Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili za lolote kutokea katika Uchaguzi wa Mwaka huu

Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili za lolote kutokea katika Uchaguzi wa Mwaka huu

Hivi sasa ukipita mitandaoni, utaona kabisa kuna aina fulani ya watu kuanza kuhamasishana kuhakikisha haki inatendeka katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na wanasiasa ndio wanaonekana kuwa mstari wa mbele kuhakikisha haki inapatikana.

Ukisikiliza clip zao mitandaoni na kusoma wanayoyaandika,utaona ni kama watu ambao wameamua liwalo na liwe iwapo kuna watu wanapanga au kukusudia kuharibu huu uchaguzi na kwa mtazamo wangu, naona kabisa wanasiasa hawa wako desparate kwa kiasi kikubwa.

Naziona pia dalili za wanasiasa hawa kuweka tofauti zao pembeni na kutengeneza coalition isiyo rasimi ili kupitia coalition hii, wasimame pamoja iwe mvua iwe jua.

Dalili pia zinaonyesha wana taarifa za nini kimepangwa au nini kinaweza kutokea hivyo na wao wanajiandaa kukabiliananazo.

Kingine nacho kiona ni wanasiasa wa chama fulani kikongwe kuungana na hawa wa upande wa pili either kwa uwazi au kwa kuwaunga mkono chini kwa chini, na hali hii inaweza kuwa serious zaidi iwapo mchujo wa wagombea katika chama fulani utafanywa kibabe.

Naziona pia dalili za wanasiasa hawa kunufaika na uungwaji mkono mkubwa kutoka nje iwapo kuna mambo yasiyofaa yatatendeka.

Mtaji wa wanasiasa siku zote ni watu, na mtaji huu safari hii unaundwa na watu ambao kwa namna moja au nyingine, teyari ni wahanga ndani ya miaka hii mitaoni hivyo lolote laweza tokea.

Hivyo,busara ikokesekana,tunaweza shuhudia ambayo hatukuwahi kuyashuhudia.

Wasituletee mambo ya Maalim Seif huku. Analianzisha alafu anakimbia arabuni tena kwa fedha za umma na familia yake kula bata, huku anaacha watu wakikanyagana kuepuka vibomu.

Kwa safu hii 👇🏿 wanapenyea wapi wenye kudai haki au kutaka kukinukisha?

Mkuu wa jeshi la polisi, mwenye dhamana ya kutuhakikishia usalama = KANDA MAALUM

Mkuu wa Majeshi yote nchini, ´´mwenye uwezo wa kuamua kieleweke na kikaeleweka `` = KANDA MAALUM

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, mwenye dhamana ya kutangaza mshindi/mshindwi = KANDA MAALUM

Mkuu wa watoaji haki mahakamani, jaji mkuu = KANDA MAALUM

Mkuu wa waganga wa kienyeji na wachawi nchini = KANDA MAALUM
 
Uzuri ni kuwa iwe mvua liwake jua hiyo form anaichukua tu
Kama umeshiriki unaelewa kwann huyu mpiga yowe hatakiwi kupewa fomu. Bora azipigie yowe akiwa nje, akiruhusiwa akaingia ndani huo usumbufu wake vuvuzela lina afadhali. Naelewa kabisa kwann hatakiwi kuingia ndani huyu.
 
Membe tu anawatisha ndani ya chama, huku nje ndio kabisa huyo mtu wenu atakataliwa na wengi.
Kama ni tishio mchukueni nyinyi awe mgombea wenu,awasaidie na hicho kitisho chake.maana chadema hamna mgombea mpaka Sasa!!!
 
Mkuu hiyo tarehe bado ipo kwenye mabano sana ebu yafungue basi
07/07/2020..ni tarehe muhimu sana kwa wapenda haki...kwn haki huinua Taifa...kukiwa na Tume huru, bc hata mshindi hupatikana kwa haki
 
Ugoro mtupu
Wasituletee mambo ya Maalim Seif huku. Analianzisha alafu anakimbia arabuni tena kwa fedha za umma na familia yake kula bata, huku anaacha watu wakikanyagana kuepuka vibomu.

Kwa safu hii [emoji1541] wanapenyea wapi wenye kudai haki au kutaka kukinukisha?

Back
Top Bottom