Kuna matunda mengi sana, ila mimi nalipenda zaidi hili... Je wewe unapenda lipi zaidi?

Kuna matunda mengi sana, ila mimi nalipenda zaidi hili... Je wewe unapenda lipi zaidi?

The silent smile

Senior Member
Joined
Jul 17, 2025
Posts
124
Reaction score
206
Habari Wadau:

Inafahamika kuwa kila binadamu ana kile anachokipenda zaidi, na asichokipenda zaidi katika vyakula na matunda..
Kwenye upande wa matunda nayapenda mengi tuu, ila katika hayo yote kuna tunda nalipenda zaidi na bahati mbaya sikutanagi nalo mara kwa mara,
Tunda lenyewe linaitwa STAFELI (TOPETOPE) 😄 Ebanaee hili tunda nikilipataga najionaga kama namiliki dunia, kwa upande wangu nalipenda mnoo, na huaga kuna muda nalimiss sana Wallah.

Vipi wewe mdau kwa upande wako, ni tunda gani unalolipenda zaidi kuliko yote. (Msije mkamaanisha lile lingine, maana hamkawii😄).
 

Attachments

  • Stafeli.jpeg
    Stafeli.jpeg
    25.9 KB · Views: 38
Hongera kwa kulipenda stafeli lakini hili ni tofauti na topetope.

Stafeli la kijani na Lina kama mibamiba kwa juu huku stafeli likiwa la kijani chakavu likiiva linabadili rangi kwenda unjano, wekundu kutegemeana na breed.

Stafeli ni tamu saana... uliloweka kwenye picha ni stafeli.
 
Mimi huwa nakula sana fenesi nilinunua morogoro3 moja nikalila mara2 tu nilihalisha sana... na yalikuwa makubwa bahati nzuri au mbaya wana familia liliwashinda hivyo yote3 nilimaliza mwenyewe...

Ilifikia mahala hata nikiamka saa8 usiku halafu yake tu ikinijia naenda jikoni kula
 
Beer....🍻
Ikipita siku moja sijakunywa basi ujue ninaumwa, tena nina tumia dawa.
Ohhh....
Hivi kumbe mlikua mnazungumzia matunda..!!
Mudi wakiona aje watafuta hii komenti...🙄
 
Hongera kwa kulipenda stafeli lakini hili ni tofauti na topetope.

Stafeli la kijani na Lina kama mibamiba kwa juu huku stafeli likiwa la kijani chakavu likiiva linabadili rangi kwenda unjano, wekundu kutegemeana na breed.

Stafeli ni tamu saana... uliloweka kwenye picha ni stafeli.
Nikweli, yanafanana sana hiyo aina, ila topetope ndo nlikuwa nalikusudia. Dahh, yaan hadi nikiandika jina lake udenda wanitoka maana nina muda sijalila
 
Mimi huwa nakula sana fenesi nilinunua morogoro3 moja nikalila mara2 tu nilihalisha sana... na yalikuwa makubwa bahati nzuri au mbaya wana familia liliwashinda hivyo yote3 nilimaliza mwenyewe...

Ilifikia mahala hata nikiamka saa8 usiku halafu yake tu ikinijia naenda jikoni kula
Fenesi tatizo ule utomvu na sukar nyingi, mimi nikilaga nyama zake 5 tuu nishatosheka, huku nilipo yanaozeaga juu ya miti yake, na wala sinaga muda nayo
 
Back
Top Bottom