KERO Kuna kero ya Michango ya Uandikishaji na Chakula Shule ya msingi Mkuza

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari,

Mimi ni mzazi nawakilisha wazazi wenzangu ambao wamechoshwa na kero hii. Mimi ni Mkazi wa Kibaha Manispaa, mkoa wa Pwani. Tumechoshwa na kero ya michango mashuleni hasa shule ya Msingi Mkuza iliyopo kata ya Picha ya Ndege kituo cha daladala maarufu kwa Mbonde

Wamekuwa na utaratibu wa kukusanya hela za chakula ili watoto wale wawapo shuleni shida inakuja kwa wasiotoa hela ya chakula wanachapwa fimbo za mgongoni ili watoe hizo hela je nisawa?

Na wanaotoa hela chakula ni kidogo sawasawa na tonge mbili za wali pia mwalimu wao mkuu amekua na utaratibu wa kuwaandikisha hawa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa hela kama mzazi hana hiyo pesa haandikishi!

Unakuta wazazi wengine hali ya kimaisha ni duni watoto wao hawaandikishwi na pia anapokea watoto hewa ambao hawajaandikishwa wanasoma tu bila kuandikishwa mpaka watakapo toa hela je hii ni sawa???

Mwenzangu ameambiwa atoe laki moja ndio mwanae aandikishwe.

Naomba mamlaka husika ifuatilie hili jambo! Kwani ni kero sana kwetu ikiwezekana kwa kuwahoji wanafunzi kwa njia ya maandishi
 
Hapo picha linaanza subiri wawe field ndio hautaacha kuona kila rangi

Shule zinawajasiliamali wakutosha

Ukute mwalimu ameweka target ndani ya miaka mitano ijayo lazima na yeye awe na nyumba kali na usafiri ili aheshimike ukweni

Hakuna wizara mbovu kama ya Elimu na sijui kama ipo

Watoto mijini Wanakuwa kama popo wanarudi majumbani usiku mwingi mpaka inatia huruma
 
Admin mimi ni mzazi na mjumbe wa shule nipo mkoa wa Pwani Manispaa ya Kibaha kata ya Picha ya ndege shule ya Msingi Mkuza

Ndugu admin naomba niseme kero yangu katika hii shule huu mchango wa Chakula umekua haupendezi kutokana na mbinu wanayotumia kudai michango walimu hao wawili wanachapa sana watoto mwalimu mkuu msaidizi wa hii shule anaadhibu sana watoto fimbo zisizo na idadi wala kutofata kanuni ya utoaji wa adhabu

Hii inapelekea utoro kwa wanafunzi ambao wanakuwa wamekosa kiasi cha fedha kinachohitajika pia watoto kukosa AMANI katika ujifunzaji wao

Pia chakula kinachopikwa hakina kiwango stahiki na amekua na lugha mbaya hata wazazi wanapofuatilia kuhusu hili jambo tunaomba mamlaka itusaidie kufatilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…