Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Ukifa hawakuziki. Hapo ndipo wametushika pabaya
Hizo ndizo bhangi za madhehebu tunazovutishwa waumini.

Kwani wasipokuzika wao, jamii imekwenda wapi?

Kitendo cha kusitiriwa kaburini hakichukui hata zaidi ya nusu saa na baada ya hapo hakuna alama inayobaki kaburini kwamba huyu marehemu kazikwa kwa mtindo gani.
 
Nadhani pia hii inatokana na kuwa hatujawekewa vikwazo au kulazimishwa kutoa ndio mana tunakuwa wagumu.
Kiukweli upande wetu kwenye suala la kutoa ni changamoto.
Hata hawa wanaolalamika kama wangekuwa hawajabanwa wasingekuwa wanatoa ila ni kwasababu tu wamewekewa utaratibu wanajikuta ni lazima watoe
 
Hii kali
Toeni bwana muwafanyie wepesi wapendwa wenu huko kaburinj
 
Well said mkuu.
 
Ningependa kujua ni jimbo gani.

Nimekaa jimbo la Morogoro,jimbo la moshi, jimbo la Arusha na jimbo la dar es laam sijawahi kusikia huo mchango wa ada ya kua kikatoliki.
Ingawa kila jimbo lina utaratibu wake.
 
Maana ake iyo tuiite Ni tozo ya ukatoriki[emoji28]
 
Makanisa sasaivi yamekumbwa na pepo la fedha zamani kidogo katoliki ilikua nzur sana lakini walipoingia ma padre weusi ndipo dhahama ilipoingia kanisani,,siku za mwisho hizi shetani anajiinua kupita kiasi lengo lake kuu ni kuharibu kabisa amani ya kanisa,,sote tunafahamu madhara ya pesa katika dini hivo nae anapenyeza wajumbe wake kuharibu kanisa.usivunjwe moyo na michango we toa ulichobarikiwa asante.
 
Ukiona huko Katoliki na Lutheran sadaka zinakutisha na kukuchosha basi jaribu makanisa ya Pentekoste ndio utakiona cha mtema kuni.

Huko Pentekoste utatakiwa kutoa
1. 10% ya kipato chako chochote (kama una mshahara wa 1m kwa mwezi, basi kila mwezi laki moja lazima pastor aikunje mfukoni, na pastor atataka kuona mpaka salary slip)

2. Kuna sadaka za shukrani kila unapofanikiwa jambo lolote (na hii inapaswa kuwa sadaka nono fulani)

3. Kuna sadaka ya kusindikizia maombi yako kila unaposaka kuombewa mambo yako. (Hapo utapigwa mikwara kibao)

4. Kuna sadaka ya kuchangia shughuli mbali za kanisa (kuanzia ujenzi, vyombo vya muziki, uinjilisti, suti ya mchungaji, gauni la mama mchungaji nk)
 
Point[emoji106]
Wakikujibu nitag
 
Ha ha ha.....
Yaan Usipolipa utaonekana si mkristo[emoji28]
 
Lakini kuna sinodi ya maaskofu inayoendelea hio ilitoa nafasi kwa waumini kutoa dukuduku lao, mawazo yao, maoni yao na vile wanavyoliona kanisa leo na kesho.

Kwa vile ndugu mleta mada umekiri sio mhudhiriaji wa kanisani na jumuiyani hio nafasi imekupita.


Hata hivyo mapinga vikali michango mikubwa na isio mikubwa ilio mingi ndani ya parokia zetu, haswa kukukiwa na ujenzi wa kanisa, hapo panakua ni chanzo cha mapato na fursa kwa baadhi ya wengi.
 
Ha ha ha.....
Maana ake iyo sadaka kubwa ndo inwatuliza uko kaburini au?[emoji28]
 
[emoji3][emoji3][emoji3] nyumba ya kufikia bikira maria! Huo wizi wa mchana kweupe kabisa.
Alafu ukute paroko na prado lake anakuja kung'oa wake zenu na mabinti zenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…