Kuna matunda mengi sana, ila mimi nalipenda zaidi hili... Je wewe unapenda lipi zaidi?

Kuna matunda mengi sana, ila mimi nalipenda zaidi hili... Je wewe unapenda lipi zaidi?

Habari Wadau:

Inafahamika kuwa kila binadamu ana kile anachokipenda zaidi, na asichokipenda zaidi katika vyakula na matunda..
Kwenye upande wa matunda nayapenda mengi tuu, ila katika hayo yote kuna tunda nalipenda zaidi na bahati mbaya sikutanagi nalo mara kwa mara,
Tunda lenyewe linaitwa STAFELI (TOPETOPE) 😄 Ebanaee hili tunda nikilipataga najionaga kama namiliki dunia, kwa upande wangu nalipenda mnoo, na huaga kuna muda nalimiss sana Wallah.

Vipi wewe mdau kwa upande wako, ni tunda gani unalolipenda zaidi kuliko yote. (Msije mkamaanisha lile lingine, maana hamkawii😄).
Kuna tofauti kati ya Stafeli na Topetope.

Stafeli lina utamu ndani yake kwa wingi tofauti na Topetope ambalo lina kauchachu kwa mbali.

Na Stafeli haziwi kubwa kama tope tope.
 
Back
Top Bottom