Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Huyo ni mkatoliki kabisa na asemacho ni kweli bila chenga. Hata mm ni mkatoliki naunga mkono home yake. Katoliki ukusanyaji wake wa fedha hata hao TRA wakasome.

Ili wakuhesabu unafaa huduma zao, lazma wajue kama unasali jumuia. Na huko jumuia ndio kuna michango na mikusanyo ya fedha isiyo mithilika. Kwa nyongeza tu, hata shule za katoliki bei ipo juu kama za watu binafsi, na zina michango na mahitaji ya malipo ya ajabu sana. Hata Mia ikipungua wanamtimua mtoto. Kwanza kuzipata tu hizo shule kwa mzazi alieshiriki michango ya ujenzi ni shida, hata kama mtoto ana vigezo.

Mleta mada kaeleza vyema sana, kuwa kama vyanzo vya mapato kama kumbi Mashule mahospitali frame za maduka vimejengwa kulisaidia Kanisa, sasa kuna haja gani ya kukakamua namna ya uporaji waumini walioshiriki ujenzi wake kwa fedha zao?

Hakuna mahali imeandikwa kwny biblia kuwa Utaenda mbinguni kwa kutoa sadaka au hutoenda kwakua hutoi sadaka. Unadhania Yesu alipo mwambie yule jamaa kauze ulivyonavyo uwape masikini kisha unifuate, angekuwa hawa mapadiri au wachungaji wa sasa, angesemaje kama sio kusema kauze ulivyonavyo kisha uvilete hapa ndio unifuate.
Ahsante kiongozi wangu umeeleza vyema kabisa itoshe sasa kuukubali ukweli Roman Catholic are satanic believers
 
Ukishaingia mfumo wa jumuia lazima utowe pesa ya kuwa mkatoliki kila mwezi.

Pili harambee za kipuuzi na sadaka nyingi kwenye ibada inaondoa system ya kikatoliki ambayo tulizoea ibada ya misa ya jumapili ni lisaa limoja na nusu tu na ikizidi kwa special case ni masaa mawili tu, sasa kwa huu upumbavu ulioanza ibada inakwenda mpaka masaa matatu, misa ya kwanza mnaingia saa 12 asubuhi mnatoka saa mbili na kitu.
Si uache kwenda wewe unaenda kufanya nini?

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Toa ndugu toa ndugu..ulichonacho..halafu unataka usitoe hilo kanisa litapelekaje injili..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje wahudumu..unataka usitoe hilo kanisa litalipaje bills tofauti kama umeme na maji...unataka usitoe hilo kanisa litafanyeje logistics mbali mbali...unataka usitoe maintaince na repairs ya vifaa na miundombinu mbalimbali utatoa wewe.??

Acha kulalamika sana kama huna hela kaa kutulia

Uzuri hujalazimishwa..ila mkristo wa kweli hawezi kuona kama ni wizi mana hayo ndio mahitaji muhimu ya kuendesha taasisi.

Kingine kutoa ni upendo..kiwango itachojaliwa kutoa kinatosha sana.

Kama unaona hufiti nenda huko ambako hawatoi sadaka..hakuna aliyekushikiria unabaki kanisani.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote.

#MaendeleoHayanaChama
Ameen

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Nilijuwa watetezi hamuwezi kukosekana, hebu nieleze tu miradi ya kanisa katoliki ina faida gani kwa kanisa? Na ile benki yetu ya Mkombozi inalifaidisha vipi kanisa?

Kwani huko nyuma tuliweza vipi kujenga makanisa na mashule kwa sadaka za kawaida bila huu uharamia mpya ulioingia? Ni nini kilichobadirika?

Sisi parokia yetu ilikuwa na vigango vitatu na vyote vimekuwa parokia sasa zenye makanisa makubwa tu, tuliwezaje hayo kwa mwendo wa kawaida bila watu kunung'unika na leo kimebadirika nini?
Kikubwa hapo huna unachoweza kuwabadilisha wakatoliki hapo ni wewe kubadilika tu acha kuhudhuria kanisani na ikikupendeza silimu kabisa kuna ndugu yangu ameselimu sasa hivi ni muislamu ni mwaka wa 3 sasa na maisha yanasonga mbele kama kawaida.
Ukiwepo watatoa sadaka usipokuwepo watatoa sadaka maradufu hakuna tofauti cha msingi ni wewe kubadilika tu ufuate direction yako

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Roman Catholic Church lina changamoto za kiuchumi dunia nzima:

1. Kupungua kwa Waumini/Wachangiaji kindakindaki hususan Ulaya

2. Kuongezeka kwa kesi/matukio ya unyanyasaji wa kingono uliofanywa na Makasisi/Viongozi ktk miongo hii mitatu imeigharimu kwa kiasi kikubwa Kanisa kifedha

3. Kushuka ushawishi wa Kanisa Serikalini (special case in Tz) Miaka ya 2000 kurudi nyuma RC walikuwa na mkono wa juu ktk miradi mingi iliyokuwa ikishirikiana na Serikali ya Tz ukilinganisha na sasa
Viongozi wa RC walikuwa na ulwa mkubwa Serikalini, ndio taasisi iliyo ikiongoza kwa tax exemption

Nakumbuka ktk miaka hiyo ukienda pale TEC Kurasini mnakutana hata taasisi 4 tofauti za Serikali na SU semina zinafanyika pale + accommodation + meals

4. Kuongezeka kwa ushindani toka Makanisa mengine

5. Kuongezeka kwa UELEWA/KUJIELEWA kwa Waumini. Miaka ya zamani ilikuwa ni aghlabu kukuta Muumini wa RC akifunguka kama mtoa uzi alivyofunguka
Ilifikia stage baadhi ya maeneo vijijini Waumini wa RC watu wazima walikuwa wanapanga foleni kuchapwa viboko kwa sababu ya kutotimiza baadhi ya amri za Kanisa, hapa Tz tuna incidences zaidi ya 2 ambazo zili trend miaka ya hivi karibuni

Wakatabahu
 
Siyo lazima utoe sadaka ya cash. Nimeona waumini wengine wanaleta katoni 2-3 za maji ya Hill, miche ya sabuni ya kufulia, juisi, hata kuku mzima, etc. Lakini hii ni trend mpya kwa Wakatoliki. Wameiga kutoka Walutheri.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mtu aliyeanza kwenda kanisani jana utamjua
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
Mkuu Matola unadhani watu huwa wanaanzisha "dini" ili mwende pale kuzurura kisha kutoka tu hivi hivi?. Waasisi wa dini ni miongoni mwa Super intelligent people,wanaanzisha dini na wanakuwa na mikakati endelevu ya kuwafunga(kuwapumbaza) waumini kwenye hizo dini ili wawe watumwa wao milele.

Imagine mtu anazaliwa tu anakutana na ubatizo,kakua kua kidogo anakutana na sijui kumnyo na vipaimara,hajakaa sawa kafungishwa ndoa na mahabuba wake hapo hapo,kafa kazikwa na dini hiyo hiyo. Yaani mtu anashikiliwa tangu kuzaliwa hadi kufa kwake yeye na kizazi chake. Kunasuka hapo ni mpaka Neema ya Mungu katika Kristo Yesu iingilie kati.
 
Hizo fedha wanapelekaga wapi ukizingatia jamaa wanasema hawaruhusuwi kuoa na wenzao hawaruhusiwi kuolewa?
Hivi wanakatwaga VAT kweli? nina miaka 3 sijasali kanisa katholiki ndiyo kanisa langu ....

na nikidanchi wasipo nizika kwa ibada waniache hapohapo niwanukie
 
Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?
Wala usiteseke kwa kuandika uharo wako huu usio na ukweli hata kidogo, hama wewe, mkeo na vitoto vyako nenda kwa mwamposa, gwajima, kakobe kakanyage, mafuta, chumvi namaji kwa sana na michango yote ya kule ambayo ni mara 50 ya Roman au Kkkt katoe huko. usituchoshe! RC tupo hapa tulipo kutokana na michango yetu!
 
Pilipili kichaa haiwezi kuniwasha mimi, nyani haoni kundule, unauona utapeli wa kina Mwamposa ila utapeli unaofanywa na kanisa lako unafumba macho, huu ni unafki.
 
Roman Catholic Church lina changamoto za kiuchumi dunia nzima:

1. Kupungua kwa Waumini/Wachangiaji kindakindaki hususan Ulaya

2. Kuongezeka kwa kesi/matukio ya unyanyasaji wa kingono uliofanywa na Makasisi/Viongozi ktk miongo hii mitatu imeigharimu kwa kiasi kikubwa Kanisa kifedha

3. Kushuka ushawishi wa Kanisa Serikalini (special case in Tz) Miaka ya 2000 kurudi nyuma RC walikuwa na mkono wa juu ktk miradi mingi iliyokuwa ikishirikiana na Serikali ya Tz ukilinganisha na sasa
Viongozi wa RC walikuwa na ulwa mkubwa Serikalini, ndio taasisi iliyo ikiongoza kwa tax exemption

Nakumbuka ktk miaka hiyo ukienda pale TEC Kurasini mnakutana hata taasisi 4 tofauti za Serikali na SU semina zinafanyika pale + accommodation + meals

4. Kuongezeka kwa ushindani toka Makanisa mengine

5. Kuongezeka kwa UELEWA/KUJIELEWA kwa Waumini. Miaka ya zamani ilikuwa ni aghlabu kukuta Muumini wa RC akifunguka kama mtoa uzi alivyofunguka
Ilifikia stage baadhi ya maeneo vijijini Waumini wa RC watu wazima walikuwa wanapanga foleni kuchapwa viboko kwa sababu ya kutotimiza baadhi ya amri za Kanisa, hapa Tz tuna incidences zaidi ya 2 ambazo zili trend miaka ya hivi karibuni

Wakatabahu
Umedadavuwa vyema na ni kweli unalijuwa kanisa letu vizuri.

Sasa swali ni kwamba hiyo miradi yote inasaidia vipi kanisa ikiwa matumizi karibu yote ya kanisa wanacover waumini?
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
unataka wazungu wakabane wakuleteeni
 
Hivi wanakatwaga VAT kweli? nina miaka 3 sijasali kanisa katholiki ndiyo kanisa langu ....

na nikidanchi wasipo nizika kwa ibada waniache hapohapo niwanukie
hhhhhhhhh ukiwanukia ata manispaa watakuzika
 
Yaani ili swala nilijua mimi peke yangu
kuna siku nilikua naongea na brother mmoja wa katoliki na yeye alikili michango imekua mingi alafu najiuliza hivi biashara zao kama shule na hospital hayatoshi kujiendesha manake tunachangishwa hadi mchango wa gari la padri
 
Mnataka kanisa liendelee na kuwa na vitu vya kisasa kama magari nk hivyo vitu vitatoka wapi?

Kanisa katoliki walizoesha waamini wao kuishi kwa kubebwa na misaada toka kwa wazungu bila kuwafunza wenyewe kujitegemea.
Sasa hivi mkiambiwa mtoe fungu la kumi ni shida wakati biblia inawataka hivyo.
Acheni kulalamika hivi mnajua hao mapadri na masista nao wanataka kuishi maisha mazuri kama ninyi waamini.
Au kwa kuwa wao hawana watoto mnadhani hawana mioyo ya kutamani?
Toeni sadaka nyingi ili mbarikiwe acheni ubahiri usio na maana.
 
Nadhani mtoa mada bado uko enzi za wafadhili wa kanisa. Kwasasa kanisa linajiendesha,kama ufadhili unapatikana kwa bahati sana. Hivyo usipotoa unasababisha anguko la kanisa. Tutoe,tujenge vyakwetu. Wakati wakufanyiwa haupo tena.
Kutoa siyo jambo baya sema kitu watu tunachokataa ni namna wanavyo endesha ibada yani makanisa kwasasa yamekuwa kama SACOS
kila vikao mnavyo kaa ni vyakutoa tu .... minada inayoendelea niyakipigaji kuliko kawaida neno la MUNGU tunapatq kwa kiwango kidgo sana nako wanasisitiza kutoa ....MUNGU aturehemu kwakweli
 
Back
Top Bottom