Wana Jf wote heshima kwenu, ni muda sasa tunaona siasa za Tanzania na Rwanda zinavohitilafiana.
Na hivi majuzi Serikali kwa kutumia kodi zetu imemtuma Mwandosya Rwanda, lakini cha ajabu kabisa, gazeti la jana la News of Rwanda linakuja na habari ambayo kiuhalisia inashangaza na kama tutaiangalia kwa umakini labda ndio ile kauli ya bwana Paul ya 'me, i will wait for the right time and then i will hit him'.
Sioni mantiki ya habari hii kama serikali ya Tanzania inajaribu kutafuta suluhisho la kidiplomasia lakini wenzetu wako na mambo haya. Kama haitoshi nafikiri kuna haja ya ku-demand kwa serikali yetu ituambie hii nchi ni salama kiasi gani kama Rwanda wanaweza kuwa na habari nyeti hivi (kama ni kweli) zinazomuhusu mkurugenzi mkuu wa usalama wa Taifa na Raisi wetu.
Tafadhali watu wa serikali kama mnasoma hapa tungependa kupata majibu hii nchi ni salama kiasi gani????