econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Kuna jambo nalitafakari kwa kina na ninadhani watu wengi hawajaliona Wala kulifikiria. Iwapo Lissu atafanyiwa figisu kwenye uchaguzi ndani ya CHADEMA na akatimkia ACT Nini kitatokea? Hili Jambo watu hawalioni.
Lissu akihamia ACT ndio utakuwa mwisho wa CHADEMA kama chama kikuu Cha upinzani. Maana ataipa back up huku bara na kuwa chama chenye ushawishi mkubwa, na kule visiwani tayari ACT Ina mizizi. Ndipo kwama mara ya kwanza tutapata chama chenye kuungwa mkono Zanzibar na bara.
Hili Jambo nimelitafakari kwa kina Sana nikawaza itakuwaje?. Naomba Wana CHADEMA wenzangu tufanye uchaguzi kwa haki, atakaye shindwa aone ameshindwa kwa haki na tusikubali pesa zikatufanya tufanye maamuzi batili. Tuiangalie CHADEMA ya kesho sio Leo au Tusifanye uchaguzi wa kumpendeza mtu hapana, tufanye uchaguzi kwa Nia ya kuleta mabadiliko ndani ya CHADEMA.
Wakati wetu ni Sasa, tusiruhusu chama chetu kikapotea au kufa kwa sababu za kibinafsi za maslahi ya wachache, tumchague mgombea mwenye maono mapya na mwenye kujua uchungu wa harakati. Tusifanye makosa kabisa, Tanzania inatutegemea. Tusurudie makosa ya RENAMO Msumbiji mpaka ikapitwa na chama Cha PODEMOS kwa ushawishi na uungwaji mkono.
NB.
Siiamini ACT na Wala sidhani Kama kina Nia ya dhati ya kuiondoa CCM madarakani.