Shibalanga
Senior Member
- Mar 1, 2011
- 178
- 93
Kwa mgeni wa siasa za Tanzania anaweza ukampa hizo bashiri au lamli zako lakini kwa mtu aliyeshuhudia chaguzi za Tanzania kuanzia mwaka 1995 baada ya vyama vingi yaani ni sawa na kusema ni mvinyo ule ule tofauti kifungashio tu, hakuna uchaguzi uliowahi kuwa mgumu kama wa mwaka 1995 kipindi anagombea Mrema na mwingine ni wa 2015 alipogombea Lowassa, wanaojua siasa za Tanzania watakubaliana na mimi, uchaguzi huu ni kutimiza takwa la katiba tu hata wao washindani wanajua hakuna wa kumshinda John Pombe Magufuli, ukweli huu kuna watu wanajisahaulisha tu! Fanyeni utafiti kidogo tu hasa vijijini ambako ndiko watanzania waliko achaneni na taralila za watu wa mjini kwenye mitandao ya kijamii ambao kimsingi kwanza huwa hawajitokezi kujiandikisha na hata siku ya kupiga kura.Hivi sasa ukipita mitandaoni, utaona kabisa kuna aina fulani ya watu kuanza kuhamasishana kuhakikisha haki inatendeka katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na wanasiasa ndio wanaonekana kuwa mstari wa mbele kuhakikisha haki inapatikana.
Ukisikiliza clip zao mitandaoni na kusoma wanayoyaandika,utaona ni kama watu ambao wameamua liwalo na liwe iwapo kuna watu wanapanga au kukusudia kuharibu huu uchaguzi, na kwa mtazamo wangu, naona kabisa wanasiasa hawa wako desparate kwa kiasi kikubwa.
Naziona pia dalili za wanasiasa hawa kuweka tofauti zao pembeni na kutengeneza coalition isiyo rasimi ili kupitia coalition hii, wasimame pamoja iwe mvua iwe jua.
Dalili pia zinaonyesha wana taarifa za nini kimepangwa au nini kinaweza kutokea hivyo na wao wanajiandaa kukabiliananazo.
Kingine nacho kiona ni wanasiasa wa chama fulani kikongwe kuungana na hawa wa upande wa pili either kwa uwazi au kwa kuwaunga mkono chini kwa chini, na hali hii inaweza kuwa serious zaidi iwapo mchujo wa wagombea katika chama fulani utafanywa kibabe kwa kutegemea Bwana fulani ameamkaje siku hiyo.
Naziona pia dalili za wanasiasa hawa kunufaika na uungwaji mkono mkubwa kutoka nje iwapo kuna mambo yasiyofaa yatatendeka.
Mtaji wa wanasiasa siku zote ni watu, na mtaji huu safari hii unaundwa na watu ambao kwa namna moja au nyingine, teyari ni wahanga ndani ya miaka hii mitaoni hivyo lolote laweza tokea.
Hivyo,busara ikokesekana,tunaweza shuhudia ambayo hatukuwahi kuyashuhudia.