KUNA KIMFUKO KIDOGO CHA KARATASI NIMEKIKITA KWENYE MKOBA WA MKE WANGU

Eti asile peke yake wala kuletewa maji. Maisha gani hayo sasa? Kwa nini asimuulize tu?
 
Shemela tukienda jamaa ataweka uzi, "Wana jeiefu wawili wamefika nyumbani kukiangalia kimfuko cha mke wangu"
Hahahahah. Na sisi tutapanda na uzi kimfuko cha mke wa mwanajf kilikuwa na chumvi aliyobakiza wakati anakula maembe mabichi.
 
Hii inaonyesha huna imani naye hata kabla ya kukiona kifuko chake.Ungekuwa na imani na mkeo wala usingefungua mkoba wake.Yeye ndo anakupikia ,anakufulia,,anakutayarishia maji nk.Je hayo yote akitaka kujufanyia utayaona? Dawa ni kuwa na imani naye ili usipate stress
 
Nadhani una hoja muhimu. Si jambo zuri kwa mwenza kuwa na imani na nguvu za giza (kama ni lengo la hako kamfuko), ingawa wote hatujui. Hata hivyo, dwa za kienyeji zipo na zinatibu matatizo ya kawaida. Ila majibu unaweza kuwa nayo wewe mwenyewe kuliko sisi wana JF.

1. Kama mna changamoto ya uzazi huenda ameitafuta kwa ajili ya kujaribu kutibu tatizo hiko na si kosa

2. Kama mna shida ya tendo la ndoa vilevile huenda ametafuta dawa kwa ajili ya hilo

3. Kama mmoja wenu ana chronic illness vilevile, sana sana magonjwa Kama UTI na magonjwa ya sehemu za siri nk watu wengi huamini miti shamba hutibu, ingawa linaweza kuwa ni reoccurring probably kutokana na mmoja kujitibu na mwingine kubaki anamwambukiza mwenzake.

4. Worst-case scenario ni kama anaamini mitishamba katika kudeal na vitu kama mapenzi, migogoro ya ndoa, michepuko etc. Chukua hatua kabla hujatiwa uzezeta, hii ni pamoja na kurejesha mapenzi kwake, mwenzako kashindwa kuvumilia.

But all in all tafuta namna nzuri ya kujua ni nini, huenda ni dawa ya kuua mende tu, au local facial scrub bibiye anatafuta namna ya kupendezesha ngozi yake. Possibilities ni nyingi mno.
 
Itoe nyamaza ficha mbali.. Uone anakuwa je.. Vizia simu za kujificha usikilize.

Kama ni ya kazi kwako.. Subiria utaona ingine ndani kwako..

Mbele ya yote Sala muhimu na sadaka.
 
Ndio maana halisi ya Mwana kulifind Mwana kuliget kutafuta yasiyo kuhusu Mwanamke cha msingi watoto wafanane na wewe tu
 
Yaelekea unamuogopa sana mkeo, kwa nini unashindwa kumuuliza yeye uje utuulize sisi wakati kitu umekiona wewe?Wacha hizo
 
Wanaume wa siku hizi mnadeka
Sasa hiko si cha kumuuliza mkeo tu.. kwani hadi uje ushtaki humu
 
Yote hayo ya nini sasa na asimuulize? Watu wanatembea wana mambo mengi ukute alikutana na masai akanunua dawa ya vidonda vya tumbo, maumivu ya miguu, fungus, sukari, presha ya kupanda na kushuka, akasema ngoja nikajaribu kunywa afu cha ajabu ameiweka kwenye mkoba toka aliinunua akasahau😀😀😀
 
Heroins
 
Eti kwamba jf members wanaeza kuwa na majibu sahihi kuliko mkeo? Mbona kama hakuna ndoa hapo mnaishi kwa kuviziana, kitu kama hiko ukute ni cha kawaida kabisa ila badala ya kumuuliza umekuja kutuuliza kina sisi tukupe majibu ya kubomoa familia yako
 
Eti kwamba jf members wanaeza kuwa na majibu sahihi kuliko mkeo? Mbona kama hakuna ndoa hapo mnaishi kwa kuviziana, kitu kama hiko ukute ni cha kawaida kabisa ila badala ya kumuuliza umekuja kutuuliza kina sisi tukupe majibu ya kubomoa familia yako
 
Wanaume wanawaogopa wake zao, hawawezi kuwa-face.

Watu wanaishi kama digidigi, kujifichaficha, huku wanachunguzana, hawako huru.

Fikra za kishirikina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…