GE2025 Kuna kila dalili CCM wakakatisha kampeni. Sababu ni hizi hapa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
4.Zomea Zomea haiwezi tokea sababu 99% ya wahudhuriaji ni waajiriwa serikalini,wanajeshi,jkt, na makundi mengine yote yasiojulikana

Hawa wote kazi yao ni kupika kelele za kushangilia, lakini ingekua mikutano inajazwa na wananchi wa kweli sisi tulioko Mtaani ZOMEA ZOMEA ingeanzia siku ile ile kampeni zinazinduliwa pale KAWE.

Imeshindikana sababu lile nyomi lote ni lao wenyewe yani ni Baba amekaa na wanae chini anawahubiria, unategemea kuna mtoto atamzoea baba ake?

CCM ni lidude likubwa sana kuliangusha inabidi kutafuta punch za maana sana ila hv hv sijui kama tutaweza.

Hawashindwi kuwachukua Diaspora walioko mataifa huko wakawaleta kwenye kampeni hawashindwi na ndio ninachokiona.

Kuna CCM wengi sana nchi za wenzetu naamini wamebebwa wote wameletwa TZ na watakuepo mpka KAMPENI na UCHAGUZI uishe wapige kura ndipo warudishwe nchi zao.

ZIle BILIONI zilizokusanywa msifikiri ni za kueka benki ni za kulipia watu VISA,TICKET waje nchini kutimiza jambo.

CCM wanashindaga kwa tekniki nyingi na moja ya TEKNIKI kubwa inayowafanya wasitoke madarakani ni UWEZO WAO WA KIPESA hili li chama hamna linachoshindwa kuna MENGI pole pole hajayasema sababu bado yeye ni MWANA CCM ila kuna uhuni unaendelea chini ya KAPETI ambao ni kiapo OLE WAKO UUROPOKE na POLE POLE Hawezi uropoka huo UHUNI na ndipo Point 3 za ushindi wa CCM zilipojificha.
 
Sasa tuanze kwenda mikutano yao kwa lengo la kuzomea tu, ianze sasa hii campaign mkuu
 
Aaha, kumbe unafikiri hivyo!!???

View: https://youtu.be/GtZS0v0W32I?si=if0CuobNGl56Ik6C
 
Tutafute namna ya kuwatoa sisiem, uzeni mawazo yenu chanya ili utawala wa hawa wakoloni wa ndani ukome. Nyinyi ndiyo wasomi wetu jamii hii yote inategemea mawazo mapya kutoka kwenu kuelekea mabadiliko.
CCM must go
 
Kwa hiyo we pendekezo lako ni lipi??
 
We unadhani ni kwa nini Nchimbi amesukumiziwa kanda ya ziwa?
 
Mshana, naamini wewe ni mkongwe, ccm Hawa ambao hawasikii! Wala hawana Soni kabisa!! Hawa dawa Yao ni mapinduzi ya umma tu!! Ndio lugha wanayoweza sikua!! Hizi lugha zingine sijui nani kaongea, hizo kwao ni kekele za mlango!! Unamjua Kenge? Kenya wanamwita mbulukenge, Ili asikie kuwa amepigwa, hula laxima atoke damu maskini, hapo ataona amepigwa!! Ccm waliko fikia, wanahitaji kipigo hasaa ndio wataelewa!! Inabidi tufanye mapinduzi ya umma!! Tena tushughulike na familia zao.
 
Baada ya hizi Ramli na utabiri mnanufaika nini๐Ÿ˜๐Ÿ˜ Kila jambo mnatabiri na halitokei mnasahau utabiri wa mwanzo mnatabiri kingine tena hadi mnazeeka kichwa kimechoka kwa ramli zisizo na uhalisia au motokeo
 
Iiko hivi.. Wanawasomba vizuri wanawafikisha mpaka eneo la tukio kisha wakifikishwa tu wanasepa๐Ÿ˜‚
Sasa wakisepa watarudije makwao? Mfano jana Ngere ngr.tufanye umetolewa Kinguluwila au Moro mjini. Halafu watarudije? Dawa ni kugoma kabisa kwenda.
 
CCM wanashindaga kwa tekniki nyingi na moja ya TEKNIKI kubwa inayowafanya wasitoke madarakani ni UWEZO WAO WA KIPESA hili li chama hamna linachoshindwa kuna MENGI pole pole hajayasema sababu bado yeye ni MWANA CCM ila kuna uhuni unaendelea chini ya KAPETI ambao ni kiapo OLE WAKO UUROPOKE na POLE POLE Hawezi uropoka huo UHUNI na ndipo Point 3 za ushindi wa CCM zilipojificha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ