Tetesi: Kuna Mawaziri watapanguliwa kazini muda wowote

Sitaki kutaja majina ila tetesi zilizopo ni kuwa

1 : Mkuu wa taasisi nyeti ya Serikali mmoja ataondolewa

2: Mawaziri wa baadhi ya wizara kupanguliwa.

Ni kutokana na mkuu analalamika mambo hayaendi kama anavyotaka yaende.

My take: pole yenu mtakaopatwa na mtikisiko.

Stay tuned

Kwa style yake ya uongozi mambo hayawezi kwenda kweli. Atabadili mwishowe ataacha tu mambo yajiendee
 
Nikuulize mleta mada, je ni mambo gani hayaendi sawa? Usipojibu swali hilo basi utakuwa umechanganyikiwa
Bandarini(FLOW METER)mwanzoni mwa awamu hii Raisi na PM walitembelea bandari na kugundua mafuta yanapakuliwa bila kuhesabiwa.hadi jana apita tena bado mita hizo hazifanyi kazi!!!!!!!
 
Kuna habari zimetapakaa hapa mjini kuwa Rais Makufuri anatarajia kupangua Baraza la Mawaziri siku yoyote kuanzia sasa.

Imeelezwa sababu za Rais kupangua Baraza hilo ni kuwafuta kazi baadhi ya mawaziri ambao wameshindwa kwenda na kasi ya Hapa Kazi Tu hivyo ameona bora awabwage baadhi ya mawaziri mizigo badala ya kuendelea kuing'ang'ania kuwabeba.

Hii itakuwa ni mara ya pili Rais kuwafuta kazi mawaziri tangu alipomfuta kazi Waziri Charles Kitwanga kwa sababu ya kulewa akiwa kazini. Mtangulizi wake Rais Kikwete alibadili Baraza la Mawaziri zaidi ya mara 8 kwa sababu mbalimbali zikiwemo kashfa maarufu za Richmond, Operesheni Tokomeza na Escrow.

Tusubiri tuone ni kina nani watakaopitiwa na panga hili la Makufuri na nani watapenya kwenye tundu la sindano. Kuna kila dalili kwamba kuna baadhi ya mawazi watafutwa kazi kwa sababu ya ama kumdanganya rais au kutojituma ipasavyo kwenye nafasi zao. Je, unaweza kutabiri nani atakuwa wa kwanza kupitiwa na panga hili?

Nawasilisha
 
kama zimetapakaa mjini, MBNA mm cjacikia
 
amewachagua watu wengi kwa kuangalia ukada na uchama mwisho wa siku kumbe performance hawana awatumbue tu hamna namna,ajitahidi kutuangalia na sisi tusio na mrengo wowote wa kichama na kazi tunaziweza!😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom