Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Huyo anawapotezea muda ndugu, hana ukatoliki . Mimi nilivyosomaga thread yake moja kwa moja niligundua ni mtu wa imani ipi, japo hapa katika uwasilishaji wake amejivika sura ya ukatoliki.
 
Huyo anawapotezea muda ndugu, hana ukatoliki . Mimi nilivyosomaga thread yake moja kwa moja niligundua ni mtu wa imani ipi, japo hapa katika uwasilishaji wake amejivika sura ya ukatoliki.
Inawezekana ikawa kweli si mkatoliki lakini mbona wakatoliki wengi humu wanaunga mkono hiyo hoja kuna upigaji kweli makanisani tungestiki na mada nadhani
 
Hujui waroma ww kama hutoi na ww huduma hupewi
Hili sikulijuwa ndio leo nasikia kwa hapa wanakosea sana maana sio kila mtu anatafuta huduma za kiroho ana uwezo mimi muislamu tuna changamoto kama hizo ila sisi sio lazima unacho unatoa huna unakausha tu sio issue na ibada unafanya tu hakuna wa kukuingilia na msiba ukikupata utahudumiwa kama anayetoa na asiyetoa, labda ukitaka huduma specific kwa shekh utampa kitu kidogo japo hakuna kiwango. Ila hili la leo kuwa ukiwa hutoi basi unatengwa hapa ndugu zangu jifikirieni kidogo maana watu hawako sawa.
 
Waroma wanakosea bigtime..,.....
hela mbele
 
Tatizo sisi waislamu mashekh watu wapigaji kuna msikiti mmoja kuna mtu kajitolea kutaka kumalizia ujenzi hawataki wanataka wapewe pesa wao jamaa akajivuta. Wenzetu pamoja na haya ambayo siungi mkono kumtenga mtu kwenye msiba au harusi lakini wanaendeleza walichonacho kama mashule na makanisa sisi mpaka shule zetu tunaziuwa.
 
Ukishajua nguzo ya iman yako ni nini basi hugombani na mtu
 
Kanisa Katoliki zamani lilikua linaendeshwa na Misaada Toka Ulaya .
Kule Ulaya Kuna watu walikua wanatoa Sadaka zao zije kuwahudumia maaskofu,mapadri, masisita na watumishi wengine Parokoani ili wewe huku usitoe Sadaka nyingi lakini Sasa hali imebadilika. Ulaya hawaendi sana makanisani hasa Vijana na matajiri Kwa hiyo Ile misaada imepungua sana. Hakuna namna ya kuendesha kanisa zaidi ya waumini wenyewe.

Na umshukuru Mungu mana maparokia Mengi yalijengwa na wakoloni wenyewe wakati huo waafrika hawana uwezo wa kifedha. Maparokia Mengi na majumba ya kifahari wanayoishi mabrother na masister yalijengwa na waumini waliokua wanachangishwa Huko Ulaya na kuja kama Misaada. Hata Vatikani Iko siku itaanguka na kubaki ikijiendesha yenyewe mana nayo inategemea Kodi za nchi mbalimbali Duniani zinazopelekwa pale kama kanchi Kenye balozi mbali mbali Duniani wakati zile ni ofisi za kidini na sio serikali Wala nchi. Ni ujanja ujanja ulifanywa na Tawala za kirumi kulinda Mila zao na Dola lao Kwa mgongo wa dini.

Hata Kwa waislam Kuna watu wanaotoa Sadaka zao Huko Uarabuni na zinajenga misikiti kila mahali lakini wale wanaotoa hawalalamiki.

Tatizo ninaloliona Kwa Makanisa yote ni ubinafsi wa kila parokia au Dayosisi au usharika au kanisa Fulani binafsi.
Wangekua wanasaidiana Kwa mahitaji basi kila kitu kingekua sawa.

Kanisa katoliki na Lutherani Kwa mfano yana miradi mingi sana lakini haieleweke kuwa zinamufaisha nani hasa.Je, Kuna waumini maskini wanaonufaika au Bado michango inahamasishwa hata pale ambapo miradi ingegharamikia .? Hapo
 
Aisee nimechekaaa sana daa eti unadondosha jiti tu. Mkuu kuna vyombo vya sadaka ukiweka sarafu vinapiga kelele balaa.
 
Tukienda kwenye historia ya kanisa katoliki ndio unaweza usiende tena kanisani, tusifike huko naelewa kuliko unavyoelewa wewe.
Yeah nenda ukaisome tena, ukimaliza tafuta tena encyclopedia of religion soma kuhusu dini zote unazozijua ulimwenguni mambo kama haya hayatakupa mshangao.

Nadiriki kusema hakuna unachoelewa kuhusu dini.
 
Inawezekana ikawa kweli si mkatoliki lakini mbona wakatoliki wengi humu wanaunga mkono hiyo hoja kuna upigaji kweli makanisani tungestiki na mada nadhani
Hakuna upigaji hapo, ndiyo maana nikasema ukiwa muumini wa dhehebu fulani, jaribu kujifunza historia& utamaduni wa dini husika. Mtu unaabudu hujuhi hata history & culture of your religion ndiyo maana unakuta mtu anayumbishwa imani kwa jambo dogo sana.
 
Wewe ni paroko wa kanisa lipi?
 
kuanzia jumapili ijayo natoa sadaka moja tu nitakuwa na uchuna wa mbuzi kimyaaaa kama sio mimi
 
Tatizo hilli lipo kweli kwa makanisa mengi ya Kikristo ila kwa sisi KKKT michango yote kanisani siyo LAZIMA na hakuna adhabu kwa ambaye hatatoa hiyo michango ila ni sadaka moja tu ambayo ni lazima utoe ili uhesabike upo active na kanisa, sadaka ya ahadi ambayo inakuwa na bahasha yake na hata kama hujaenda kanisani unakuta unampa mtu akupelekee kwenye bahasha yako,
kimsingi Sadaka ni mbili tu kwa sisi KKKT (sadaka ya ahadi na shukrani ya wiki ) hizi hutolewa kila ibada ya jpili ,sadaka nyinginezo ni optional (kama fungu la kumi,shukrani ya pekee,mavuno nk )ambazo kimsingi kama Mkristo kweli hizi siyo sadaka za kudoubt.kama Mkristo mwenzako nakushauri mkuu acha kulalamika lakini toa michango pale unapoona inafaa kutoa na uwezo wa kutoa unao,
All in all viongozi wajitafakari sana kwa maana maswali ni mengi kuliko majibu kuhusiana na sadaka zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…