Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Ninapohudhuria misa za maziko kwa dhebu la mtoa mada napata hasira. Ati baada ya kuaga mwili wanaweka kikapu cha sadaka ya kumuombea marehemu (hii kiongozi aliyeendesha misa anaondoka nayo), kisha kinakuja kikapu cha rambirambi.
 
imetabiliwa watu watapenda pesa kuliko kitu chochote
 
Usisahau kanisani muhimu kuliko yote huwa tunafuata neno, sasa haiwezekani injili ihubiriwe dakika 20 halafu misa itumie masaa karibu matatu kuendesha harambee ndani ya kanisa.

Wewe hata kama ni mwislamu jaribu kusikiliza hotuba za mapadre wa kikatoliki halafu msikilize mtu kama Mwamposa hotuba yake utajuwa hapa naongea nini, wanaokwenda kwa Mwamposa wanashiba neno na ndio kitu muhimu zaidi.

Sasa ibada ya misa kipaumbele cha muda mwingi kikiwa ni sadaka mbalimbali na harambee mbalimbali kwangu ni useless ni bora hata nikikaa nyumbani nitune channel ya Arise and shine Mwampisa atanibariki sana kwa neno na anatowa hotuba kwa muda mrefu mpaka unashiba neno.
 
Chief mbona vitamu vipo vingi sana na vinaruhusiwa ndani ya dini ya kiislamu....unaweza ku giveup kitimoto na still uko fine tu! Karibu kwenye uislamu

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hapo kwakweli hawajafanya vizuri.
Kwa kipindi hiki walitakiwa wao ndio wamsaidie hasa ukizingatia alikuwa muumini mzuri.
Wakati mwingine watu huvunjika moyo kwasababu ya mambo kama haya na kuwafanya kushuka kiimani au kuamua kubaki bila dini kabisa.
 
Kweli michango imezid na inakera. Unatoa sadaka kabla hata kanisani hujafika na kabla hujashiriki mtiririko mwingine wa ibada.
Japo siwez hama kwa hizo sababu lakin inabid warekebishe mahali wanatukwaza waumini.
Huku uchaggani picha linaanza kwanza Padri anaheshimika Kama mungu.

Yaani mtu anaweza kuitwa kwenda kea Mtendaji wa Kijiji au Police aisende lakini akiitwa kwa Padre. Kwanza anapata hofu kubwa kuwa tatizo ni nini🤣

Na ukifiwa Padre akija ile sadaka ya ibada ya mazishi anabeba anaondoka nayo. Na kwako ni masikini hata ibada ya mazishi hamalizi, anafanya nusu akimaliza naaepa anawaachia waumini waendelee.

Ila binafsi naona utamaduni wa uchaggani ndio umepelekea tatizo kuwa kubwa sana. Maana huku ukipata MSIBA usitegemee kabisa ushirikiano kutoka kwa watu.

Hata Kulia Wala maombolezo Wala huzuni. Kwahiyo kinachofanyika ukipata MSIBA, inabidi uwe na pesa ukodi VITI, MAHEMA, POMBE, NYAMA na MUZIKI.

Muziki ndio utaomboleza pamoja na watu wa kukodiwa ( TARUMBETA).

Bila kufanya hivi Hakuna mtu atajua kwako Kuna msiba. Na kibaya zaidi na kanisani ukiwa umetengwa, utazikwa Kama mzoga was mbwa Koko.

Hii ndio hali HALISI.
 
Kama hauamini kwamba utapata ufalme wa Mungu kanisani basi taka sana kuzifahamu kazi za roho mtakatifu. Yesu Kristu Katika mafundisho yake neno kanisa alilitaja mara moja tuu Rejea
Mathayo 16:13-17
Na wakati anaondoka aliwaachiwa mitume kazi ya kufundisha juu ya ufalme wa Mungu kwa msaada wa roho mtakatifu.

Mtakatifu Paulo ndio mwalimu wa mwanzo wa kanisa na mifumo mingi imeasisiwa nayeye jitahidi kumsoma kwa kina na uelewe hoja ya kwanini imempasa kasisi kuishi useja. Ukristo ni kazi tena ni nguvu jibidiishe kujifunza ili kujenga Imani yako juu ya mwamba imara
 
Ninapohudhuria misa za maziko kwa dhebu la mtoa mada napata hasira. Ati baada ya kuaga mwili wanaweka kikapu cha sadaka ya kumuombea marehemu (hii kiongozi aliyeendesha misa anaondoka nayo), kisha kinakuja kikapu cha rambirambi.

Hapo kumleta padri kuja kuombea marehemu unatozwa pesa. Akifika lile kapu pale wanaondoka nalo la kwenda parokiani mambo ya ajabu sana.

Niliwai udhuria msiba wa msabato mmoja. Ile watu wamemaliza kutoa yule mchungaji akachukua pesa akampa mume alifiwa mke. Itamsaidia mbele ya safari na dharura atakapokua ana mpumzisha mkewe.

Nilijutia sana kwa nini sikunyanyuka kutoa sadaka. Ila nipendezwa na jambo lile.

Ukatoliki wetu ni changamoto
 
[emoji23][emoji23] haya masihala sasa mtani. Kiingiacho halimtii mtu najisi bali kitokacho
 
Hizo huduma za kiroho ni ngumu tatizo sisi tunaenda kanisani na mitizamo ya kibinadamu/kipagani. Huyu Mungu tunayemtafute/tuitafute kweli mioyoni mwetu na tuijue. Huduma za kiroho ni gharama hakuna cha bure isipokuwa kusali tu unapokuwa wewe mwenyewe.
 
Hahah, mzee baba siku hizi nasikia kuna kanisa linaitwa sijui Free Church la yule jamaa wa Ze Comedy, ukitaka kusali unaibuka tu hakuna sadaka za mafungu mafungu...
Alizisoma nyakati akabaini taabu na kero za machangizo
 
[emoji851][emoji851][emoji851][emoji851]
 
Usipotoa ni Bora hata kanisani usiende kwasababu huduma za kanisa hutapewa.

Hata kuzikwa Padre anaweza asije
Uzuri padri hashiko septu wala jembe wala habebi jeneza na mfu hayatambui yanayojiri. Sasa sijui hofu i wapi?

Okonkwo atabaki kuwa shujaa wangu japo ni fixious myth!
 
Uzuri padri hashiko septu wala jembe wala habebi jeneza na mfu hayatambui yanayojiri. Sasa sijui hofu i wapi?

Okonkwo atabaki kuwa shujaa wangu japo ni fixious myth!
Padre hashiki Jembe lakini ana uwezo wa kuwaambia watu wasishike wakakubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…