Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

This is very sad. Michango imekua Mingi sana makanisani na ukiwa mtoaji ndio unaonekana mkristo kamili.
 
Daaah we jamaaa wewe..umegonga mfupa..lkn sasa huku watu wana moyo wa kutoa...sasa huo moyo wanaubadili maana hari imekuwa tete mnooo. Sasa unatoa sadaka 7 kwa day moja hapo uko na mke nae 7...vijana wa sunday school unao wa4 nao sadaka...walau uwe na 100,000k ya sadaka siku hiyo.
 
Du! huu sasa ndo WIZI... 🤣 🤣
 
Hii nimeipenda maana rambirambi zinaweza kuokoa jahazi. Ni uchuro kwa ndugu waliobaki kuona ndugu yao hakuzikwa na Padre!
Mimi nikifa wakaamua kutonizika ni wao. Roho yangu itakua mahali pengine na harufu itawatesa wao. Siwezi kujinyenyekeza ili wanizike as if wao ndio final say huko peponi
 
Ni wapi uliambiwa uombee WAFU? Au MAITI yako isipoombewa kuna kitu utakosa?
 
Mtoa mada hajasema hana hela ya kutoa au tusitoe sadaka. Hoja ni kuwa Sadaka na Michngo sasa hivi imekuwa mingi mno mpaka inatuchanganya waumini. Kama sisi sasa hv ukifika tu kanisani inabiidi ukachukua bahasha ya zaka..maanake sasa Zaka inalipwa kila jumapili badala ya mwisho wa mwaka au mara moja kwa mwaka, hii ni tofauti na sadaka unayotoa kwenye kikapu. Ukianza hesabu mlolongo wa michango mpaka unajiuliza..Hv mbona huku kazini tunavyolipwa mishahara huwa atuambiwi hii ni ya umeme, hii ni ya chakula, hii ni ya ada, hii ni usafiri, hii ni michango ya harusi? unalipwa mshahara then utachambua mwenyewe kipi ni muhimu katika mahitaji yako..Vivyo hivyo nafikiri Catholics wangefanya hivyo tutoe Sadaka na labda mchango wa pili (ujenzi wa kanisa au kusaidia maskini) wao wakikusanya ndio wakagawe kama hii ni ya tengeneza jimbo, hii ya kupeleka Bethsaida etc. Kingine miradi ya Catholics haisadii au kuwanufaisha walioijenga hao wakatoliki wenyewe. Shule wamejenga kwa michango na sadaka zetu lakini nenda kaulize ada zao? hazina tofauti na za private..basi hata sisi tuliochangia ujenzi wa shule hizo au hosptali tupewe kipaumbele au commission fulani ya unafuu kupata huduma hizo..Nenda Agha Khan hospital uone mhindi anavyopewa kipaumbele akifika pata matibabu kulinganisha na wewe mswahili! Kunahitajika mabadiliko kidogo ndani kanisa kuendana na hali ya maisha ya sasa!
 
Ila wewe ni mbugila.maendeleo hayana vyama,kauli ya kilofa sana hii.na ilitolewa na mnafiki mwandamizi
 
Umeandika kwa muhemuko sana ... Tatizo ni lipi? Kama ni sadaka .. Wewe hujaenda kanisani muda, unaenda kwa kubeep.. Sasa kuna shida gani kama watu wenyewe wanapenda kutoa sadaka? Ingekuwa shida kama unalazimishwa na kama huna labda unafukuzwa au kutolewa nje .

Kama una imani ya kweli hiyo haiwezi kukuzia kwenda kanisani au kuweka jumuisho kuna shida kwenye ukatoliki..Basi ungetafuta kanisa ambalo ni kamilifu uende ukasali huko..Huwezi kupata kanisa kamilifu, ndio maana Kristo ndiye kanisa halisi na yupo kwa watu wanaomtafuta.
Umedai waislam wako sahihi , mbona umefanya kwa ujumla? unawaongelea waislam wapi? Wapo madhehebu tofauti tofauti .. Shia, Suni na ipo misikiti tofauti tofauti na wana taratibu za kuomba au kukusanya sadaka zao.. Je ulitembelea na waislam?

Kama wako vizuri, mbona hujaenda kuungana nao katika imani yao?
Imani ni yako, kanisa ni jukwaa la kuonyesha au kuungana na wengi kufanya kazi ya mwili wa Kristo.. Hata siku moja , hutaweza kupata kanisa la namna hiyo au mtumishi mkamilifu... Ukamilifu upo kwa Kristo peke yake ..... Amani ya Bwana itawale.
 
Hili swala huwa linanifikirisha sana....
 
Unaendaje kanisani na buku 5 mkuu? Wakati baa mnaingia na laki beba kuanzia hamsini ukiona unahoji mambo ya sadaka jua umekufa kiroho toa ulichonacho huna tulia Mungu anakuona matumiz ya sadaka hayatuhusu imarisha uhusiano wako na Mungu kwa kutoa
Mchango ya malofa Huwa kama ulivyoandika .
 
Acha moyo mbaya toa Kama ipo ,mbona kwenye. Baa unatimia hata laki kwa Mambo yasiyo na maana,hata Kama Kuna ujenzi kanisani kwenu haiwezi kuwepo Kila siku,ukitoa Mungu ananibariki,ibada Ni pamoja na kutoa
 
Jiulize hyo elfu kumi yako unatimia shs ngapi,mbona watu wanatoa zaidi y a elfu kumi kwenye ibada moja,?Mtu asiyejua uwepo wa Mungu ndiyo alalamike hiyo
 
Cha msìngi beba mia 7 yani shilingi mia ziwe 7,kuanzia sadaka ya kwanza adi ya 7 unanyanyuka tu na washirìka wanakuona umetoa!
Wala hutaumia,kikubwa Mungu anaona moyo wako!
 
kwani ukifa wasipo kuzika hautaoza??kwani wasio enda kanisani hawafi na kuzikwa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…