Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia. Lakini polisi watafanya uchunguzi bila ya kupata chanzo cha tukio kwa mashuhuda wa ajaliii?
Wahanga wapo, hivyo niwajibu wa hao wahanga wakashirikiana na polisi iliuchunguzi ufanyike kiuelediii.
Kwani shida iko wapiiii??
Na kwa nini wahanga hawafuatiliii wala kudai mwisho wa uchunguzi ulipofikia??
Sawa twende kwa hoja sasa;
Ni miaka mingapi imeshapita tangia tukio litokee?
Je polisi kutokana na mafunzo yao ya investigation and forensic wanauwezo wa kuwapata washiriki wa tukio hilo bila uwepo wa shuhuda ama mhusika au wanao?
Je baada ya Tundu Lissu kupata fahamu hakuwahi kuwaita polisi waende wakamhoji hospitali wakati yupo Nairobi? Je polisi walienda?
Aliporudi nchini alisema wazi polisi wakimhitaji ye yupo 24/7 je walishamhitaji?
Alipoenda kuguata gari lake pale central polisi Dodoma wakumbuka aliambiwa nini na RPC wa Dodoma?
Mkuu tuuweke uchama pembeni tuangalie facts na tukubaliane tu bila kurumbana.
Yote yaliyotokea kuanzia kushambuliwa kwake;
Kukatazwa na onyo kutolewa kwa wabunge wataokwenda kumtembelea,
Kuzuiliwa kwa mkusanyiko wa maombi ya kumuombea,
Kamatakamata ya wote waliokuwa wanavaa fulana zenye maandishi ya kumtakia afya njema,
Kunyimwa pesa za matibabu
Kuvuliwa ubunge bila kufuata sheria na katiba za jamhuri wa Tz
Tuanzie hapo bila hiyana. Hayo kichwani mwako yanakupa tafsiri gani?
THE RULE OF INVESTIGATION WORLDWIDE IS TO CONNECT THE DOTS AND COME UP WITH SOMETHING