Kuna mji wenye usafiri mzuri wa daladala na elimu nzuri kuliko Mbeya?

Kuna mji wenye usafiri mzuri wa daladala na elimu nzuri kuliko Mbeya?

Mm nachojua Mbeya n Kijiji kikubwa

Huwez fananisha na Arusha kwa kweli

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Endelea kujua hivyo hivyo ..

Sweet Mbeya 👇

2940500_tzcucom-___CP4r_ptNOB5___-.jpg


2940503_Screenshot_20210918-123445_1631958166649.jpg


2940501_jr_sports_tz-___CRcAdcUroHE___-.jpg


2940502_mdopeiddehotel_tz-___CTujdtdtA1K___-.jpg
 
Mbeya inajitahidi

Inatosha kusema hivyo. By the way poleni kwa Vumbi
 
Mbeya imenyimwa barabara kwa sababu za kisiasa ndo maana ni mji umejaa vumbi kwa sababu barabara za mtaa zote hazieleweki.

Mara ya mwisho kwenda Mbeya ni lini?

Mbona kama mji una lami sehemu nyingi tena ndani ndani, kitu ambacho kimefanyika Sugu akiwa mbunge...

Na ukitazama bado kuna sehemu wana mpango wa kutandaza lami...
 
Hakika sijaona mji wenye system nzuri ya daladala kama Mbeya. Stendi kubwa zipo tatu kuna ya mjini ambayo ni stendi kuu ya zamani na ni kubwa kiasi kwajili ya mabasi ya mikoani na daladala, kuna stendi kabwe hii ni kwajili ya daladala na bajaji na pia utaikuta stendi kuu ya nane nane.

Nimejaribi kufananisha na miji mingine bado sijaona, kwa mfano pale Arusha hakuna hata stendi moja inayoeleweka kwajili ya daladala yaani hata stand ya mabasi ya mkoani pale town bado sana.

Elimu -

Shule za msingi - zipo shule tatu za serikali za mtaala wa Kiingereza ada laki 3, ipo Shule ya Azimio, Mkapa na Magufuli. Shule za private nazo zipo kuna Umoja, Riverside, Saint Mary, Uwata, n.k. shule za serikali pia zipo kibao kama utitiri, Sisimba ndio kinara na kongwe

sekondari - zipo za umoja wa wazazi kuanzia Sangu, Meta, Ivumwe, Mbalizi, n.k huku niseme tu ya kwamba ufaulu upo ila na njiti zinatembezwa hasa, ukija shule za serikali nazo zipo Samora, Mbeya day, forest, n.k ukija private nazo zipo st marys, uwata, pandahill, Swilla, n.k. shule za kata ni nyingi sana.

Vyuo - M.U.S.T, Udsm - mchas, Udsm - ucc, Mzumbe, Tia, Open, utumishi, cbe, Saut, Adem, Tumaini, Teku, n.k ukija vyuo vya uuguzi na ufundi napo vimejaa si mchezo kuna Mbalizi, k's, moravian, veta, n.k ni vingi sana.

Kwa hali hii wacha niwape pongezi Mbeya
Kiongozi umetoa mfano mzuri sana kwa daladala za Mby hata madereva wana nidhamu sana tofauti dereva wa daladala Dar na Vifodi Arusha very hopeless
 
mkuu, labda mbeya ya zamani, siku hizi daladala nyingi ni costa kubwa tu
Hizo zote ni Costa mizigo
Matenga na magunia ya vitunguu mengi kuliko abiria.
Halafu usifungue dirisha, mbepo.
Kama watu hawaelewi maana ya madirisha na hewa safi elimu iko wapi.
 
Mm nachojua Mbeya n Kijiji kikubwa

Huwez fananisha na Arusha kwa kweli

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Arusha stendi ya mabasi zina viwango vya chini mno, ile ya pale mjini haifikii hata robo ya stendi ya zamani ya Mbeya.

kuhuusu vyuo ukiachana na IAA, Arusha tech na uoa kuna chuo kipi? kunashule ngapi za mitaala ya kiingereza za serikali??
 
Mbeya kuna barabara mbaya sijawahi kuona kwanza ni nyembamba sana jiografia yake ni mbaya sana milima mingi yani kwa wale wenzangu na mie wa Daslam wapenda mbio hiku kudanja ni dakika sifuri ukitoka tu barabarani umeingia kwenye miti au korongo biashara imeisha...mfani barabara ya kutoka mbeya kwenda kyela mbaya sana
Dar mnaendeshaga kwa spidi mnaendaga wapi?
 
Maskini mkibishana katika ubora wenu wakati mi Niko zangu Burj khalifa Dubey nawazoom tuu!
We maskini mwingine piga ufagio uzoe nya za hao waarabu wakishachimbana mitaro.
Wenzio tuko NYC hatuongei we bishana na maskini wenzio.
 
Back
Top Bottom