Acha kushikiwa akili na wanasiasa uchwara wewe. Ni aibu kuona kijana kama wewe umezaliwa ili utumiwe na wanasiasa uchwara ambao wao watoto wao wako ulaya na marekani wakitengeneza maisha yao na ya wazazi wao ( hao wanaokutumia)
Nchi moja kuingia mkataba na nchi nyingine haimaanishi kwamba serikali imeshindwa, bali ni katika uboreshaji wa mbinu za kiuchumi.
Hii dp world ndio inayoendesha bandari za Marekani, Uingereza na nchi nyingine kubwa ambazo wenye akili na wafuatiliaji wa mambo ya dunia wanazifahamu.
So wewe unafikiri raisi wa Marekani au Queen Elizabeth wa Uingereza hawakuwa na uwezo wa kuendeleza bandari zao hadi kuwakabidhi hao jamaa?
Je wao hawana jeshi, fbi, cia nk?
Hawana matajiri wa kuziendesha bandari zao?
Akili za kuambiwa changanya na zako, usiwe kama bata anaerushiwa tunge la ugali na kukimbilia kulimeza bila kufikiri labda sometimes anaweza kuwekewa jiwe katikati ya tonge ili baadae lije kumdhuru.
Shtuka kijana, acha kutumiwa na wapiga deal, wakwepa kodi bandarini na wapitisha madawa ya kulevya.
Wenzio wanapiga kelele ili kupambania kitumbua chao pale bandarini afu wewe unaishia kutumia bando lako, pumzi yao na nguvu zako kupigania ulaji wao.