hakika wengi wetu humu tufahamu taifa la israel, wayahudi, historia ya wayahudi na nguvu zao kisiasa na kijeshi. Na pia naamini wengi tunahamu rwanda, tutsi, historia yao na nguvu yao kisiasa na kijeshi. Hawa watu historia yao inafanana kiasi, wote wamepitia kipindi cha kuuliwa na kunyanyaswa sana tofauti wayahudi waliuliwa na wanazi wa kijerumani, na dikteta amin,nk kwa upande wa tutsi wao waliuwawa na majirani zao wahutu. Kwa sasa hawa watu wana dola wanaziongoza wayahudi israel watutsi rwanda na tunashuhudia jinsi hizi dola mbili zilivyo na usumbufu kwa nchi jirani israel mashariki ya kati na rwanda mashariki mwa afrika kiasi kwamba nchi za magharibi wakiongozwa na kilanja wao mkuu marekani wanashindwa wafanyeje na kubaki kusema kwa maneno tu eti israel ikomeshe kujenga makazi ya walowezi kule israel mara rwanda inasaidia waasi kule kongo waache mara moja, ukweli hizi jamii mbili ni hatari sana sasa, zilitaabika sana kwa kuuwawa kwa maelfu lakin hivi sasa mwenyezi mungu anazifuta machozi ukizigusa tu umeisha, mungu anakuadhibu. Ukiangalia israel kazungukwa na mataifa ya kiarabu ambayo baadhi ama yote hayampendi kwa sababu ya kunyanyasa ndugu zao wa palestina, kwa akili ya kawaida si wangeungana wakampiga ili akome ila kwa kuwa wale wahusika wanajua siri ya urembo. Ukija kwa upande wa rwanda utasikia serikali ya congo inalalamika rwanda wanasaidia waasi na wanapora madini rais analalamika, jeshi la congo linalalamika lakin kwa akili ya kawaida fikra zinasema kwa nn linchi likubwa kama congo lisikavamie na kukaadhibu karwanda ili kakome na kihelehele chake cha kuwasaidia waasi kunyanyasa wakongoman na kupola rasilimali zao? Ila wahusika kwa kuwa wana busara wanaijua siri ya urembo. Sasa huu msala naona umehamia kwa nchi yetu tanzania na kuna watu huku mtaani wanasema tuivamie rwanda weweweweweh! Sio jambo la kuthubutu kabisa hilo make cha moto tutakacho kipata hatutasahau sisi hadi wajukuu wetu. Hoja eti sisi nchi yetu kubwa karwanda kadogo. Hivi sisi nchi kubwa kuliko kongo? Vita sio linchi likubwa asee ndo unawin. Mfano marekani na nato wanapigana na kakikundi tu taliban waulize mziki ulivyo mnene. Namaliza kwa kusema hivi 'ushauri mzuri sio rahisi kuupata na hata ukiupata sio rahisi kuufuata hasa kwa mswahili' nashauri tanzania tusipigane na rwanda kijeshi tutajuta bali tupigana hivi kwa maneno au haya mambo yaishe kabisa na haya yote rais anajua na jeshi letu linajua sasa nyie huku kitaa shobokeni tu.