Kuna mpasuko unafumwa kisayansi ndani ya CCM na wamefanikiwa kwa 100%. Rais amechelewa kusoma mchezo

Ni maoni tu ya kawaida, binafsi unavyoona mwenyewe hali ilivyo. Samia kayakoroga mengi zaidi kuliko hayo uliyo yataja wewe. Ni kiongozi aliyetokea tu kuwepo bila ya kuwa na uwezo wa kuongoza.

CCM unayo izungumzia kwa kiasi kikubwa ni ya makundi ya maslahi tu. Sioni kiongozi mwenye uzito wa kimtazamo na dira ya wapi chama kinakotakiwa kusimamia.

Ushauri wako kwa CHADEMA huko mwisho uzingatiwe kwenda mbele; wasifanye tena mambo kimazoea.

Kama kuna la kujifunza kwa vyama vya upinzani, hasa CHADEMA; na wananchi kwa ujumla wasioshabikia uchama pekee na maslahi; haya yanayojitokeza sasa ni 'trailor' tu la yanayo kwenda kujitokeza kwenye chaguzi za Serikali za mitaa na huo uchaguzi mkuu mwakani.
Kama kweli tunataka Tanzania isitumbukie shimoni, inabidi kuanza sasa hivi kukataa kwa nguvu zote hujuma hizi zinazopangwa na Genge la Samia.
 
Asigombee itakuwa heri maana miaka takriban 4 nchi imedorora ndo akae mingine 5 Zimbabwe itakuwa nafuu,
Alafu hapo hapo nasikia form four failure Lukuvi akasema Samia aendelee hadi 2035!

Kwanini watu wanachezea Katiba kiasi hiki?

Inajulikana Mungu akipenda Muda wake ni 2030 Ila Haya ya 2035/40 Hapana


Britanicca
 
Alafu hapo hapo nasikia form four failure Lukuvi akasema Samia aendelee hadi 2035!

Kwanini watu wanachezea Katiba kiasi hiki?

Inajulikana Mungu akipenda Muda wake ni 2030 Ila Haya ya 2035/40 Hapana


Britanicca
Hata hiyo 2030 hatakiwi kufika aishie hapo 2025, huyo fom foo kaokotwa jalalani anajiropokea tu,
 
niliwaza kitu kama hiki kichwani
Umeeleweka vyema
 
Tukiacha chuki binafsi huyu mama anajitahidi sana ...imagine ajira zote zilifungwa lakini now aghalau anaajiri...sasa hivi wanasiasa hasa upinzani wanaongea freely lakini nyuma kidogo hili halikuwezekana..mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni
Alivyoanza ndivyo ilivyokuwa lkn alipo na anapoelekea tayari ameshapoteza muelekeo. Sasa hivi anategemea ramli chonganishi toka kwa DAB (rej: "nimetumiwa clip ya.... na kuisikiliza")
 
Asigombee itakuwa heri maana miaka takriban 4 nchi imedorora ndo akae mingine 5 Zimbabwe itakuwa nafuu,
Mkuu, sijui una maana gani unaposema "asigombee"!
Huyu hagombei kwa maana tuijuayo ya kugombea. Huyu tayari anatengeneza mipango ya kuendelea kuwepo kwa hiyo nguvu ya dola.
Tena umetaja Zimbabwe, ambako ndiko mfano wake unatumika sasa hivi kuhakikisha Samia anabaki kwenye madaraka.

Kama hutaki iwe hivyo, umiza kichwa kutafuta njia zitakazo zuia hilo lisitokee, na toa mchango wako huo watu wau angalie kama unafaa kumzuia asiendelee kuwepo madarakani kwa mabavu.
 
Mimi niliogopa sana Mheshimiwa Rais aliposema AMETUMIWA CLIP YA KATIBU MKUU WA CCM na kaisikiliza...

Unajua Nani alimtumia na kwanini Amtumie??

Uking’amua hili basi
Hata mimi kwa hili nilishangaa sana kumsikia akitamka hivi....

Hivi katibu mkuu wake angewezaje kwenda kufanya Press Conference kuongea na waandishi wa habari kuhusu maswala ya nchi bila mwenyekiti wake wa chama na Rais wa nchi kuwa wamekaa na kukubaliana...?

Kama Dr. Emmanuel Nchimbi (GS - CCM) hakumshirikisha wala kuwasiliana na mwenyekiti wake wa chama siku ile anaongea na Press, basi haina shaka yoyote kuwa KUNA MPASUKO MKUBWA SANA CCM na anguko la Samia Suluhu Hassan liko plotted humohumo...

Mimi nakubaliana na wewe kabisa. CCM imeyumba na ndiyo maana nchi nayo sasa inayumba na Rais anachezeshwa shere naye analicheza kwelikweli...!
 
Haahaa sema umemaliza kila kitu, wale wakusikilizia ndo wabaya sana hao
 
Huyu mama ana tatizo la kufikiri

Yeye anadhani Chadema ni adui yake kumbe the real adui ni CCM humo ndani

Hua namshangaa sana

Yaani yeye kwa akili yake anadhani adui yake yeye ni Mbowe na Lissu?Really?

Ngoja aipate sawasawa ndio ataelewa Lissu,Mbowe na Chadema ni wenzake na sio maadui kama anavyodhani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…