Kuna kiongozi yeyote wa CCM kalaani kauli ya RPC wa Dodoma kuhusu binti aliyebakwa?

Kuna kiongozi yeyote wa CCM kalaani kauli ya RPC wa Dodoma kuhusu binti aliyebakwa?

Siko hapa kuwatetea polisi, polisi wa Tanzania wana matatizo mengi sana.

Lakini, mpaka sasa sijaelewa kosa halisi la polisi kwa muktadha wa maongezi haya ni nini.

Kwa mujibu wa maelezo ya msemajinwa polisi (attached hapi juu post #6), RPC kaulizwa kama huyo binti alikuwa anajiuza. RPC akajibu hata kama binti alikuwa anajiuza, hakustahiki kufanyiwa hivyo.

Muandishi wa habari kaandika kuwa RPC kasema binti alikuwa anajiuza. Hatuoni hapo kuwa alichosema RPC na kilichoandikwa na muandishi ni vitu viwili tofauti?

Kama alichoandika msemaji wa polisi ni sahihi, muandishi akiandika hivyo kwa kutokujua au kwa kupotisha makusudi ili auze magazeti yake tu?

Naona kama kwenye thread hii, kwa hoja hii soecificalky, mpaka sasa, watu wanaoshutumu polisi wanaenda kwa mazoea na bila evidence wala fact.

Tunajua polisi wetu wanakosea sana, lakini pia tunajua kuwa waandishi wetu wa habari wanaharibu reporting sana.

Sasa, kwa kujua hayo yote na kusoma communique ya msemaji wa polisi, tunawezaje kujiridhisha polisi alisema nini na muandishi wa habari alichoandika kinaendana vipi na uhalisia wa alichosema polisi?

Muandishi wa habari ana recording ya sauti ya polisi ili kukanusha madai ya msemaji wa
Baada ya RPC wa Dodoma kutoa kauli inayoonekana kuhalalisha kitendo cha binti kubakwa, watu wengi wakiwemo wanasiasa na wanaharakati, wamelaani kauli ile na kutaka RPC awajibishwe.

Hata kuondolewa kwa huyu RPC bila shaka ni matokeo ya watu waliopoza sauti na si vinginenyo.

Swali ni je, kuna kiongozi hata mmoja wa CCM aliejitokeza hadharani na kulaani hiyo kauli?

Inashangaza sana hata Raisi wa nchi japo ni mwanamke, sijui kama amewahi kutoa kauli yoyote kuhusu hili tukio walau kufariji umma wa watanzania kuhusiana na hili tukio.

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
ALITAKIWA AHOJIWE KABLA NA UFANYIKE UCHUNGUZI .NATUACHE RPC HUYU INAMAANA VYOMBOVUA UCHUNGUZI WAMESHINDWA KUTATUAJAMBOHILI AMBALO NI JEPESIKABISAAAA WASTAKIWA WAPO MTENDEWA YUPO WANAKWAMA WAPI HIZI ZINAWEZAKUA SINEMA
 
Na mpaka sasa, kwa kuangalia rekodi ya majibizano, muandishi anaonekana alipotosha, tena inavyoonekana ni kwa makusudi ili auze gazeti lake tu
Hauna rekodi ya majibizano kati ya RPC na mwandishi, mpaka sasa licho unacho ni alichosema RPC na mwandishi tu.
 
Mwananchi sio wajinga na wapo makini balaa hasa baada ya ishu ya mchechu kuwageukia.
Kama wapo makini hivyo, waweke audio ya mazungumzo ya muandishi wao na RPC tusikie wenyewe kilichosemwa na tujue kama polisi wana spin. Au watoe hata kauli ya kupinga maneno ya polisi.

Mpaka sasa Polisi wamesema Mwananchi wameandika habari za uongo, lakini Mwananchi hawajajibu wala kukanusha kauli hiyo ya polisi.

Huo si umakini.

Wameharibiwa credibility, kitu ambacho ni muhimu sana kwa chombo cha habari.

Sasa chombo cha habari kilichoharibiwa credibility na kukaa kimya tu utakiitaje makini?
 
Sijasema RPC hajakosea. Mpaka sasa watuhumiwa kutofikishwa mahakamani tu ni issue. Nimetaja hii kama issue hapo juu.

Na mpaka sasa, kwa kuangalia rekodi ya majibizano, muandishi anaonekana alipotosha, tena inavyoonekana ni kwa makusudi ili auze gazeti lake tu

Kama hajapotosha, ajitokeze na kuweka rekodi yake sawa.

Hizi habari za asingekuwa salama zinatuondoa kwenye mazungumzo yaliyo evidence based tunaleta conjecture.

Waandishi wa habari wanatakiwa kusimamia haki za wanajamii wote.

Sasa muandishi wa habari gani anayesingiziwa uongo yeye mwenyewe na kukaa kimya tu?

Yani ni hivi, hata kama polisi wanamzushia muandishi wa habari kuwa kawazushia uongo polisi, muandiahi wa habari kukaa kinya bila kujibu ni kosa.
Watuhumiwa tayari wameshafikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka. Tusubirie uamuzi wa mahakama
 
Baada ya RPC wa Dodoma kutoa kauli inayoonekana kuhalalisha kitendo cha binti kubakwa, watu wengi wakiwemo wanasiasa na wanaharakati, wamelaani kauli ile na kutaka RPC awajibishwe.

Hata kuondolewa kwa huyu RPC bila shaka ni matokeo ya watu waliopoza sauti na si vinginenyo.

Swali ni je, kuna kiongozi hata mmoja wa CCM aliejitokeza hadharani na kulaani hiyo kauli?

Inashangaza sana hata Raisi wa nchi japo ni mwanamke, sijui kama amewahi kutoa kauli yoyote kuhusu hili tukio walau kufariji umma wa watanzania kuhusiana na hili tukio.

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Ushasikia walawiti na wabakaji wa mali na binadamu wanalaani wenzao?!
 
Hauna rekodi ya majibizano kati ya RPC na mwandishi, mpaka sasa licho unacho ni alichosema RPC na mwandishi tu.
Naam,

Na rekodi mpaka sasa inaonesha polisi wamewaita Mwananchi waongo, Mwananchi hawajajibu.

Ukiitwa muongo, usipojibu, unaonekana umekubali kuwa wewe ni muongo.

Vinginevyo, kama wewe si muongo, kanusha hiyo kauli kwamba wewe ni muongo kwa ushahidi.

Mpaka sasa muandishi wa Mwananchi anaonekana ni muongo tu.

Kama si muongo, akanushe kaui ya polisi.
 
Watuhumiwa tayari wameshafikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka. Tusubirie uamuzi wa mahakama
Uamuzi wa mahakama utahukumu kama watuhumiwa wana hatia au hawana hatia.

Hapa kuna jambo lingine tofauti kama muandishi wa Mwananchi aliandika habari za uongo ama la kwamba RPC kasema binti alikuwa anajiuza.

Credibility ya Mwananchi imewekwa kwenye mahakama ya public opinion, na Mwananchi hawajajibu tuhuma za Polisi.
 
Naam,

Na rekodi mpaka sasa inaonesha polisi wamewaita Mwananchi waongo, Mwananchi hawajajibu.

Ukiitwa muongo, usipojibu, unaonekana umekubali kuwa wewe ni muongo.

Vinginevyo, kama wewe si muongo, kanusha hiyo kauli kwamba wewe ni muongo kwa ushahidi.

Mpaka sasa muandishi wa Mwananchi anaonekana ni muongo tu.

Kama si muongo, akanushe kaui ya polisi.
Ukisoma taarifa ya Polisi, nasema wanaomba radhi kwa hiyo kauli na hapo hapo wanachunguza kupata usahihi wa hiyo kauli. Mpaka hapa hushangazwi tu na hii taarifa ya Polisi?

Yaani unaomba radhi kwa kauli ambayo bado hujaithibitisha?

Yaani Polisi wanakubali tuhuma ambazo wao wenyewe bado hawajajiridhisha nazo?

Kama uko sahihi, basi nilitarajia Polisi wangeseme RPC huyo anaondolewa kupisha uchunguzi lakini sio kuomba radhi kwa kauli ambayo bado wanatafuta usahihi wake.

Wameomba radhi kwasbabu wanajua ukweli wote , vinginenyo wasingeomba radhi.
 
Simtetei RPC. Kwanza mimi nina bias against Tanzanian police, sasa nitamtetea vipi polisi wakati mini bias yangu ni against the police?

Nimewalaumu pokisi hapo juu kwa kusema kesi ya mtu akiywchoma moto picha ya Samia inefikishwa mahakamani mara moja, hii wanaichelewesha, kwa nini? Sasa hapo namtetea vipi RPC?

Nimeweka communique ya msemaji wa polisi na link ya audio ya RPC.

Wote wanasema RPC hakusema binti alikuwa anajiuza.

Wanasema RPC aliulizwa kama binti alikuwa anajiuza.

RPC akajibu kuwa, hata kama binti alikuwa anajiuza, hakustahili kufanyiwa alivyofanyiwa.

Muandishi wa habari akaandika kuwa RPC kasema binti alikuwa anajiuza.

Sasa, kama kweli mahojiano yalikuwa hivyo, huoni kuwa huyo muandishi wa habari ni mzushi aliandika nukuu ya nje ya muktadha ili kuuza magazeti yaje tu?

Tutamuamini vipi muandishi kama huyo?

Hapo nimemtetea vipi RPC?

Kwa nini mnataka kuifanya hii habari iwe simple story ya "Us against them"?

Kwani haiwezekani ikawa pilisi wana makosa mengi, kama nilivyisema hapo juu, kwa mfano, wamechelewesha kuifikisha kesi mahakamani, halafu pia, kuna waandishi wa habari washenzi, wanataka kupindisha maneno ili kuuza magazeti yao wakati kuna mtu kabakwa?

Haiwezekani mawili yote yakawa kweli?

Where does this false dichotomy come from?
Nakuhakikoshia kama muandishi angekuwa kapotosha haya yangetokea.
1. Gazeti lingeamrishwa na polisi liombe radhi
2. Huyo afande asingetolewa kwenye cheo chake
 
Kama wapo makini hivyo, waweke audio ya mazungumzo ya muandishi wao na RPC tusikie wenyewe kilichosemwa na tujue kama polisi wana spin. Au watoe hata kauli ya kupinga maneno ya polisi.

Mpaka sasa Polisi wamesema Mwananchi wameandika habari za uongo, lakini Mwananchi hawajajibu wala kukanusha kauli hiyo ya polisi.

Huo si umakini.

Wameharibiwa credibility, kitu ambacho ni muhimu sana kwa chombo cha habari.

Sasa chombo cha habari kilichoharibiwa credibility na kukaa kimya tu utakiitaje makini?
Kama mwananchi ni waongo kwanini RPC katolewa kwenye hicho cheo?
 
Ukisoma taarifa ya Polisi, nasema wanaomba radhi kwa hiyo kauli na hapo hapo wanachunguza kupata usahihi wa hiyo kauli. Mpaka hapa hushangazwi tu na hii taarifa ya Polisi?

Yaani unaomba radhi kwa kauli ambayo bado hujaithibitisha?
Kuomba radhi kwa hiyo kauli si issue, inawezekana kabisa kwa Jeshi la Polisi kuomba radhi kwa wananchi kupata kauli hiyo iliyotokana na mahojiano ya muandishi wa Mwananchi na polisi hata kama kauli hiyo iliyotolewa na muandishi wa Mwananchi ni potofu.

Yani, hata kama muandishi kapindisha habari baada ya mahojiano na RPC, inawezekana Jeshi la Polisi likawa na kitu cha kuomba radhi pia, kwa mfano, kwa jeshi la polisi kutotoa audio ya mahojiano kati ya muandishi na RPC hata kabla ya muandishi kuandika alichoandika kwa upotofu, inawezekana jeshi la polisi lina kitu cha kuomba radhi kwa kuwa limesababisha taarifa potofu zitamalaki katika jamii.

Hapo kwenye ufuatiliaji unaofanyika ili kupata usahihi wake ndiyo pana utata mkubwa zaidi, lakini mimi naona inawezekana wakawa wanataka kumaanisha kuwa wao wametoa upande wao wa polisi lakini pia wanafuatilia upande w amuandishi kama ana kingine cha zaidi ya walichotoa upande wao polisi.

Pia, inaweza kuwa ni lugha ya kipolisi ya kujiachia escape route tu mambo yakichukua njia tofauti waseme "tulisema bado tunafanya uchunguzi zaidi".
 
Tundu
kabisa, kila mtu anamajukumu yake, kukosoa na kulaani hiyo ni kazi ya tundulissu na watu wake. ila jamaa mtata huwa analaani kwenye ulaji

Tundu wachaga wamemzidi akili kwenye ulaji.
 
Nakuhakikoshia kama muandishi angekuwa kapotosha haya yangetokea.
1. Gazeti lingeamrishwa na polisi liombe radhi
2. Huyo afande asingetolewa kwenye cheo chake
Kama muandishi hajapotosha, halafu kasingiziwa kupotosha, na kakaa kimya, ana tatizo kubwa tu bado.

Muandishi anayetakiwa kuipigania jamii ipate ukweli ameshindwa hata kujipigania yeye mwenyewe rekodi yake ibakie kuwa safi.

Kasingiziwa kupotosha, kashindwa kujitetea.

Ataweza kumtetea mtu baki anayesingiziwa kupotosha?

Vyovyote utakavyoliangalia suala hili, muandishi bila kujibu anakuwa kaharibu tu.
 
Kama mwananchi ni waongo kwanini RPC katolewa kwenye hicho cheo?
Hapa unaunganisha mambo mawili ambayo si lazima yawe na uhusiano, logical fallacy ya non sequitur.

Yani unajenga hoja kuwa ikiwa RPC kakosea, basi Mwananchi lazima wawe wakweli.

Wakati inawezekana RPC kakosea mambo mengine huko, kachelewesha kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, lakini hilo halina uhusiano wowote na kauli ya muandishi wa Mwananchi kuwa RPC kasema binti alikuwa anajiuza.

Ni hivi, inawezekana RPC kakosea kuchelewesha kumaliza uchunguzi, au inawezekana polisi wameona RPC huyu kashajijengea jina baya na jamii tu, tumtoe hapa kwa sababu haaminiki, hata bila kukosea.

Au, inawezekana RPC hakusema binti anajiuza, lakini RPC hakujieleza vizuri sana kiasi akaacha mwanya wa kutafsiriwa vibaya na muandishi, hivyo hata kama hajasema binti anajiuza, alitakiwa kuwa muangalifu zaidi na maneno yake anavyoyasema ili asiache mwanya w akutafsiriwa vibaya.

Na wakati huo huo, muandishi wa Mwananchi akawa kaweka nukuu vibaya kwa makusudi ili kuuza magazeti.

Hakuna fact yoyote inayolazimisha kuwa RPC akitolewa hapo tu basi ni lazima itakuwa kwa sababu muandishi wa Mwananchi kasema ukweli kwenye habari ya RPC kusema binti alikuwa anajiuza.

UPDATE.

Habari za hivi punde ni kwamba RPC alikuwa kashapangiwa uhamisho tangu kabla ya issue hii, polisi wametekeleza tu hilo na watu wanaona sababu ni hii issue.
 
Baada ya RPC wa Dodoma kutoa kauli inayoonekana kuhalalisha kitendo cha binti kubakwa, watu wengi wakiwemo wanasiasa na wanaharakati, wamelaani kauli ile na kutaka RPC awajibishwe.

Hata kuondolewa kwa huyu RPC bila shaka ni matokeo ya watu waliopoza sauti na si vinginenyo.

Swali ni je, kuna kiongozi hata mmoja wa CCM aliejitokeza hadharani na kulaani hiyo kauli?

Inashangaza sana hata Raisi wa nchi japo ni mwanamke, sijui kama amewahi kutoa kauli yoyote kuhusu hili tukio walau kufariji umma wa watanzania kuhusiana na hili tukio.

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Kwani unafahamu tu maana ya ccm.Ninavyojua ni chukua chako mapema.Je kama ndivyo vipi wahangaike na yasio na manufaa ya moja kwa moko kwao?
 
Namsikiliza mtu hapa anasema RPC kasema binti alikuwa anajiuza.

Yani watu hawawezi kufuatilia habari kabisa.

Halafu wanajadili mambo kwa emotions badala ya facts.
 
Back
Top Bottom