Kuna mtu anazurura na Hummer EV hapo mjini. Chuma hata kwenye kikokotoo cha TRA haipo!

Kuna mtu anazurura na Hummer EV hapo mjini. Chuma hata kwenye kikokotoo cha TRA haipo!

Nje ⁴ya mada:


Mbona hivi vi pikipiki vya umeme havina usajiri/number plate.
Tax Act ya mwaka 2004 hakiulelezea mambo ya EV , mfumo wa calculation zile base kwa ukubwa wa engine “cc” na rate zake, hizi EV na gari ya full LNG hazikupigiwa hesabu ndio maana haziko kwenye mfumo wa kodi kama za magari ya diesel na petrol
 
Kwa gari kama Hummer, ambalo ni kubwa na zito, halipo efficiency sana.
Hii ina efficiency ya 2.6 km kwa kWh. Yaani unit moja ya umeme inaenda kilometa 2.6 kwahiyo kwa kilometa 450 utatakiwa uwe na unit 173 ambazo ni kama Tsh Elfu 60.

Ila gari kama Tesla model 3 ina efficiency ya 7-8 km kwa Kwh. Yaani unit moja ya umeme unaenda kilometa 7-8.
Hii inatokana na uzito na drag coefficient, kwahiyo kwa izo kilometa 450 ukiwa na Tesla utatakiwa utumie unit 56 ambazo ni kama Tsh 20,000/=

Efficiency ni kama unavyosema fuel consumption ya gari.
Ukichukulia hiyo hiyo hummer bado ya umeme ni nafuu zaidi ya mafuta.. Kwenye matumizi ya nishati.
Umeme wa elfu 60, unaweza kuambulia lita zipatazo 22 hivi.. Kwa gari inayotembea km 5-8 kwa lita, unaweza jikuta umeenda km 100 mpaka 150+ hivi, yaani hapi dar moro, hujafika Morogoro chuma inadai wese... Ila ya umeme kwa umeme wa 60k, unaisaka Dom bila tabu.
 
Back
Top Bottom