KUNA KIMFUKO KIDOGO CHA KARATASI NIMEKIKITA KWENYE MKOBA WA MKE WANGU

KUNA KIMFUKO KIDOGO CHA KARATASI NIMEKIKITA KWENYE MKOBA WA MKE WANGU

Tafu
1; Tafuta unga tofauti na huo ila uelekee kufanana na huo,weka kwenye kimfuko kama ulivyokuta halafu rudisha mkobani.
2; Tunza unakojua wewe halafu tulia kana kwamba hakuna ulichoona.
3; Weka mbadala wa hicho ulichokuta,halafu hayo mazaga yapeleke ofisini kwa Mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi,peleka kiasi na kiasi endelea kuficha.
4; Usipende kuwa na sehemu yako maalumu ya kukaa (kwenye sofa kaa kwa hamahama) ikiwezekana geuza vya kukalia juu chini uone kinacho ning'inia huko.
5; Ikiwezekana epuka matumizi ya mto wa kulalia.
6; Usipende kula pekee yako,wala kumtuma eti niletee maji ya kunywa.
7; Oya,kaa CHONJO.
Eti asile peke yake wala kuletewa maji. Maisha gani hayo sasa? Kwa nini asimuulize tu?
 
Shemela tukienda jamaa ataweka uzi, "Wana jeiefu wawili wamefika nyumbani kukiangalia kimfuko cha mke wangu"
Hahahahah. Na sisi tutapanda na uzi kimfuko cha mke wa mwanajf kilikuwa na chumvi aliyobakiza wakati anakula maembe mabichi.
 
Hii inaonyesha huna imani naye hata kabla ya kukiona kifuko chake.Ungekuwa na imani na mkeo wala usingefungua mkoba wake.Yeye ndo anakupikia ,anakufulia,,anakutayarishia maji nk.Je hayo yote akitaka kujufanyia utayaona? Dawa ni kuwa na imani naye ili usipate stress
 
Nadhani una hoja muhimu. Si jambo zuri kwa mwenza kuwa na imani na nguvu za giza (kama ni lengo la hako kamfuko), ingawa wote hatujui. Hata hivyo, dwa za kienyeji zipo na zinatibu matatizo ya kawaida. Ila majibu unaweza kuwa nayo wewe mwenyewe kuliko sisi wana JF.

1. Kama mna changamoto ya uzazi huenda ameitafuta kwa ajili ya kujaribu kutibu tatizo hiko na si kosa

2. Kama mna shida ya tendo la ndoa vilevile huenda ametafuta dawa kwa ajili ya hilo

3. Kama mmoja wenu ana chronic illness vilevile, sana sana magonjwa Kama UTI na magonjwa ya sehemu za siri nk watu wengi huamini miti shamba hutibu, ingawa linaweza kuwa ni reoccurring probably kutokana na mmoja kujitibu na mwingine kubaki anamwambukiza mwenzake.

4. Worst-case scenario ni kama anaamini mitishamba katika kudeal na vitu kama mapenzi, migogoro ya ndoa, michepuko etc. Chukua hatua kabla hujatiwa uzezeta, hii ni pamoja na kurejesha mapenzi kwake, mwenzako kashindwa kuvumilia.

But all in all tafuta namna nzuri ya kujua ni nini, huenda ni dawa ya kuua mende tu, au local facial scrub bibiye anatafuta namna ya kupendezesha ngozi yake. Possibilities ni nyingi mno.
 
Itoe nyamaza ficha mbali.. Uone anakuwa je.. Vizia simu za kujificha usikilize.

Kama ni ya kazi kwako.. Subiria utaona ingine ndani kwako..

Mbele ya yote Sala muhimu na sadaka.
 
Ndio maana halisi ya Mwana kulifind Mwana kuliget kutafuta yasiyo kuhusu Mwanamke cha msingi watoto wafanane na wewe tu
 
Yaelekea unamuogopa sana mkeo, kwa nini unashindwa kumuuliza yeye uje utuulize sisi wakati kitu umekiona wewe?Wacha hizo
 
Wanaume wa siku hizi mnadeka
Sasa hiko si cha kumuuliza mkeo tu.. kwani hadi uje ushtaki humu
 
Usimuulize kitu tafuta kimfuko kingine weka kahawa kisha mrudishie

Kwa kuwa ni mkeo anza kufuatilia mienendo yake kama utaweza tafuta zile mini spy camera weka hapo nyumbani yeye asijue na usimfanye ajue

Hii itakusaidia kujua hicho ni nini na nia yake ni nini
Yote hayo ya nini sasa na asimuulize? Watu wanatembea wana mambo mengi ukute alikutana na masai akanunua dawa ya vidonda vya tumbo, maumivu ya miguu, fungus, sukari, presha ya kupanda na kushuka, akasema ngoja nikajaribu kunywa afu cha ajabu ameiweka kwenye mkoba toka aliinunua akasahau😀😀😀
 
Habari zenu?
Kuna kitu kimenipa mashaka,,nilikuwa napanga vitu ndani, ghafla MKOBA WA MKE WANGU ukawa umedondoka,,Kuna KIMFUKO Cha nailoni kulikuwa kimefungwa fundo kilitoka kwenye MKOBA wake,, kiukweli kimenipa Wasiwasi,,,nilikifungua ndani yake Kuna kama unga unga hivi wa kahawia, kiukweli nimekuwa na Wasiwasi.,,,hata sielewi,, nifanye Nini kwa sasa,,,ili kuang'amua hiking kitu.

NIMEWEKA PICHA HAPO CHINI NDUGU ZANGU👇👇👇
Heroins
 
Eti kwamba jf members wanaeza kuwa na majibu sahihi kuliko mkeo? Mbona kama hakuna ndoa hapo mnaishi kwa kuviziana, kitu kama hiko ukute ni cha kawaida kabisa ila badala ya kumuuliza umekuja kutuuliza kina sisi tukupe majibu ya kubomoa familia yako
 
Eti kwamba jf members wanaeza kuwa na majibu sahihi kuliko mkeo? Mbona kama hakuna ndoa hapo mnaishi kwa kuviziana, kitu kama hiko ukute ni cha kawaida kabisa ila badala ya kumuuliza umekuja kutuuliza kina sisi tukupe majibu ya kubomoa familia yako
 
Wanaume wanawaogopa wake zao, hawawezi kuwa-face.

Watu wanaishi kama digidigi, kujifichaficha, huku wanachunguzana, hawako huru.

Fikra za kishirikina.
 
Back
Top Bottom