A
Anonymous
Guest
Habari,
Mimi ni mzazi nawakilisha wazazi wenzangu ambao wamechoshwa na kero hii. Mimi ni Mkazi wa Kibaha Manispaa, mkoa wa Pwani. Tumechoshwa na kero ya michango mashuleni hasa shule ya Msingi Mkuza iliyopo kata ya Picha ya Ndege kituo cha daladala maarufu kwa Mbonde
Wamekuwa na utaratibu wa kukusanya hela za chakula ili watoto wale wawapo shuleni shida inakuja kwa wasiotoa hela ya chakula wanachapwa fimbo za mgongoni ili watoe hizo hela je nisawa?
Na wanaotoa hela chakula ni kidogo sawasawa na tonge mbili za wali pia mwalimu wao mkuu amekua na utaratibu wa kuwaandikisha hawa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa hela kama mzazi hana hiyo pesa haandikishi!
Unakuta wazazi wengine hali ya kimaisha ni duni watoto wao hawaandikishwi na pia anapokea watoto hewa ambao hawajaandikishwa wanasoma tu bila kuandikishwa mpaka watakapo toa hela je hii ni sawa???
Mwenzangu ameambiwa atoe laki moja ndio mwanae aandikishwe.
Naomba mamlaka husika ifuatilie hili jambo! Kwani ni kero sana kwetu ikiwezekana kwa kuwahoji wanafunzi kwa njia ya maandishi