Tetesi: Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...

Tetesi: Kuna jambo baya linaendelea Mtwara...

Kama watawapata wafanye hivyo.Ila ujue vita havina macho.
Katika kusaga unaweza kujikuta nawe unasagwa pia.

Kwanza ni muhimu kujua nia yao ni nini?
Maana wao huwa wanasema wazi wanafanya hivi kwa sababu gani.
Katika hili tusiwe lelemama eti tutalaumiwa na umoja wa mataifa - saga hao watu kabisa, yaani wasagwe kiasi kwamba wakisikia neno Tanzania wanajificha -wasituzoee kabisa
 
Sasa ndugu mbona wanaoumia ni RAIA wasio na hatia?Unaposema dawa ya mjinga ni kuumia,je unadhani hao wanaotakiwa kuchukua hatua wanaumia kweli?

Mungu awanususuru wanyonge maana yeye pekee ndiye mtetezi wao
Swala hili limeanza muda Sana, toka enzi ya Kibiti,mkuranga na ikwiriri mauaji Yale!
Sasa tunayosikia na kuona Ni matokeo ya Operation MKIRU,

Kuna uzembe umefanywa na vyombo vyetu vya ulinzi, hil lazima tukubali uzembe umefanyika,

Hawa jamaa waliopo msumbiji taarifa zao zipo toka 2015 , na mipango ilishafanyika tatizo uzembe ktk utekelezaji!

Kwanini walifanikiwa kuweka kambi ya jeshi mji wa kibiti?

Kwanini wameshindwa kufanyia kazi swala la mpaka na msumbiji km ilivyo ktk mipango na malengo ya kuwakabili Hawa Jamaaa?

Dawa ya mjinga Ni kuumia

Hivyo tunavuna tulichopanda!!

Ushauri: Jeshi hasa viongozi waandamizi wafanyekazi kwa uweledi bila kukubali tutumika na viongozi wakisiasa wasiojua athari za wafanyayo zaidi ya kutaka madaraka tu!!
 
Wazee leo katika mishe mishe Sina hili Wala lile nikapokea simu ya dogo wangu ni mwanajeshi kambi flani akaniambia bro niko safarini naelekea Mtwara.

Katika kunieleza akasema kule kuna Hawa Islamic State wameingia na mbaya zaidi walimkamata mwanajeshi wamemuua na wakamkata kichwa. Pia kuna habari kwamba wameteka watu zaidi ya 30. Sasa basi juzi waliitisha kikao kambini na kupewa maelekezo na wameanza safari ya kuelekea mtwara huko kupambana na hawa magaidi.

Katika kumuuliza zaidi na kuomuombea kwamba Mungu amlinde na wamelize zoezi salama huku nikiwa na mshituko kidogo dogo akaniambia usiwe na wasiwasi tuko vizuri na tumejipanga pia tumebeba siraha nzito nzito yani tukifika ni Moto tu paka waelewe yani kimsingi tuko vizuri

Daah hili nalo linakichanganya kwamba wamebeba siraha nzito na za kutosha huko kuna nini?

Kwa wanaojua je huko kumetokea Nini na kwa Nini serikali Kama hakuma taarifa za haya matukio?

Yote kwa yote nawaombea Askari wote wanaoenda huko na dogo pia Mungu awe nao na warudi salama
In God we trust[emoji123]
Mungu atalilinda jeshi letu na dogo atarudi salama
 
Nimebahatika kuona video jamaa wamemchinja mtu kwa nyuma ya shingo Hadi kichwa kimetolewa alaf mmoja akaamuru kiwekwe barabarani.

Hao wavamizi wanaongea kiswahili kizur Sana na wanajitambulisha kuwa ni Alshabab kutoka msumbiji na ili kuthibisha wapo Tz wakaenda had kwenye picha ya kampen ya mgombea rais wa CCM huku wakitaja na jina la Kijiji, Kuna picha baadhi inaonyesha wameteka kifaru cha jeshi.

Hii kitu ipo serious sana wazee japokua taarifa zinafichwafichwa lakin ni vyema watu wawe na tahadhari sana.
weka hyo vdeo tuione
 
Kilichopo tu ni kwamba baada ya 'Wahuni' hawa 'Wanamgambo' kuondolewa na JWTZ kwa 'style' ambayo hawatakuja Kuisahau huko Mkuranga, Kibiti na Rufiji 'walipoichokoza' Tanzania baadhi yao hasa wale Waandamizi wao walikimbilia nchini Msumbuji ambako ndiko kuna Ngome yao Kuu na hata walipokuja huku Pwani na kule Amboni Tanga walitokea huko huko.

Taarifa nilizothibitishiwa na Chanzo kutoka katika 'Kikosi Maalum' ni kwamba hawa 'Wahuni' wanatamba na kusumbua sana tu huko nchini Msumbuji japo kwa miezi kama Saba ( 7 ) hivi iliyopita walikuja maeneo ya mpakani na Tanzania ila kutokana na 'Intelligence' imara ya Tanzania na ile ya Jeshini ( CMI ) waliweza 'Kudhibitiwa' na wakakimbilia huko 'Ngomeni' Kwao Msumbiji.

Na ni kweli kwamba 'Wahuni' hawa ( ambao ni Wanamgambo ) wana 'Vifaa' vikubwa tu na uwezo mkubwa wa Kivita hasa hii ya Msituni ( Guerrilla ) na 'Mafunzo' makubwa sana ya 'Kivita' hali ambayo imefanya mpaka wameweza 'Kupambana' vilivyo na 'Jeshi' dhaifu kwa sasa la Msumbiji na kuweza kuteka Bandari muhimu huko ambayo inawasaidia Kuwaingizia Kipato na 'Kutamba' pia.

Kuna taarifa tulipewa kuwa Wanajeshi wa Tanzania ( JWTZ ) sijui 'wametekwa' na Kukimbia hadi Kukiacha 'Kifaru' huku tukiaminishwa kwa 'Video' ila ukweli ni kwamba kilichoonekana siyo 'Kifaru' bali ni 'APC' nadhani wale Watu wa 'Medani' hapa mtakuwa mnaelewa na si vibaya pia mkija kutusaidia zaidi 'Kutuelimisha' juu ya hiki Chombo.

Kuhusu Picha ( Poster ) ya Mgombea Urais wa CCM ( sasa ni Rais ) Dkt. Magufuli kuonekana kwa hawa Wahuni ( Wanamgambo ) ni sehemu tu ya 'Propaganda' ya Watu wenye 'Chuki' na Tanzania na hasa ikiwa inaelekea katika Uchaguzi Mkuu huu ujao kama 'Kuichafua' na hata Kuzua 'Hofu / Tafrani' miongoni mwa Watanzania na hasa hasa Wakazi wa huko Mtwara.

Tumeambiwa kuwa kuna Watanzania 'waliokufa' huko na kwamba hali ni ya 'wasiwasi' mno huko Mkoani Mtwara hasa eneo la Nanyamba ila ukweli ni kwamba eneo liko salama kabisa tena 100% na hakuna 'Mauwaji' yoyote yale isipokuwa Jeshi la Tanzania ( JWTZ ) kwa Kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vimeendelea tu 'Kuimarisha' Usalama huko.

Kilichonishangaza zaidi GENTAMYCINE ni kwamba nina Ndugu zangu huko na nimefanya 'Jitihada' za 'Kudadisi' kama kuna 'sintofahamu' ya aina yoyote ile inayohatarisha Amani huko ( kama tunavyoaminishwa ) nilichojibiwa tu ni kwamba Mtwara iko salama. Na nawaombeni nanyi wana JF pia mjaribu Kuwasiliana na Watu wenu huko ili muweze 'Kujihakikishia' juu ya hili.

Nimalizie tu kwa Kuishukuru Serikali ya Tanzania chini yake Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Magufuli pamoja na Vikosi vyote vya Ulinzi na Usalama nchini Tanzania kwa 'Kupuuza' na Kuunyamazia 'Uzushi' huu ambao 'unaratibiwa' vyema kabisa na wale wasioitakia mema nchi yetu na kutaka kuleta 'taharuki' hasa wakiwa na lengo la Kuitia nchi 'Doa' la Kiusalama na Amani yake.

Asante sana na mno Wewe 'Chanzo Changu' kutoka hapo 'Kikosi Maalum' juu ya hili na Mimi nimeamua 'Kushea' hapa na Watanzania wenzangu.
Acha uongo ww
 
Duuh huu uzi umerejeshwa last week kila ukitupiwa humu ulikuwa unaondolewa haraka.
Tuna Imani na jeshi letu watafanya kazi kutokana na weledi waliofunzwa
Ila hawa magaidi Wana kiswahili kizuri Kama wabongo.​
 
Duh! Mbona hii hatari sasa, tatizo la Watanzania, huwa hawataki kuungana na majirani kwenye kupambana na haya magaidi, tuliwaambia uhusika wetu Somalia huwa tunapambana kuhakikisha mashababi hayaoti mapembe na kuvuruga ukanda wote wa Afrika Mashariki, tunawafuata hadi kwenye shina.

Watanzania wamekua wakichekelea na kukunja mikia kwa uwoga huku majirani wote wakiwemo Uganda, Rwanda n.k. wakipeleka majeshi yao Somalia wamesahau kuna vijana wa Kitanzania wengi tu wameenda kupata mafunzo ya ugaidi Somalia, na tunao ambao wamekamatwa Kenya wakifanya ugaidi.

Vivyo hivyo Tanzania imekua ikionyesha udhaifu na uzembe kwenye vurugu za Msumbiji, wanaambiwa kwamba raia wao Watanzania haswa ndio magaidi kule, wanachekelea na kunyamaza, sasa hayo magaidi yameanza kugeuza na kurudi nyumbani. Yanachoma vijiji na kukata watu vichwa, halafu huwa siyaelewi haya magaidi, unaua wanavijiji ili iweje, hovyo sana bladi mani na zao.

Magaidi wanapaswa kuuawa bila huruma, Watanzania acheni uwoga, uzembe na udhaifu, unganeni na wenzenu kwenye hili pambano, hawa vijana hawapaswi kuogopwa, wapewe moto kama dawa.
Uko sahihi mkuu, yule chatu anayemeza watoto wa jirani kule Msumbiji ameanza kumeza wa huku kwetu, juhudi za kikanda zinahitajika kushughulikia hili maana nchi moja pekee haitaweza kutatua hili tatizo kwani ugaidi hauna mipaka.
 
Back
Top Bottom