Kuna Maisha Nyuma ya Hizi 'ID' Zetu, Tusiache Kupendana ❤️

Kuna Maisha Nyuma ya Hizi 'ID' Zetu, Tusiache Kupendana ❤️

Umezungumza jambo la msingi na la kiungwana sana, Mshana Jr. Hakika umegusa nyoyo za wengi.
Ni kweli kabisa kuwa nyuma ya hizi ID zetu za kufikirika kuna binadamu halisi wenye hisia, changamoto, na mapambano makubwa ya kimaisha. Wakati mwingine maneno yetu ya faraja humu jukwaani yanaweza kuwa ndio tiba pekee ya mtu inayomfanya asikate tamaa. Asante kwa kutukumbusha umuhimu wa upendo, uvumilivu, na kutengeneza mazingira salama kwa kila mmoja wetu. Mungu akubariki pia kwa moyo huu wa kipekee.

Mwisho kabisa kiongozi wangu, kwa kuwa umesema JF ni mahali pa kuchangamsha akili na kupeana changamoto... Kuna swali moja wadau humu chini chini wanajiuliza: Hivi bado una ile biashara yako ya kufuga na kuratibu majini, au siku hizi umeamua kuegemea kabisa kwenye mambo haya ya kiroho na upendo pekee? 😄🙌
Asante Sana brother! Kijana wa Ifoza ..! Kile kilinge na mambo yake yote niliachana navyo na kumrudiq Mungu wangu🙏🏿💪🏿.. Kwasasa Mimi ni mtumishi natumika kwenye madhabahu za nuru..!
 
Umezungumza jambo la msingi na la kiungwana sana, Mshana Jr. Hakika umegusa nyoyo za wengi.
Ni kweli kabisa kuwa nyuma ya hizi ID zetu za kufikirika kuna binadamu halisi wenye hisia, changamoto, na mapambano makubwa ya kimaisha. Wakati mwingine maneno yetu ya faraja humu jukwaani yanaweza kuwa ndio tiba pekee ya mtu inayomfanya asikate tamaa. Asante kwa kutukumbusha umuhimu wa upendo, uvumilivu, na kutengeneza mazingira salama kwa kila mmoja wetu. Mungu akubariki pia kwa moyo huu wa kipekee.

Mwisho kabisa kiongozi wangu, kwa kuwa umesema JF ni mahali pa kuchangamsha akili na kupeana changamoto... Kuna swali moja wadau humu chini chini wanajiuliza: Hivi bado una ile biashara yako ya kufuga na kuratibu majini, au siku hizi umeamua kuegemea kabisa kwenye mambo haya ya kiroho na upendo pekee? 😄🙌
Wakati mwingine maneno yetu ya faraja humu jukwaani yanaweza kuwa ndio tiba pekee ya mtu inayomfanya asikate tamaa.💕💕💕
 
Ingekuwa ni nchi za nje hapo aliposimama akifungia zipu tu t
Niseme tu Asante sana icon wa JF Mshana Jr

Hakika maandishi yako huku yame add kitu kwenye maisha ya wengi.

Wengine ambao nawakubali sana humu ni wafuatao
Erythrocyte
secretarybird
Mbaga Jr
ShesRise_1
Seran
leo dada
min -me
Marcostilone
Bujibuji Simba Nyamaume
Infropreneur
Kiranga
Eli Cohen
Pascal Mayalla

Na wengine wengi ambao sijawa mention Asanteni sana, Mungu awabariki
Leo dada


Unamkumbuka kwa lipi ?
Jina lake limenivutia
Huenda nami nikawa kama wewe,
Emu sema
 
Amri iliyo kuu ni UPENDO! Basi tupendane..
Leo nimekaa nikitafakari kwa kina kuhusu jukwaa letu.

Mara nyingi tunakutana humu kuchangamsha akili, kubishana, na wakati mwingine kupeana changamoto za kimaisha.

Lakini ukweli ni kwamba, nyuma ya kila jina unaloliona humu (hata yale ya kufikirika), kuna binadamu halisi.

Kuna mtu anasoma posti yako huku yuko wodini anaumwa, mwingine ananuka madeni, mwingine kaachwa...

Mwingine kapoteza kazi, mwingine ana msongo mkubwa wa mawazo na JF ndio kimbilio lake pekee la kupoteza muda ili asijisikie mpweke.

Humu ndani wengi hatujuani kwa sura, lakini mioyo yetu inagusana kupitia maandishi yetu.

Huu uzi sio wa ligi wala malumbano. Ni uzi wa faraja. Kama kuna mwana-JF uandishi wake umewahi kukufariji siku ukiwa na upweke, mtag hapa umwambie "Asante". Kama uliwahi kumkwaza mtu kwa maneno makali humu ndani, omba msamaha hapa.

Maisha ni mafupi mno, na hatujui kesho yetu.

Tuigeuze JF kuwa sehemu salama (safe space) ya kupendana, kufarijiana, na kuinuana kiroho.

Mimi nawaombea heri na baraka ninyi nyote mnaosoma ujumbe huu. Mungu awabariki na kuwapa amani ya mioyo yenu. Nawapenda sana! 🙏🌹View attachment 3648845
Bonge la ujumbe mkuu 🙏🏽🙏🏽
Nimeupokea kwa mikono miwili 🤝🤝
 
Bonge la ujumbe mkuu 🙏🏽🙏🏽
Nimeupokea kwa mikono miwili 🤝🤝
Let love lead❤
87b9d3f6-caba-4cf1-ad9a-06a5b9b99cf4.jpeg
 
Asante pia kwa kuyageuza MAWAZO yako ya busara kuwa maandishi mkuu,,atakaye pingana na hili, hakika atakuwa si mwenzetu,,💪🏽💪🏽
 
binafsi kama mtumishi na kiongozi wa wananchi,
wadau wote wa JF ni ndugu, jamaa na marafiki zangu.

nitawaheshimu, nitawathamini na kuwapenda daima licha ya utofauti wa mirengo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Siwezi kua na chuki ya muda mfupi au muda mrefu na mdau yeyote yule wa Jf kwasababu yoyote ile jukwaani.

I love you all my fellow Tanzanians without any condition 🐒
Heshima yako mkuu nakupa salute 👮🫡 Tlaatlaah
 
binafsi kama mtumishi na kiongozi wa wananchi,
wadau wote wa JF ni ndugu, jamaa na marafiki zangu.

nitawaheshimu, nitawathamini na kuwapenda daima licha ya utofauti wa mirengo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Siwezi kua na chuki ya muda mfupi au muda mrefu na mdau yeyote yule wa Jf kwasababu yoyote ile jukwaani.

I love you all my fellow Tanzanians without any condition 🐒
Id zetu hizi Zina mambo mengi lakini walio na I'd hizi ni watu pia, wanakula nakutembea, tuachane nayo hayo Leo Yanga amewaka balaa 😀
 
Back
Top Bottom