Kuna Maisha Nyuma ya Hizi 'ID' Zetu, Tusiache Kupendana ❤️

Kuna Maisha Nyuma ya Hizi 'ID' Zetu, Tusiache Kupendana ❤️

Attachments

  • FB_IMG_1737571634559.jpg
    FB_IMG_1737571634559.jpg
    72.2 KB · Views: 9
Umezungumza jambo la msingi na la kiungwana sana, Mshana Jr. Hakika umegusa nyoyo za wengi.
Ni kweli kabisa kuwa nyuma ya hizi ID zetu za kufikirika kuna binadamu halisi wenye hisia, changamoto, na mapambano makubwa ya kimaisha. Wakati mwingine maneno yetu ya faraja humu jukwaani yanaweza kuwa ndio tiba pekee ya mtu inayomfanya asikate tamaa. Asante kwa kutukumbusha umuhimu wa upendo, uvumilivu, na kutengeneza mazingira salama kwa kila mmoja wetu. Mungu akubariki pia kwa moyo huu wa kipekee.

Mwisho kabisa kiongozi wangu, kwa kuwa umesema JF ni mahali pa kuchangamsha akili na kupeana changamoto... Kuna swali moja wadau humu chini chini wanajiuliza: Hivi bado una ile biashara yako ya kufuga na kuratibu majini, au siku hizi umeamua kuegemea kabisa kwenye mambo haya ya kiroho na upendo pekee? 😄🙌
 
Amri iliyo kuu ni UPENDO! Basi tupendane..
Leo nimekaa nikitafakari kwa kina kuhusu jukwaa letu.

Mara nyingi tunakutana humu kuchangamsha akili, kubishana, na wakati mwingine kupeana changamoto za kimaisha.

Lakini ukweli ni kwamba, nyuma ya kila jina unaloliona humu (hata yale ya kufikirika), kuna binadamu halisi.

Kuna mtu anasoma posti yako huku yuko wodini anaumwa, mwingine ananuka madeni, mwingine kaachwa...

Mwingine kapoteza kazi, mwingine ana msongo mkubwa wa mawazo na JF ndio kimbilio lake pekee la kupoteza muda ili asijisikie mpweke.

Humu ndani wengi hatujuani kwa sura, lakini mioyo yetu inagusana kupitia maandishi yetu.

Huu uzi sio wa ligi wala malumbano. Ni uzi wa faraja. Kama kuna mwana-JF uandishi wake umewahi kukufariji siku ukiwa na upweke, mtag hapa umwambie "Asante". Kama uliwahi kumkwaza mtu kwa maneno makali humu ndani, omba msamaha hapa.

Maisha ni mafupi mno, na hatujui kesho yetu.

Tuigeuze JF kuwa sehemu salama (safe space) ya kupendana, kufarijiana, na kuinuana kiroho.

Mimi nawaombea heri na baraka ninyi nyote mnaosoma ujumbe huu. Mungu awabariki na kuwapa amani ya mioyo yenu. Nawapenda sana! 🙏🌹View attachment 3648845
Utuuzima dawa, ndo hii sasa.👏
 
Back
Top Bottom