Labda kwenye gas niseme hili
1. Sehemu ndogo ya gas itokayo Mnazibay ndiyo inayotumika kuzalisha umeme Mtwara na umeme huo, kuilisha mikoa ya Mtwara na Lindi. Sina uhakika kama umeme huo umeungwa kwenye grid ya taifa kwa huko Mtwara au Lindi
2. Sehemu kubwa ya gas itokayo Mnazibay (M&P), inaungana na gas itokayo Songosongo (PanAfrica) pale Somanga na kuelekezwa Dar (Ubungo na Kinyerezi) kwa ajili ya uzalishaji wa umeme unaoingizwa kwenye grid ya taifa
3. Gas itokayo Mnazibay na Songosongo inapelekwa pale TBL Dar kwa ajili ya Production ya vinywaji (Unajuwa ulipaji wa kodi wa TBL)
4. Gas itokayo Songosongo na Mnazibay, inapelekwa Twiga cement kwa ajili ya uzalishaji wa cement
5. Gas itokayo Mnazibay, kwa sasa imepelekwa mtaani huko Mtwara kwa ajili ya matumizi ya majumba
6. Gas itokayo Mnazibay na Songosongo, imepelekwa baadhi ya mitaa huko Masaki Dar kwa ajili ya matumizi ya majumbani
7. Kioo limited nao nimepewa taarifa kwamba wanatumia gas itokayo huko kusini kwenye uzalishaji wa vioo vyao
8. Kuna kipindi, Dangote Cement nao walikuwa kwenye mazungumzo ili waipate gas hii kwenye uzalishaji wa cement yao. Sijui wamefikia wapi
9. Kuna kitu kinapatikana kama BY-PRODUCT baada ya kuisafisha gas, kinaitwa CONDENSATE.. Malori kwa malori kila baada ya muda fulani, huenda pale Madimba kuikusanya (kwa kununua) na wao huitumia kutengeneza plastic, sabuni etc
Hivyo, ukiangalia hayo maelezo hapo juu, utaona jinsi gasi hii inavyotumika kitaifa...
Tatizo wana siasa wameacha kuizungumzia gas hiyo, au hata wakiizungumzia inatajwa in a NEGATIVE WAY, kiasi kwamba nyie msiofahamu habari ya gas inazalishwaje, inasafishwaje na inasafirishwaje na nini kinapatikana baada ya kuisafisha MNAYABEBA YA WANASIANA NA MNAONA KAMA VILE HAINA MAANA