Kuna mtu amewahi kupata kazi ya maana kwa kutumia waganga wa jadi?

Inawezekana ndio hitaji lake la kwanza hilo.
 
Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe.
 
Sawa ngosha
 
Duuh
 
Hakuna kitu kama hicho kazi una apply kupitia portal au email je utaroga mfumo wa computer?
Tatizo vijana wenzetu wamevurugwa na maisha na wanazidi kuji vuruga zaidi. Haya mambo ni imani maana kuna watu wamezaliwa katika familia au koo zenye kuendekeza ushirikina so wanafikiria kila jambo ni ndumba tu. Imagine, sampuli ya watu hawa wanakua wasindikizaji tu maana hata wakibahatika wanakua mizigo hawana ile feeling ya kuhustle in reality. All in all, Vijana wenzangu endeleeni na ndumba na kuroga ili mfanikiwe na endeleeni kuwaangalia wanaume wanaotoka jasho na kuumiza kichwa wakiwa wanapambania fursa.
 
Achana na waganga matapeli wa dar hao.

Njoo huku kwetu morogoro nikupeleke kwa wataalamu huko ifakara ndani ndani.

Vijana msione watu ni mawaziri mkadhani ni bahati, ile ni kazi ya ndumba
Ifakara sehemu gani kuna mganga zaidi ya kukaa matapeli tu.
Mganga mwenyewe hana kazi ndio akupe wewe kazi.
Wajinga ndio waliwao.
 
Itakuwa ngumu sana kuhusishanisha kupata kazi na huo u-witchdoctor. Inabidi ukawaulize na waliokuwa kwenye interview panel kuwa walijisikiaje alipoingia candidate huyo mwanzo mpaka mwisho.
 
Mkuu.umenikumbusha kuna kipindi bro wangu alikua na kesi ya roberry..tukaenda huko morogoro kwa mtaalamu..at the beginning bro alikua kapigwa 30 yrs..surprisingly bro akachomoka kwenye rufaa kama babu alivyotuahidi.
Kaka yako ni jambazi na mnamuacha uraiani
 
Mganga anaweza kukupa dawa, na certificate yako ukamuendesha mwenye degree kama gari. Wapo wengi makazini wanaotamba kwa ajili ya waganga. Ila maana mafanikio ni siri, wametulia na wanapasua Sala kama kawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka mwaka 2010 kuna jamaa yangu alipataga kazi alipewa dawa na mganga mimi nilikataa sababu ya imani yangu.
Leo hii mimi nipo kitaa nilipataga kazi ikayeyuka na nikapoteza kila kitu. Jamaa yangu ni finance and administration director wa NGO kubwa tu hapa bongo na amefungua pub inakimbiza sana mjini kwa kifupi jamaa ana kila kitu anachotakiwa kuwa nacho kijana aliyefanikiwa. Sijawai kumuuliza tangu wakati ule kama alitumia tena ndumba nyingine ila na mimi nafikiria kwenda kwa mtaalam anisaidie hali yangu ya maisha imekuwa mbaya kazi zimefungwa.
 
hahahahahhaahaahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…