Kuna Kila dalili tukapata coalition ya CCM na CHADEMA kabla 2025 huku bara

Kwenye madaraka ni ngumu.

Labda kuteuana kwenye nafasi za kawaida tu Kama ilivyokuwa inafanyika kwa MBATIA.

Ila kwa nafasi za kikatiba Kama PM, Makamu Rais ni ngumu. Hata Speaker tu ngumu
Kwani mbunge wa jimbo "a" akipelekwa "futi sita chini" halafu kukatangazwa uchaguzi jimbo hilo "a", na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani akaambiwa gombea pale ili hatimaye uwe PM, hili haliwezekani kufanyika na kufanikiwa!!!??
 
Nina mashaka makubwa kama unajua siasa vizuri wapinzani wanapaswa kubaki kuwa wakosoaji ambapo kila kitu anachokifanya mtawala watafute hoja ya kusahihisha. Hii ya kumkubali mwenykiti wa chama tawala kiasi Cha kumpa tuzo ni kwamba mnautangazia umma na dunia Kwa ujumla kwamba mna Imani sana na huyo mwenykiti wa hicho chama tawala. Kama mna Imani kiasi cha kumtunuku tuzo why tusiamini kwamba
Mtamkampenia uchaguzi inayofuata?
 
Kama ambavyo wewe na wahafidhina wenzako hamna chenu ndani ya chama chenu chini ya mwenyekiti wenu aliyewapa pigo la karne!!!??
Nilitegemea uainishe mbinu ambazo Mbowe anataka kuwatega ccm kumbe unakuja na kejeli
 
Serikali ya mseto yaweza tu kuwepo baada ya uchaguzi.
Kinachoweza kufanywa kwa sasa ni katiba mpya yenye uwezekano wa kuunda serikali ya mseto. Sababu kuu zikiwa;
1. Mama ni mwanamke hivyo kukosa kura nyingi kwa sababu ya mfumo dume (tamaduni, mila zetu na hata dini zinamshusha mwanamke).
2. Mama anatoka visiwani (Zanzibar), hivyo ubara, ukabila au ukanda unaweza kuathiri kura zake kwa asilimia kubwa..
Kwa sababu hizo mbili juu, watu wa mama (siyo chawa), inatakiwa kazi na mbinu za ziada kuhakikisha anashinda.
 
Ni njaa za viongozi wa cdm tu lakini kwenye ulimwengu ww siasa za hoja katu huwezi panda jukwaani ukasifia pande hasimu... Ulimwengu wa sasa utasimama eti uponde utawala wa Magufuli wa ccm afu uje usifie utawala wa Samia ambaye alitamka wazi kwenye kampeni zake kuwa CCM itashinda kwa namna yoyote.
TL ameupuuza upuuzi wa cdm na Mbowe kufanywa kutaka kuwa praise timu. Cdm inahitaji shape mpya ya viongozi vijana watakaoendana na siasa za sasa, Mbowe kujifanya bwana busara kumbe analamba asali ni upuuzi wa kiwango cha SGR..... Saizi cdm ni ya hovyooo afadhali na Ashimu Rungwe.
 
CHADEMA ninayoifahamu ya tangia siku za Mkapa haikuwahi kuwa na mtazamo laini kuelekea CCM kama ilivyo leo.
Ulishawahi kuona Mwenyekiti wa CCM taifa akitembelea Jukwaa Kubwa la Chadema tangu tupate Uhuru??

Sasa utashangaa chadema wakimuunga mkono?
 
Kwa nini umewatoa Chawa😅😅
 
Wazee wa mapanga shaa! Mnazidi kuumbuka.
 
Ulishawahi kuona Mwenyekiti wa CCM taifa akitembelea Jukwaa Kubwa la Chadema tangu tupate Uhuru??

Sasa utashangaa chadema wakimuunga mkono?
Sijawahi kuona na sii tu kutowahi kuona ila kwa namna ambavyo upinzani ulikuwa agressive dhidi ya ccm sidhani kama wangethubutu kumualika kiongozi wanayemshutumu Kwa mambo kibao eti aje kwenye jukwaa lao.
Kiufupi ni kwamba chadema wamempa mama jukwaa rahisi sana la kuwamaliza kisiasa. Lile vibe alilopata mama pale lililipa sana Kwa ccm Kwa hiyo ninadhani mama Kwa huruma zake ataweza kuwazawadia walau viti kadhaa vya udiwani na ubunge ikibidi hata nafasi za uteuzi jambo ambalo sio baya hata kidogo hii nchi ni yetu sote.
 
Kama ambavyo wewe na wahafidhina wenzako hamna chenu ndani ya chama chenu chini ya mwenyekiti wenu aliyewapa pigo la karne!!!??
Ukiisoma vizuri michango yangu ya mawazo utagundua kuwa mimi sio mhafudhina hata kidogo ila labda kama huu msamiati ni mgeni kwako
 
Kwani mbunge wa jimbo "a" akipelekwa "futi sita chini" halafu kukatangazwa uchaguzi jimbo hilo "a", na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani akaambiwa gombea pale ili hatimaye uwe PM, hili haliwezekani kufanyika na kufanikiwa!!!??
Linawezekana,tena simpo tu,tena uko kupelekana futi sita ni mbali sana,tunamwambie achage moja,arejeshe kadi yetu au aandike barua ya kujiuzuru,halafu tunamtafuta mbunge mwingine dhaifu,anakosa vikao kadhaa vya bungee,tunamtoa Jimbo linakuwa wazi,tunamtoa ubalozi maisha yanasonga
 
Kwani mbunge wa jimbo "a" akipelekwa "futi sita chini" halafu kukatangazwa uchaguzi jimbo hilo "a", na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani akaambiwa gombea pale ili hatimaye uwe PM, hili haliwezekani kufanyika na kufanikiwa!!!??
Rubbish
 
Natamani itoke hii kitu, tupate upinzani wengine waamshe nchi hii.
 
Binadamu msio na jema nyie!. Kumbe we ni mmoja wa wahafidhina mliotajwa katika hotuba ya Rais Samia. We ulitaka iweje, kwa mfano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…