel au ata feel maumivu haya ya kiuchumi kidunia kwa kiwango kidogo sana..!!