Kuna muda kiongozi unahitaji ukichaa kufanya mabadiliko yenye tija

Kuna muda kiongozi unahitaji ukichaa kufanya mabadiliko yenye tija

SheriaE

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
626
Reaction score
557
Wakati wana wa Israel wanaelekea kanaani kuna Muisrael alietwa Kora yeye kazi yake kubwa ilikua kupinga safari ya Musa na wana wa Israeli. Bila Mungu kuingilia kati kumuangamiza Kora huenda mpk leo wana wa Israeli wasingefika kanani.

Pia inanikumbusha hadithi ya Gadaffi na wa Libya walipopandikizwa sumu hatimaye wakamuua huku wasisikie maneno yake akilia kwakuwambia "wanawadanganya muniue lakini mtakuja kujuta"kuna muda Wazungu wanatuona manyani maana Muafrika akiwa mbele ya mzungu ni fulu kuponda nchi yake na viongozi wake..kusema kweli mafisadi/ wapiga dili/ mabepari/ wazembe/ Waajiriwa wakisikia jina la Magufuli wanaweweseka ila wazalendo wakisikia jina hilo wanafurahi halafu wanakukumbuka zama za kina Thomas Sankara, P Lumumba, Samora Machel, J.kNyerere.

Rais anayeamini kwenye kujaribu na kushindwa kuliko kutokujaribu kabisa ipo neema kwenye kujaribu Afrika yote inamtaka Magufuli sisi tunamchukulia poa kwa kuwa ndo zetu waswahili kuponda mtu akiwa madarakani na kumpa hongera akimaliza madaraka yake Albert Einstein aliwahi kusema "tofauti ya ujinga na akili kuwa akili ina ukoma ila ujinga hauna ukomo".

Magufuli akiwangalia mabeberu anaona ushindi ila wapinzani wanaona Tanzania ikitengwa,wanaona bora tuendelee kuliwa kuliko kuwapinga mabeberu,Magufuri anakwea miti mingi kwa wakati mmoja kwakufanya miradi mingi yani anazungumza na kutenda anaposema hapa kazi tu anamaanisha mana nchi haijengwi kwa mikutano na marumbano ya hoja bari wa vitendo gazeti la The Sunday independent la Africa ya kusini liliandika hivi "Africa inahitaji rais kama Magufuli amenonesha nidhamu ya dhani kwa matumizi ya serikali na hapo ndipo liliozaliwa neno la Magufulification for Africa.

Nchi inazizima kwa mwanaume mmoja akifanya ziara za kushtukiza na kufanya tumbuatumbua mpk kupeleka January Makamba kusema "Madaraka ni kama koti la kuazima ukilipata usilivae kwa mikogo" Mzee ameisafisha nchi imesafishika.

Sote tumezaliwa tukiwa wajinga hivyo tunahitaji bidii kidogo tuwe na maarifa au bidii kubwa tuendelee kuwa wajinga Benjamin Franklin alisema tukiamka usingizini tutajua kwann aliitwa Magufurification for Afrika.

Kuna muda kiongozi unahitaji ukichaa kufanyaa mabariko yenye tija. Tupo kwenye Taifa ambalo wasomi na wasio wasomi wanavuruga utulivu wa nchi kwa kusambaza tarifa zisizo rasmi.

Vijana nchi inahitaji Uzalendo.

Copied from somewhere.
 
Watakuponda wengi ukwel Africa itajengwa na waafrika wenyewe ila kuhusu demokrasia na uwazi usibague watu hapo ndipo viongoz wa kiafrika wanapofeli ukiruhuzu haya .utakuwa umefanikiwa
 
Raisi hawezi fanyakazi kwa kufuata propaganda za kale ka kijana kalikotimukia ugaibuni baada ya kukwepa aibu ya kugaragazwa
 
Makala yako ingekamilika kama ungeweka kipengele cha kuwaongelea "Ben Saanane na Azory Gwanda" jinsi maisha yao yalivyozimwa kama mshumaa. Wazazi/Wake/Watoto na Marafiki zao wanatamani hata wangepewa nafasi ya kuwapumzisha kwa amani au lau hata wangepata nafasi ya kuwaaga buriani huku wakiwatazama sura zao zikiwa bila uhai na zisizo na hatia.

Halafu hao unaowaita watetezi wa wanyonge tutakao wakumbuka jinsi walivyochukulia maisha ya hao wahanga kwa wepesi, kana kwamba wale ni wanyama wasio na haki hata ya kupewa ibada ya mwisho.

Sidhani kama unajua uchungu wa mzazi au mke kupotezewa/kuuliwa mtoto/mume wake kipenzi, na kutokupewa nafasi hata ya kuuona hata mwili wake au kaburi lake lilipo.

Omba yasikukute.
 
Kuhusu kichwa cha mada: sijasoma hayo mengine ..., kiongozi huyo huyo na ukichaa wake anaweza pia "kufanya mabadiliko yasiyo na tija"; au unasemaje mkuu 'SheriaE'!
Wakati wana wa Israel wanaelekea kanaani kuna Muisrael alietwa Kora yeye kazi yake kubwa ilikua kupinga safari ya musa na wanawa Israeli. Bila Mungu kuingilia kati kumuangamiza kora huenda mpk leo wanawa Israeli wasingefika kanani.
Na huu mstari wako wa kwanza ni ushahidi tosha kwamba kinyume chake pia kinawezekana. Kiongozi huyo kichaa anaweza kabisa akawa ndiye Kora katika hadithi yako hii.

Je, Mungu ataingilia?
 
Kuna muda kiongozi unahitaji ukichaa kufanyaa mabariko yenye tija . Tupo kwenye Taifa ambalo wasomi na wasio wasomi wanavuruga utulivu wa nchi kwa kusambaza tarifa zisizo rasmi..
LOoo, aisee!

Imenibidi nirudi nisome mada yako huko mwisho ndipo nikakutana na mstari huo hapo juu uliouandika.

Yaani hii ndiyo sababu na msukumo uliokufanya uandike hii mada?

Kiongozi awe kichaa ili watu wasisambaze taarifa zisizo rasmi...!

Hii ndiyo "tija" unayoitafuta kwa kiongozi awe nayo?

Mbona umepotea sana!

Aaah, naomba unisamehe. Nisingejibu kwenye mada yako hii kama ningesoma yaliyomo humo katikati.

Nimemulika harakaharaka nikakuta kumbe ni mada nisiyostahiri kuisoma wala kuijibu.
 
Hujawahi kukaa ukafikiria. Haya yote ni ujinga unaouckia ckia ukaamua kuuchukua na kuja kuuexpose hapa, aibu kwako.
 
Kila siku mnataja na kuimba neno mabeberu. Lakini hamjawahi kutaja hata mfano mmoja tu wa hao mabeberu. Taja nchi moja tu ambayo ni miongoni mwa mabeberu na ambayo sisi hatuna ushirika nayo.
 
Back
Top Bottom