Kuna mmama alikuwa ananiangalia sana hadi nikajishtukia, nilipomchunguza vizuri nikagundua ni class mate wangu

Hahahaa mi napenda kunenepa ila nisiwe jimamaa lenye kitambi, niwe na mwili fulani hivi ila waaaapii , ngoja niendelee kufukia msosi
 
Hahahaa mi napenda kunenepa ila nisiwe jimamaa lenye kitambi, niwe na mwili fulani hivi ila waaaapii , ngoja niendelee kufukia msosi
Mkuu,
Usipo beba mizigo moyoni...hautembei na watu kichwani mwako (umebeba burden nyingii)

Trust me,
Akili ikitakata mwili lazima unawiri na kunenepa (hata ngozi utakua na mng'aro amazing)

Kuna factor nyingi ili uweze kutakata akili...
 
Ukiwa na miaka 20s ukazingatia ushauri wa prof Janabi.

Kula kwa kias

Stress free

Unajua ukila chakula kingi metabolism .... Hufanya mwili muda wote kufanya kazi ya kumengenya chakula.


That's is why watu wa kijijini wanazeeka haraka sababu ni kula chakula kingi.


Kuzeeka sio tatizo Ila unabidi kuzeeka katika ubora wako.
 
Mimi ki umri aisee nimekula chumvi ila ki umbo aah ..nikitoa hizi ndevu na huu upara ..walahi narudi sekondari kabisa
Kuna siku nimekutana na Class mate wangu (KE) shule ya msingi, mtoto wake wa kwanza, naweza mposa na nikaoa kabisa.

1. Lakini yeye sasa, kawa mbibi kabisa na ana wajukuu wakubwa tu.... Miaka yetu kwanza ndiyo tunaingia kwenye ghorofa ya Nne. Wanawake wanawahi sana kuchoka plus stress za maisha ndiyo kabisa
 
Wakishazaa wanapata ile minyama ya juu ya kiuno imejikunja kunja, akivaa gauni lakubana linamweza na hizo nyama. Tayari anaonekana bibi kabisa.
 
Kundi ambalo linachelewa kuzeeka ni waalimu,, nadhani ile kufundisha wamesimama zoez tosha,,

Hizi kazi unakula kiyoyozi chapati tatu na misupu,, lazima uchoke,,

Lakin pia inategemea na udongo
First born wangu anasomeshwa na mwalimu aliyenifundisha chekechea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…