Tetesi: Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...

Tetesi: Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...

Aibu JWTZ badala ya kulinda mipaka na maisha ya watanzania
Bado wako bize kulinda masilahi ya chama pendwa
JWTZ walienea mpaka wote lkn kuna taarifa kwamba walipunguzwa kwa sababu ya maandalizi ya uchaguzi.

Kwa bahati mbaya sana eneo la Kitaya ni eneo ambalo mto Ruvuma haujapanuka sana kwahiyo ni rahisi watu wa upande mmoja kuvuka kwenda upande mwingine.
 
Hii hali JWTZ waingilie mapema wakipuunza hadi kipindi cha uchaguzi historia ya Tanzania itabadilika.
 
Labda kwenye gas niseme hili

1. Sehemu ndogo ya gas itokayo Mnazibay ndiyo inayotumika kuzalisha umeme Mtwara na umeme huo, kuilisha mikoa ya Mtwara na Lindi. Sina uhakika kama umeme huo umeungwa kwenye grid ya taifa kwa huko Mtwara au Lindi

2. Sehemu kubwa ya gas itokayo Mnazibay (M&P), inaungana na gas itokayo Songosongo (PanAfrica) pale Somanga na kuelekezwa Dar (Ubungo na Kinyerezi) kwa ajili ya uzalishaji wa umeme unaoingizwa kwenye grid ya taifa

3. Gas itokayo Mnazibay na Songosongo inapelekwa pale TBL Dar kwa ajili ya Production ya vinywaji (Unajuwa ulipaji wa kodi wa TBL)

4. Gas itokayo Songosongo na Mnazibay, inapelekwa Twiga cement kwa ajili ya uzalishaji wa cement

5. Gas itokayo Mnazibay, kwa sasa imepelekwa mtaani huko Mtwara kwa ajili ya matumizi ya majumba

6. Gas itokayo Mnazibay na Songosongo, imepelekwa baadhi ya mitaa huko Masaki Dar kwa ajili ya matumizi ya majumbani

7. Kioo limited nao nimepewa taarifa kwamba wanatumia gas itokayo huko kusini kwenye uzalishaji wa vioo vyao

8. Kuna kipindi, Dangote Cement nao walikuwa kwenye mazungumzo ili waipate gas hii kwenye uzalishaji wa cement yao. Sijui wamefikia wapi

9. Kuna kitu kinapatikana kama BY-PRODUCT baada ya kuisafisha gas, kinaitwa CONDENSATE.. Malori kwa malori kila baada ya muda fulani, huenda pale Madimba kuikusanya (kwa kununua) na wao huitumia kutengeneza plastic, sabuni etc

Hivyo, ukiangalia hayo maelezo hapo juu, utaona jinsi gasi hii inavyotumika kitaifa...

Tatizo wana siasa wameacha kuizungumzia gas hiyo, au hata wakiizungumzia inatajwa in a NEGATIVE WAY, kiasi kwamba nyie msiofahamu habari ya gas inazalishwaje, inasafishwaje na inasafirishwaje na nini kinapatikana baada ya kuisafisha MNAYABEBA YA WANASIANA NA MNAONA KAMA VILE HAINA MAANA
 
Siamini maaana Jeshi letu lipo macho ktk mipaka yetu yote na haswa mpaka wa Msumbiji na Mtwara, usalama upo wa uhakika, hakuna wa kutishia usalama wa watanzania Jeshi letu liko Imara sana.
 
Amboni na kibiti ni kazi mujarab za Jeshi tukufu la Polisi.
Mkuu una uhakika na ulichoandika?

Iko hivii? Mambo yanapoharibika ndani ya nchi hukabiliwa na polisi na ndiyo hubeba dhamana ya operesheni husika, ndiyo maana ulikuwa ukisikia polisi, polisi hafi mwisho bila ya wanajeshi kutajwa.

Polisi wanapozidiwa kiutendaji ama ki mbinu,huomba msaada wa jeshi kusaidia ama kuingilia kati na ndivyo ilivyokuwa kwa opersheni hizo za kibiti na Amboni.

Elewa kwamba kikosi kizima cha Marine Commandos pamoja na wanajeshi wengine wa Jwtz kutoka maeneo mbalimbali nchini walishirikishwa kwenye operesheni hiyo na kupelekea kupata ufanisi mkubwa katika utokomezaji wa magaidi hao.
 
Hivi vikundi vya kigaidi havina mbabe kabisa.

Tena hao JW unaowataja wanaweza wakawa wabovu zaidi.

Mpaka leo licha ya Israel kuwa na Teknolojia kubwa lakini bado inahaha na mambo haya.

Ni kuomba Mungu aepushe suala hili.
Nasikia hali ni tete,tuombe kwa umoja wetu ili hawa watu waondoke lakini operation kama ile ya kibiti inahitaji huko, ili kuwamaliza kabisa
 
IMG_20201015_175052.jpg
 
Kama tuliwasambaratisha magaidi hewa wa mapango ya amboni kule tanga hatuwezi kuwashindwa hawa....

Kazi ya jwtz nj kulinda mipaka sasa mpaka wanaingia walikua wapi?
 
Uvamizi wa mipakani ni mbaya sana.

Wasije wakatengeneza vichochoro vya kupitisha silaha then tukafanya uchaguzi kwa kutumia vyuma.
 
Back
Top Bottom