Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Kuna kitu hakipo sawa makanisani, ni muda wa wakristo kuamka na kuhoji

Nazungumzia uwepo wa hizo imani za dini na sio mahudhurio ya kanisani, labda ulete takwimu zenye kuonesha kwamba huko ulaya sasa watu wengi hawana dini kama North korea na kwengineko ambako watu hawana dini.

Screenshot_20220412-121501_Chrome.jpg
 
Mchungaji/Padri akitaka gari au nyumba mnamchangia.
Muumini/mshirika ukitaka gari au nyumba unaombewa[emoji3][emoji3][emoji3]

Aliyezileta hizi IQ yake ni ya sayari nyingine kabisa.
 
Hahahaha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu mbona vitu vidogo tu ndugu!
Utatafuta mbadala mfano kuku au mbuzi.
Aisee Ile kitu hatari arafu si haramu kwaiyo siwezi kuwa Islamic wakati nishaitumia😂😂😂
 
Hujui Dini Yako na hautaona ahueni yoyote popote uendako maana hata Kwa Waislam wamegawanyika Sana tu, kuwa na makanisa utitiri Kuna kuzuia vipi wewe kuwa Mkristo? Kuwa mkristo na Kwenda Kanisani ni vitu viwili tofauti, Ukristo uko moyoni mwako. Soma Vizuri biblia na uelewe sio unapelekwa na maneno ya mitaani.
Mzee unasali wapi kwa mzee mwingira au ufufuo na uzima 😂😂
 
M nakushauri tu jaribu kuusoma na Uislamu
Jaribu kuwa muelewa hivyo vyote ni chuki kwa Mungu hata katika Biblia imeandikwa hizo ni tamaa za kibinadamu.

Kwani hakuna mashekhe wanaofanya kinyume na maandiko ya Quran???
 
Leo ni Jumapili ya matawi Yesu anaingia Jerusalem, lakini nikitafakari imani yangu ya ufuasi wa kristu napata mashaka makubwa sana.

To declare interest mimi nimezaliwa nimejikuta tu ni mkatoliki kwahiyo nipo hivyo mpaka leo, mahusiano yangu na Mungu naamini ni mazuri kiroho lakini mahudhurio yangu kanisani kwa miaka ya karibuni si mazuri huwa nakwenda na kuacha kwenda.

Basi mambo yasiwe mengi last Sunday nikatimba church kwenye parokia yetu mambo niliyokutana nayo huko ni ya kusikitisha na nathubutu kuita kile alichokikemea mwokozi wetu Yesu kristu kwamba wasigeuze nyumba ya baba yake kuwa pango la walanguzi, kwa hakika hicho ndicho kinachoendelea parokiani kwetu si kanisa tena bali ni pango la walanguzi.

Sisi Wakatoliki huko nyuma tulikuwa tukiwacheka Lutheran kwa utaratibu wa sadaka nyingi na bahasha nyingi kumbe sasa utaratibu huo umeingia kwa speed kubwa kwenye kanisa katoliki ibada ya misa moja sadaka mnatowa mara saba, sina hakika na parokia zingine hali ikoje.

Sasa kila mwanaparokia unapewa kadi ya kuchanga pesa ya kuwa mkatoliki mume na mke 10,000)= kwa mwezi na watoto buku mbilimbili kila mwezi hii ni nje ya sadaka harambee na michango mingine, tunakwenda wapi?

Najuwa wapo watetezi waliolewa mvinyo wa dini watatetea uharamia huu kwa utetezi ni lazima tuchangie ujenzi wa kanisa, hakuna anayekataa hilo na tumekuwa tukijitolea miaka yote kwa kiasi, lakini naamini mtu ambaye yuko free minded hawezi kutetea uharamia huu kugeuza kanisa kuwa pango la walanguzi, na wasiokuwa na pesa za kuamka kwenye mabenchi mara saba kutowa hizo sadaka hawatojisikia vizuri na wataacha kuja kanisani kwa kuteswa kihisa kila watu wakiinuliwa kwenye mabenchi wao hawana kitu.

Hiyo sasa tisa kumi ni hawa jamaa zetu born again, nipo hapa nyumbani namsikiliza mtumishi wa Mungu akitangaza viwango vya sadaka ya kugombowa uzao wa kwanza ni laki mbili, uzao wa pili laki na na nusu, uzao wa tatu laki.

Kutokana na uharamia huu na unyang'anyi unaoendelea kupitia mwamvuli wa dini serikali haiwezi kusaidia lolote katika hili kwa sababu ni partners muhimu in crime.

Kwakuwa waislamu wanajitambuwa sana katika hili ni wakati sasa kwa wakristu wote kuamka na kupinga dhulma hii ambayo cha kusikitisha sasa imeingia radmi kanisa katoliki na hakuna hata mkatoliki mmoja aliwahi kuhoji miradi yote ya kanisa hadi mkombozi bank ipo kwa faida ya nani na inalisaidia vipi kanisa?

Tumsifu Yesu kristu.
Ilo tatizo ni Tz nzima sa hivi nafikiri mapadre wanawaonea wivu wahubiri wa makanisa ya kilokole wakina mwamposa, gwajima, lusekelo nk na ivyo wanahisi watu wanapesa kumbe za kutoa pesa nyingi,
 
Jaribu kuwa muelewa hivyo vyote ni chuki kwa Mungu hata katika Biblia imeandikwa hizo ni tamaa za kibinadamu.

Kwani hakuna mashekhe wanaofanya kinyume na maandiko ya Quran???
Mkuu sasa hasira za nn? m kusema ivo we kimekuuma kipi?
 
Mkuu sasa hasira za nn? m kusema ivo we kimekuuma kipi?
Kimeniuma kipi?wakati nakwambia kuwa muelewa.
Umeanza huko juu kujibu dini ya haki ya kiislamu mara soma na uislamu ndo nmekujibu kuwa muelewa.
 
Huyo ni mkatoliki kabisa na asemacho ni kweli bila chenga. Hata mm ni mkatoliki naunga mkono home yake. Katoliki ukusanyaji wake wa fedha hata hao TRA wakasome.

Ili wakuhesabu unafaa huduma zao, lazma wajue kama unasali jumuia. Na huko jumuia ndio kuna michango na mikusanyo ya fedha isiyo mithilika. Kwa nyongeza tu, hata shule za katoliki bei ipo juu kama za watu binafsi, na zina michango na mahitaji ya malipo ya ajabu sana. Hata Mia ikipungua wanamtimua mtoto. Kwanza kuzipata tu hizo shule kwa mzazi alieshiriki michango ya ujenzi ni shida, hata kama mtoto ana vigezo.

Mleta mada kaeleza vyema sana, kuwa kama vyanzo vya mapato kama kumbi Mashule mahospitali frame za maduka vimejengwa kulisaidia Kanisa, sasa kuna haja gani ya kukakamua namna ya uporaji waumini walioshiriki ujenzi wake kwa fedha zao?

Hakuna mahali imeandikwa kwny biblia kuwa Utaenda mbinguni kwa kutoa sadaka au hutoenda kwakua hutoi sadaka. Unadhania Yesu alipo mwambie yule jamaa kauze ulivyonavyo uwape masikini kisha unifuate, angekuwa hawa mapadiri au wachungaji wa sasa, angesemaje kama sio kusema kauze ulivyonavyo kisha uvilete hapa ndio unifuate.
Ni vyema unapokuwa mtu wa imani ya dini fulani, basi ujitahidi kusoma na kuifuatilia kwa kini historia na utamaduni wa dini hiyo, kwani mambo kama hayo hayatakupa shida kabisa, haya siyo mambo ya kushangaa dini ni ushuru na biashara (hii imeonyeshwa kote, katika biblia & quran).

Huyu aliyeleta uzi, siyo mkatoliki.
 
Wavaa kobazi ni bahili hatari..wategemezi kila kitu wafanyiwe na waarabu..hadi tende wanasubiri waletewe na waarabu.

Ukristo ni dini ya upendo na utoaji..kama huna hela kaa kimya sio kutaka kuharibu utaratibu na tamaduni za wakristo.

#MaendeleoHayanaChama
Ndiyo maana nimesema unapokuwa muumini wa dini fulani, penda kusoma na kujua historia na utamaduni wa dini yako.

Mleta uzi hawezi kuwa mkatoliki, ila kajivika kofia ya ukatoliki kufikisha ujumbe wake.
 
Ndio maana nchi zilizoendelea makanisa yamegeuzwa museums watu walishashtuka siku nyingi kwamba huu wa sasa ni upigaji. Huku kwetu ndio bado watu wameng'ang'ania ila taratibu tutakuja kuelewana tuu.
Yes Bro ni suala la Time, First Time Ughaibuni nikasema Niende Church, Daah mzee Bonge jengo ila tulikuwa wachache sana; SO nadhani Kwa Africa ni suala la Muda tu, pia watu wanafunguka sana, hata hawa wa kwa manabii baadae wataona wanaibiwa hivyo nao wataona bora watulie tu waendelee na Maisha.
 
Kimeniuma kipi?wakati nakwambia kuwa muelewa.
Umeanza huko juu kujibu dini ya haki ya kiislamu mara soma na uislamu ndo nmekujibu kuwa muelewa.
bora ninyamaze mna ata sikuelewiii
 
Siyo lazima utoe sadaka ya cash. Nimeona waumini wengine wanaleta katoni 2-3 za maji ya Hill, miche ya sabuni ya kufulia, juisi, hata kuku mzima, etc. Lakini hii ni trend mpya kwa Wakatoliki. Wameiga kutoka Walutheri.
Kuleta hizo katuni za maji ni matoleo, tumefanya hayo miaka nenda rudi.

Tunachohoji ni kwa nini sasa hivi makanisani hatuendi kushibishwa neno badala yake michango ndio imetawala?

Hivi mjuwe tuna akili timamu aisee.
 
Ndiyo maana nimesema unapokuwa muumini wa dini fulani, penda kusoma na kujua historia na utamaduni wa dini yako.

Mleta uzi hawezi kuwa mkatoliki, ila kajivika kofia ya ukatoliki kufikisha ujumbe wake.
Wewe huna akili, kama kuanzia post ya kwanza mpaka hii ya mwisho hujanielewa basi huna akili kichwani.
 
Kuleta hizo katuni za maji ni matoleo, tumefanya hayo miaka nenda rudi.

Tunachohoji ni kwa nini sasa hivi makanisani hatuendi kushibishwa neno badala yake michango ndio imetawala?

Hivi mjuwe tuna akili timamu aisee.
Nafikiri Wazungu Wamisionari walipondoka na kuwaachia Watanzania, na misaada kutoka sadaka za Waumini wa Kizungu zikapungua, na pengineyo kukaauka kabisa.
 
Back
Top Bottom