nadhani hujamuelewa, kile anachokiwasilisha hapa ndicho pia ninachokiwaza. CHADEMA ya sasa sio tena ile iliyowafanya wananchi wengi kuipenda na kuiamini kuwa ilikuwa mbadala wa CCM katika kushika mamlaka ya kuiongoza nchi yetu.
Hii ya sasa ipo kujipoza na machungu waliyoyapata kutoka katika awamu ya JPM, ni kweli waliteseka sana hilo halina ubishi, ila wengi wa viongozi hao muda umewatupa mkono hivyo walichoamua ni kuendelea kuwepo katika medani za kisiasa za nchi hii kwa namna ambayo hawaathiriki au kudhurika kama hapo awali... hawapo tena kwa ajili ya wananchi bali kwa ajili yao na mitazamo yao binafsi.
Falsafa ya viongozi wa CHADEMA kwa sasa inaendana msemo kuwa "if you can't win them, join them"... bahati mbaya au nzuri hata sie tulioipenda ile CHADEMA ya kina Dr. Slaa (wa mwanzo), Mbowe (wa mwanzo, aliyewafundisha CCM kutumia chopa), Heche, Wenje, Lema (wa mwanzo), Zitto (wa mwanzo), Lwakatare (wa mwanzo), Mnyika(wa mwanzo), Halima na Esta (wa mwanzo) tulishawatangulia kwenda CCM kwa kuwa upinzani hauna mbinu sahihi za kufanikisha kile wanachokihubiri majukwaani.
Pengine CHADEMA ingeimarika kungekuwa na mabadiliko ya uongozi. Jambo ambalo halionekani kabisa kama litawezekana kwa siku za karibuni. Viongozi wa upinzani wanapenda wafe na vyama vyao.